Hapa utazifahamu ibara zote zinazohusiana na elimu. ziko 32 na zimetajwa katika maeneo 25 ya katiba ya jamuhuri ya muungano.
KIFUPI ZIMETAJWA KATIKA MAENEO YAFUATAYO
1. HAKI ZA BINADAMU,WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI
2. HAKI YA ELIMU NA KUJIFUNZA
3. HAKI YA MTOTO
4. HAKI YA WALEMAVU
5. UCHAGUZI WA RAIS
6. UTEUZI WA WAZIRI AU NAIBU WAZIRI
7. UTEUZI WA MWANASHERIA MKUU
8. KATIBU NA NAIBU KATIBU WA SECRETARIETI YA TUME YA UHUSIANO NA URATIBU WA SERIKALI
9. UCHAGUZI WA WABUNGE
10. UCHAGUZI WA SPIKA WA BUNGE
11. UTEUZI WA JAJI MKUU
12. UTEUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA
13. UTEUZI WA MSAJILI MKUU WA WA MAHAKAMA
14. UTEUZI WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
15 MWENYEKITI NA MJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA
16. UTEUZI WA WAJUMBE WA TUME HURU YA UCHAGUZI
17. ELIMU YA MPIGA KURA
18. UTEUZI WA MKURUGENZI WA UCHAGUZI
19. UTEUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
20. UTEUZI MWENYEKITI WA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI
21. UTEUZI WA WAJUMBE WA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI.
22. MAJUKUMU YA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI
23. UTEUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI TUME YA HAKI ZA BINADAMU
24 KAZI ZA TUME YA HAKI ZA BINADAMU
25. UTEUZI WA MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKAR
NA HIZI NDIZO IBARA NA MAELEZO YAKE
HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RIA NA MAMLAKA ZA NCHI
Hii ni ibara ya nyongeza maana haijataja elimu mojakwa moja japo inahusiana moja kwa moja na elimu. Vinamba vidogo havihusiki katika namba za ibara bali ni katika kuhifadhi kumbukumbu ya mara ambazo katiba imetaja elimu.
Ibara 30.
Ibara ndogo (1).
kifungu ( A).
kifungu kidogo( iii).
kila mtu ana haki na uhuru kufanya ugunduzi,ubunifu na utafiti wa sanaa,sayansi na mapokeo ya asili
Ibara ya 41.
Ibara ndogo (2)
1.Kila mtu anayeishi katika jamuhuri ya muungano ana haki ya kuishi katika mazingira safi,salama na ya kiafya,inahusisha haki kwa kila mtu kutumia maeneo ya umma au sehemu mbalimbali za mazingira yaliyotengwa kwa madhumuni ya burudani,
elimu,afya,ibada,utamaduni na shughuli za kiuchumi.
2. HAKI YA KUJIFUNZA
Ibara ya 42.
Ibara ndogo (1)
kila mtu ana haki ya
2 (a) Kupata Fulsa ya kupata elimu bora bila ya vikwazo
3 (b) Kupata elimu bora ya msingi bila malipo na inyomtayarisha kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea na elimu ya ngazi inayofuata au kuweka msingi wa kuanza kujitegemea;
4 (c) Kupata elimu bora inyotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu; na
5 (d) Kupata fursa sawa ya kupata elimu ya juu ili mradi anasifa stahiki kupata elimu hiyo,bila ubaguzi wa aina yoyote.
6 Ibara ndogo ya (2) kwa madhumuni ya ibara ndogo (1),
kila mtu anahaki ya kuchagua taaluma na ajira anayoitaka kwa mujibu wa elimu yake na ujuzi alionao.
HAKI YA MTOTO
Ibara ya 43.-
Ibara ndogo ya (1)
kila mototo ana haki ya –
7 (c) kucheza na kupata na kupata elimu bora
HAKI ZA WALEMAVU
8 Ibara ya 45.-
Ibara ndogo(1)
kifungu (b)
mtu mwenye ulemavu anastahiki kupata elimu kwa kutumia vifaa maalumu na kushiriki katika shughuli za kijamii.
9 Ibara ya 45.
Ibara ndogo1
kifungu cha(d)
Kutumia lugha za alama maandishi na nucta nundu,maandishi yaliyokuzwa au njia nyingine zinazofaa.
10 Ibara ya 45.-
Ibara ndogo (1)
kifungu cha (e)
mtu mwenye ulemavu anahaki ya kusoma, kujifunza na kuchanganyika na watu wengine
11 Ibara ya 46.-
Ibara ndogo ya (1).
kifungu cha (b)
mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha makundi madogo katika jamii: kupewa fursa maalumu za elimu na fursa za kujiendeleza kiuchumi na fursa za ajira.
12 Ibara ya 46.
Ibara ndogo (2)
serikari na mamlaka za nchi zitachukua hatua za makusudi za kukuza na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kuweka miundo mbinu ya makazi ,elimu na afya kwaajili ya kizazi cha sasa na vijavyo vya jamii ya watu walio katika makundi madogo.
UCHAGUZI WA RAIS
13 Ibara ya 79-
Ibara ndogo ya (1)
kifungu cha (e)
mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa na kushika madaraka ya urais wa jamhuri ya muungano ikiwa anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
UTEUZI WA WAZIRI AU NAIBU WAZIRI
14 Ibara ya 101
Ibara ndogo ya (1)
kifungu cha(B)
mtu atateuliwa kuwa waziri au naibu waziri wa serikari ya jamhuri ya muungano ikiwa awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.
MWANASHERIA MKUU
15 Ibara ya 104.
Ibara ndogo (2)
Mtu anayestahili kuwa mwanasheria mkuu atakuwa na sifa zifuatazo,
Kifungu cha (b)
awe Na shahada ya sheria ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.
KATIBU NA NAIBU KATIBU WA SECRETARIETI WA TUME YA UHUSIANO NA URATIBU WA SERIKALI.
16 Ibara ya 112-
Ibara ndogo (2)
kifungu(b)
mtu atateuliwa kuwa katibu au naibu katibu ikiwa ana shahada kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria.(secretarieti ya tume ya uhusiano na uaratibu wa serikali.)
UCHAGUZI WA WABUNGE.
16 Ibara ya 125.
Ibara ndogo (1)
kifungu (b)
Mtu yeyote atakuwa na sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge endapo anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au kiingereza na elimu isiyopungua kidato cha nne.
UCHAGUZI WA SPIKA WA BUNGE.
17 Ibara ya 135.
Ibara ndogo 1
kifungu (a)
angalau awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria.
Uteuzi wa jaji mkuu
JAJI MKUU
18 Ibara ya 158.
Ibara ndogo (3)
Kifungu cha (b)
Mtu ataweza kuteuliwa kuwa jaji mkuu endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka arobaini na tano na mwenye sifa ya uadilifu ,tabia njema na uaminifu na awe na awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika jamhuri ya muungano. Inajirudia kwa naibu jaji mkuu(159)2
UTEUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA.
19 Ibara ya 169.
Ibara ndogo (3)
Kifungu(b)
mtu ataweza kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa mahakama ya rufani endapo atakuwa na sifa zifuatazo. Awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika na mamlaka inayo shughulikia elimu ya juu katika jamhuri ya muungano,na
Vivyo hivyo kwa makamu mwenyekiti wa mahakama ya rufaa.
Sifa hiyo inatumika hata kwa majaji wa mahakama ya rufaa kama ilivyoainishwa kwenye ibara 169.3
MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA.
20 Ibara ya 176.
Ibara ndogo (2)
Kifungu (b)
Mtu ataweza kuteuliwa kuwa msajili wa mahakama endapo atakuwa na sifa zifuatazo:-
Awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika jamhuri ya muungano.
TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA.
21 Ibara ya 180
Ibara ndogo (1)
Kifungu (g)
kutakuwa na tume ya utumishi wa mahakama ambayo itakuwa na wajumbe nane watakaoteuliwa na rais kama ifuatavyo;
wawakilishi wawili wa vitivyo vya sheria kutoka vyuo vikuu,mmoja kutoka Tanganyika na mmoja kutoka Zanzibar watakaopendekezwa na vyuo vya elimu ya juu husika.
MWENYEKITI NA MJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA.
22 Ibaraya186.
Ibara ndogo (3)
kifungu cha(b)
Sifa za mwenyekiti na mjumbe wa tume ya utumishi wa umma zitakuwa kama ifutavyo,
Awe na shahada ya chuo cha elimu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.
MJUMBE WA TUME HURU YA UCHAGUZI.
Mjumbe wa tume huru ya uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
23 Ibara ya 190
Ibara ndogo (6)
kifungu(d).
Awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
ELIMU YA MPIGA KURA.
24 Ibara ya 193.
Ibara ndogo (2)
tume huru ya uchaguzi itakuwa pia na wajibu wakutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi au kura ya maoni na kuratibu utoaji wa elimu ya uraia kuhusu uchaguzi na kusimamia asasi za kiraia,taasisi au makundi ya watu watakaotoa elimu hiyo.
MKURUGENZI WA UCHAGUZI.
25 Ibara ya 195
Ibara ndogo (2)
mkurugenzi wa uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo,
Awe na shahada ya chuo cha elimu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.
26 Ibara ya198.
Ibara ndogo (2).
Kifungu (d)
msajili wa vyama vya siasa atakuwa na sifa zifuatazo,
Awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
MWENYEKITI WA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI
27 Ibaara ya 200.
Ibara ndogo (5)
Kifungu cha (b)
sifa za mwenyekiti zitakuwa kama ifuatavyo:
Mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.hii ni hata kwa makamu mwenyekiti wa tume.
WAJUMBE WA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI.
28 Ibara ya 201
Ibara ndogo (2)
Kifungu cha (b)
sifa za wajumbe wa tume ya maadili ya uongozi na uwajibikaji zitakuwa kama ifuatavyo,
Mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi:
MAJUKUMU MAHUSUSI YA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI.
29 Ibara ya 203.
Ibara ndogo (2)
Kifungu cha (g)
bila kuathili masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1)majukumu mahususi ya tume yatakuwa ni: kutoa elimu kwa umma kuhusu maadili na miiko ya viongozi wa umma.
TUME YA HAKI ZA BINADAMU.
Sifa za mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume zitakuwa kama zifuatazo:
30 Ibara ya 208 .
Ibara ndogo ya (5)
Kifungu cha (b)
Mtu mwenye shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinanchotambulika kwa mujibu wa sheriaza nchi.
KAZI ZA TUME YA HAKI ZA BINADAMU.
Kazi na majukumu ya tume ya haki za binadamu yatakuwa kama ifuatavyo:
31 Ibara ya 210.
Ibara ndogo (1)
Kifungu cha (d)
kufanya utafiti na kutoa elimu kwa uma kuhusu haki za binadamu na utwala bora .
MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKARI
32 Ibara ya 216
Ibara ndogo (2)
Kifungu cha (b)
mtu ataweza kuteuliwa kuwa mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikari ikiwa ansifa zifuatazo:
Amefuzu mafunzo ya juu ya uhasibu na kusajiliwa na mamlaka husika
hiyo ni sehemu tu ya katiba iliyotaja elimu kusoma Rasimu nzima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni