Jumamosi, 15 Februari 2014

VIGEZO 12 VYA KUPATA UDHAMINI WA KIELIMU

Watu wote tunafahamu kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha na ukiikosa unahatihati ya kunyanyaswa na ulimwengu. Hata hivyo imekuwa vigumu sana kuipata kutokana na gharama na ukizingatia wakati wa kusoma mambo ya kifedha huwa magumu au huwa hayawezekani kuyafanikisha kirahisi.Wengi hujikuta wakisoma kwa msaada wa watu wengine wakiwamo ndugu ,walezi ,viongozi wa kidini ,wakisiasa , taasisi mbalimbali zikiwemo NGO’S, serikali nk.
       pamoja na gharama za elimu kuwa juu bado sio sababu ya kuikosa .kwa kuwa kuna njia nyingi za kuipata elimu mradi kama una nia ya dhati.leo nataka niiongelee hii njia ya udhamini ambayo ndiyo inayotumika na wengi katika kujiendeleza au kujipatia elimu.
Kitu cha muhimu unachotakiwa kufahamu ni kuwa elimu ni lazima bila kujali unamudu gharama au la!chamsingi ni kutafuta njia ya kuipata iwe kwa kutumia udhamini au njia nyinginezo.Endapo unataka kutumia njia ya udhamini unatakiwa kufahamu kuwa lazima uwe na vigezo vitakavyofanya uweze kupata udhamini wa elimu yako.
        Bila kukuchukulia wakati tutaangalia vigezo 12 vinavyoweza kumshawishi mdhamini yeyote kuchukua fedha yake aliyoipangilia kwa shughuli nyingine na kuamua kugharamia masomo yako.
Tazama vigezo vifuatavyo ili uweze kuona kama unaweza kuwa navyo kadhaa na kama sivyo uanze kuvijenga sasa.

(1) UFAULU
 Naweza kusema ufaulu ni kigezo namba moja kwasababu wengi wa wanaodhamini elimu hata bila kutazama vigezo vingine huwa wana tumia kigezo hiki kwa sehemu kubwa. Sababu kubwa ya wadhamini wengi kutazama kigezo hiki ni kutaka kujihakikishia kuwa hawatapoteza fedha yao kwa kumgharamia mtu ambaye hatofanya vizuri au kufeli mwishoni mwa elimu yake.kwasababu hiyo ni muhimu kuutafuta ufaulu mzuri ili kukidhi kuingia katika udhamini wa kundi hili.

(2) NIA
hiki ni kitu kingine cha muhimu sana wanachokiangalia wadhamini bila kujali ni ndugu, taasisi au walezi. Na kinachozingatiwa hasa ni nia ya dhati ya kutaka kuendelea kusoma.Bila kujali kuwa unaufaulu wa kiasi gani katika masomo yako bila nia itakayoonekana wazi wazi kwa mdhamini wako ya kutaka kuendelea na masomo ni vigumu kutoa ushawishi wa kutosha kupata udhamini.Inakupasa kuonyesha nia kuwa huna masihara au si majaribio katika uamuzi wa kusoma uliouchukua.


(3) UTAYARI
Utakubaliana na mimi kuwa kunatofauti kubwa kati ya nia na utayari nikiwa na maana kuwa unaweza kuwa na nia na usiwe tayari.kigezo hiki kinaweza kukuongezea nafasi ya kupata udhamini kwa kuwa wadhamini wengi hupenda kujihusisha na watu walio tayari.Utayari huu utaonekana pale ambapo utaonyesha kuwa tayari kuanza masomo hata kwa kupatiwa mahitaji machache .vilevile utayari wako utathibitika pale ambapo utaonekana ukipunguza shughuli zisizoendana na mambo ya kielimu na kuanzisha shuguli zinazoendana na mambo ya kielimu ,mfano kama muda wako mwingi ulikuwa ukiupoteza kwenye; michezo ya pull table,kusafiri kusalimia ndugu ,kutali,kujirusha( starehe),kucheza karata ,bao,drafti,kutazama movie,bongo flavana mengineyo na badala yake ukaanza kusoma ,vitabu ,majarida ,novel,kutazama vipindi vya kuelimisha runingani,kusoma makala zinazoelimisha kwenye mtandao na magazetini,kuhudhuria semina mbalimbali za kuelimisha,na mambo yanayofanana na hayo.

(4) UTHUBUTU
Hiki ndicho kigezo ambacho kinaushawishi mkubwa sana kwa wadhamini wengi wa maswala ya kielimu.Uthubutu unaweza kuonekana kwa kuanza kufanya jambo litakaloashiria moja kwa moja kuwa umekwisha amua kusoma tena unataka kusoma nini.Unaweza kuonyesha hivyo kwa kuchukua form ya masomo kutoka chuo kinachotoa masomo husika au kujiunga na masomo kwenye chuo husika.Hata hivyo unaweza kuthubutu kuanza masomo kwa njia nyingine ambayo si rasmi ilimradi yatakuwa ni masomo asilia ya kile ulicholenga kukisoma.

(5) UWAZI
Mdhamini yeyote hupenda kumdhamini mtu muwazi afanyaye mambo yake katika dhamira iliyo ya kweli.Katika hili ukweli ndiyo kigezo kikuu cha kumshawishi mdhamini kugharamia masomo yako.Itakulazimu kuwa mvumilivu kuruhusu taarifa zako muhimu kuwa wazi kwa anayekudhamini .Taarifa zote zinapaswa kuwa za kweli ili kutojenga mashaka ya kutapeliwa kwa mdhamini wako hasa kama mdhamini si wa familia yako. Kumbuka kuwa kama taarifa zako zitakuwa hazielewekieleweki au ni za uongo itakuwa ni vigumu kwa mtu yeyote kuwa tayari kuhairisha mipango yake kwa ajili ya elimu yako.Epuka kuficha mambo ambayo yataleta wasiwasi kwa mdhamini wako endapo yatagundulika au kujitokeza baadaye.Mfano wa mambo ambayo yanaweza kukuletea matatizo ni pamoja na ;-

*julisha hali yako halisi ya kiuchumi hata kama sio mbaya sana au kama unaye mdhamini mwingine anayeshughulikia jambo flani katika elimu yako.kufanya hivyo hakutakuwa na athali kwako pale endapo mdhamini wako mkuu atabaini uhalisia wa uwezo wako wa kiuchumi.

*julisha gharama halisi za mahitaji yako na gharama halisi za malipo yote ya chuo au shule unayosoma kwa mdhamini wako.Kufanya hivyo kutasaidia kutomsumbua mdhamini wako kubadilisha bajeti ya udhamini mara kwa mara na kukuona kuwa ni kero.Wakati mwingine imewafanya baadhi ya wadhaminiwa kuona haya baadaye kusema ukweli wa gharama walizoficha awali kwa kuhofia kuwasumbua wadhamini wao na kujikuta wakitumbukia kwenye uongo kitu kinachowatia shaka wadhamini wao juu ya matumizi yao .

(6) UNYENYEKEVU
Hakuna mtu au taasisi yeyote inayotaka kumsaidia mtu yeyote asiyeonyesha au asiye na dalili za unyenyekevu.Unaweza kuonyesha unyenyekevu kwa kuchuliana na changamoto zinazotokana na ucheleweshwaji wa malipo kutoka kwa mdhamini au namna yeyote ya maudhi yanayotoka kwa mdhamini.Namna yeyote ya ubishi ,na lugha za kulazimisha zinaweza kumfanya mdhamini kujitoa au kutokuwa na moyo wa kuendelea na udhamini.

(7) TABIA NJEMA
pamoja na mambo mengineyo lakini tabia njema inaushawishi mkubwa wa kumfanya mtu yeyote kudhamini masomo yako bila hata kutumia nguvu nyingi ya ushawishi.tabia njema inaweza kuwa ni pamoja na lugha njema ,ushiriki katika shughuli za makundi mema ya jamii,kuimarisha amani na utulivu katika mitaa unayoishi,kusaidia wenzako kufikia malengo mema,kuwasaidia watu walio na umri mkubwa,kusalimia kwa adabu watu waliokuzidi umri,kutumia lugha ya kistaarabu,mivao ya kimaadili na yanayofanana na hayo.bila kuwa hata na ufaulu wa hali ya juu unaweza kupata udhamini kutoka mahala popote kwa kigezo hiki cha tabia nyema.

(8) BIDII
Bila shaka hata wewe unapenda mtu mwenye bidii.Mdhamini hatatilia shaka kukudhamini katika masomo yako kama tu utakuwa na dalili zinazoashiria kuwa unabidii katika mambo ufanyayo.Epuka kukaa bila kujishughulisha na lolote katika jamii kwasababu miongoni mwao ndimo anamotoka mdhamini wako.Hakikisha kuwa unakuwa mtu wa kimipango na unaisimamia kikamilifu ili kupata majibu yake.Hii inaweza kuwa ni kuazisha darasa la kufundisha watoto na kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri,kuanzisha bustani ndogo ya mboga au matunda mahala unapoisha na kuhakikisha unavuna matunda yake.Azisha kitu hapo mtaani kwako na kukisimamia kikamilifu ili kitoe majibu kitu kitakachofanya kila mtu kukubali kuwa unaweza kujisimamia hivyo hata akikudhamini hutamwangusha.

(9) UVUMILIVU
Mdhamini huwa na furaha zaidi kushirikiana na mtu mvumilivu ambaye anaweza kuyakabili mazingira magumu na kuyamudu .Mazingira magumu yanaweza kujitokeza katika maeneo ya masomo na kusababisha masomo kuwa magumu kiasi cha kuyahairisha.Mtu mvumilivu anaweza kuendelea na masomo hata katika maeneo yasiyo na amani ya kutosha,baridi kali,joto kali,upungufu wa mahitaji, maeneo yenye ubaguzi wa rangi nk.

(10) UMAKINI
Umakini unatakiwa kwa kila mtu lakini kwa mtu anayetaka udhamini wa masomo inaweza kuwa kigezo kikubwa cha kukubalika kirahisi.Mtu anaweza kuonekana kuwa makini endapo atakuwa akipangilia mambo yake kwa ustadi,kukaa katika ratiba ,kutimiza appointment(mfano akiahidi kitu anatimiza kwa wakati,akiitwa anafika kwa wakati),namna anavyoweza kufanya uchaguzi wa vipaumbele vyake;( mfano hachanganyi mapenzi na elimu),anavyoweza kuchagua watu wa kushirikiana nao,anavyoweza kuenenda na wakati;mfano nini afanye wapi na wakati gani nk.

(11) UTULIVU
Unaweza ukahisi kama natoa mafundisho ya kidini lakini huu ndiyo ukweli kuwa utulivu nao ni kigezo cha kumfanya mdhamini yeyote kukukubali.Mtu mtulivu anapendwa kwasababu huwa hana papala akitumia fulsa moja kwa wakati,hujaribu jambo moja mpaka mwisho kabla ya kuhamia katika jambo jingine,hutafakari kila jambo analotaka kulifanya kabla ya kuchua hatua,huwa hana hadithi mbaya ya maisha yake (haambatani na matukio ya skendo ) shida zake huzifahamu watu wachache aliowachagua yeye.

(12) KIPAJI
Kwa kiwango kikubwa wadhaminiwa wengi wanavipaji na vimekuwa ndiyo kigezo kikubwa cha kupata udhamini wao.Ili mtu aweze kuonekana wa pekee ni namna anavyotumia kipaji chake katika maisha yake ya kila siku.Kadili kipaji kinavyokuwa ndivyo upekee unavyozidi kuonekana na kuzidi kutambulika na watu.Unaweza kutambua kipaji chako na kukitumia katika maisha yako ya kilasiku na si punde tu.Kipaji kikidhihirika kinaweza kukufanya kuwa bidhaa adimu.Kwa kuwa watu wote hupenda bidhaa adimu hivyo hawataacha ipotee bure,nawe unaweza kutumia kipaji chako kuwavutia watu kukudhamini katika masomo yako.Kama hujui kama unakipaji gani unaweza kutembelea kwa kubofya hapa  ambapo utaona kurasa inayosema( nifanye nini kabla ya kujiendeleza kielimu) kisha utatazama katika kipengele cha ( utatambuaje kipaji chako.)

Maoni 12 :

  1. Naitwa Samson Samwel nipo chuo Mwaka wa 2 faculty- Allied Healthy Science(Certificate of Medical Laboratory) natafta mdhamini wa kunidhamini niweze kumaliza elimu ya chuo kwani nyumbani hali sio nzuri ya Maisha( Hali duni)

    JibuFuta
  2. NIFANYEJE KUPATA MDHAMINI?

    JibuFuta
  3. Mimi natafuta mdhamini wa kimasomo nina nia sana ya kusoma na kutaka kutimiza vission yangu

    JibuFuta
  4. Natafuta udhamn wa masomo ngaz ya diploma kwa ICT

    JibuFuta
  5. Wapendwa mimi napenda sana kufundisha watoto wadogo wa chekechea ila sina ada ya kulipia chuo. Nisaidieni wapendwa Wa Mungu. Nifanikishe malengo yng

    JibuFuta
  6. Naitaji msaada wakusomeshwa katika ngazi ya diploma

    JibuFuta
  7. Mimi mwenyewe naomba msaada wa masomo

    JibuFuta
  8. Kwa jina naitwa sitta s mangu no mwanafunzi wa chuo cha serikali za mitaa hombolo nipo level 5 course ya maendeleo ya jamii nahitaji kupata uzamini was kuniwezesha kuhitimu masomo yangu ngazi ya diploma kwa mawasiliano wasiliana nami kwa namba 0627112584/

    JibuFuta
  9. Naitwa maria sanga nimefanikiwa kumaliza certificate of community health workers Ila ningependa kuendelea na masomo ya diploma of social work kwa huu mwaka 2022 Ila Sina ada ya kuendelea na masomo yangu ivyo ninaomba mfadhili au mdhamini wa kunisaidia kuweza kutimiza lengo langu asantee...No 0655289368

    JibuFuta
  10. Kwa Majina naitwa STELA MWASEMBE nahitaj mfadhili wa kunisomesha

    JibuFuta
  11. Nawezaje kupata ufadhili

    JibuFuta
  12. 0675676575
    Tafadhari
    Naomba
    Udhamini
    Wa
    Masomo
    Nimemaliza
    Kidato
    Cha
    Sita

    JibuFuta