Alhamisi, 24 Aprili 2014

TUACHE UNAFIKI TWENDE SERIKALI MOOOJA.



WEWE Zanzibar unalalamika kuwa mambo ya muungano yanazidi kuongezeka hivyo kuondoa utambulisho (identity) wako .

Swali linakuja kuongeza mambo ya muungano na kupunguza kupi ni kuimarisha muungano?

 katika muungano kupoteza ni lazima ndugu yangu. Hata TANGANYIKA amepoteza vingi  mpaka akafa ndiyo maana unamuona huyo mjomba wenu TANZANIA anamsimamia mambo yake.

kama kila mtu akitaka kung’ang’ania chake ndugu yangu hakuna muungano.Naomba ujitafakari usije kuwa umeanza safari, lakini safari yenyewe ikawa ni kurudi nyuma.Leo ZANZIBAR ukiogopa kumezwa na TANGANYIKA ambaye ni mzimu tuu, ukitoka nje  hautamezwa? ni dhihili kuwa utamezwa na dunia.

Kwa hiyo kitu unachotakiwa kutafakari  ni kwamba, ama uendelee kuutukuza UZANZIBARI na kumfufua binamu yakoTANGANYIKA. Akishafufuka mjadiliane pamoja na Mjomba wenu TANZANIA kupunguza mambo ya muungano  ili asikumeze. Lakini wakati huohuo jiandae kumezwa na dunia.

Najua utasema siwezi kumezwa kwasababu una ndoto.Kama unandoto za kula vizuri na kunenepa kuwa kama  HONG KONG miaka ijayo  ili kuwini uchumi wa dunia.Na kama hiyo ndiyo sababu inayokufanya udai serikali kamili!!.

Basi huyo TANGANYIKA unayemfufua, yeye unayemwogopa akali yu kaburini miaka hamsini huku wewe ukijipasua kwa mizinga 21,bendera,wimbo,nk.Sasa mwenzako atakula sahani moja na wewe,na baada ya miaka hiyo unayohesabu wewe kuwa na tumbo kama HONG KONG, yeye atakuwa na tumbo kama AMERIKA.

Kivyovyote vile safari hii TANGANYIKA hatakua na mchezo,  atakumeza na hatokupa nafasi tena kama ilivyokuwa mwanzo alipokuwa akikumeza kimaluweluwe usishangae, yaani kimzimu mzimu.

Hizi ni salamu zangu za miaka hamsini ya muungano, tutafakari  TANZANIA yetu. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUUNGANO WETU.

Jumanne, 15 Aprili 2014

MAMBO 5 YA KUFANYA KWANZA UFIKAPO CHUO AU SHULE

1.ONYESHA MSIMAMO WAKO KABLA WENZAKO HAWAJA KUONYESHA WA KWAO



Kufanya hivyo kutakusaidia kukutambulisha kuwa wewe ni mtu wa aina gani na unakubaliana na nini.Mara nyingi watakaokufahamu kwa mara ya kwanza watalazimika kufuata msimamo wako.

Wale wenye tabia ya utani,dhihaka,na mambo mengine ya masihara watajifikiria mara mbili kukuanza endapo watagundua kuwa wewe ni kinyume chake.Kuchelewa kuonyesha msimamo wako kutakufanya baadaye kuwa mtumwa wa kuanza kutengeneza msimamo mpya wakati wenzako watakapokuwa wameshazoea kukuonyesha misimamo yao.

2.KUWA TAYARI KUPOTEZA

Mara baada ya kuonyesha (consistence) yaani usiyebadilika unaweza kuingia katika janga la kupoteza baadhi ya vitu.Kitu cha kwanza utapoteza idadi kubwa ya watu watakaokuwa karibu na wewe.Hilo ni kutokana na watu wengi kupenda kuwa karibu na watu wenye misimamo rahisi .”Hata wewe bila shaka unapenda kuwa karibu na mtu anayekubaliana na wewe kwa kila kitu unachotaka au unachofanya”.Utakosa baadhi ya fursa kutokana na kuwa na idadi ndogo ya fans nk.Lakini hali hii itakusaidia kukuhakikishia kuwa kila anayekuja kwako iwe kwa urafiki au kivyovyote vile anakubaliana na msimamo wako.

2.USITAFUTE  MARAFIKI ACHA WAJE WENYEWE

Hapa naomba nisisitize kuwa,marafiki wa shule/chuo wa moja kwa moja (direct contact friends) sio kama marafiki wa facebook na twitter ambao unaweza kuwa nao hata maelfu na wasikusumbue. Hawa ni watu wanaokuona kwa uhalisia wako,wanafahamu kilakitu kuhusu wewe. Wanajua uwezo wako, udhaifu wako,siri zako,na mipango yako.Na kibaya zaidi si kila binadamu ni salama kwako.

Wapo wanaopenda wakutumie kwa faida zao na imekwisha.Wapo watakaotaka ufuate kila wanachotaka.Wapo wasiopenda kuona unamzidi kwa chochote.Kuna mambo lukuki ambayo hata wewe unayafahamu kuhusu binadamu.

Acha rafiki wa kweli aje mwenyewe.Rafiki wa kweli ni Yule anayekubaliana na hali yako halisi sio ya ki-Facebook na twitter.Kufanya hivyo kutakusaidia kuwa na rafiki ambaye hatokuwa mzigo,kero wala kikwazo katika safari yako.

3.JIWEKE MATAWI YA CHINI HATA KAMA UKO JUU

Heshima tamu ni ile unayoheshimiwa bila gharama yoyote.Ili kujipatia heshima ya kweli basi jifanye huna haja nayo ukiitaka umeipoteza.Kumbuka kuwa kila mtu anapenda kuheshimiwa.Na hakuna mtu anayepoteza muda wake kujenga heshima ya mtu mwingine.Kitendo cha kujifanya u matawi ya juu kitawafanya wenzako wajione si kitu.
 kwasababu hawatapenda kujiona si kitu wataichukia tabia yako,wakiichukia tabia yako watakuchukia hata wewe.Bila shaka umeshawahi kuona mtu anayestahili heshima lakini wala hakuna anaye mtetemekea.Wengi wao utagundua ni kutokana na tabia zao za kujifanya wako juu hata kama ni kweli wanauwezo.

4.SOMA  (STUDY) TABIA ZA WATU

Katika kipindi cha kwanza kabisa unatakiwa kusoma tabia za watu kabla ya kufanya nao chochote. Unaweza kufanya hivyo kwa kujaribu kuwasiliana na kila aliyekaribu nawe bila kuonyesha nia ya kuhitaji ukaribu.

Ni rahisi sana kuchukuliana na watu kama unafahamu tabia zao.Kufanya hivyo kutakusaidia kuwafahamu watu wasumbufu na wale wenye manufaa kwako.Wale wakorofi,wanafiki,wezi na tabia nyingine hatarishi utawatambua katika kipindi hiki.

Usipowatambua watu ni rahisi kukubadilisha au kukuingiza katika matatizo.Matatizo hayo yanaweza kuwa ni pamoja na kufukuzwa shule au chuo au hasara ambayo hutaweza kuirejesha.Matatizo hayo ni pamoja na ugomvi,wizi,ulevi,ulaghai na mengineyo.

5.KUWA MTULIVU KWA KILAKITU

Kipindi cha mwanzo watu kukutana katika mikusanyiko haswa ya kishule, huwa na kawaida ya kila mtu kutaka kuonyesha yeye ni nani.Pia katika kipindi hiki Kila mtu huwa na pilika pilika za hapa na pale haswa kwa wale wanaoishi katika maeneo ya hostel au kwenye nyumba za pamoja.Jitahidi kuvuka katika kipindi hiki bila kuchukuliwa na upepo wa pilika pilika hizi .

Kama utamudu kubaki katika utulivu huo itakusaidia kubaki na taswira ya aina moja tu ya elimu kichwani mwako.Fahamu kuwa kitendo cha kushughulika na mambo mengi hapa mwanzoni, kunaweza kuruhusu mambo mengine nje ya elimu kuanza kuchukua nafasi moja kwa moja katika ufahamu wako.Na endapo kama yatakuwa na nguvu ya kutosha basi,yanaweza kufanya swala la elimu kukaa katika nafasi ya pili.









Jumapili, 13 Aprili 2014

JINSI YA KUSOMA KWA KUSIKILIZA UKITUMIA ADOBE READER




Hatua ya 1.

Install adobe Reader kwa wale wasio na program hii kwenye Computer zao.
Ni vyema ku install toleo jipya zaidi .unaweza kudouload kutoka kwenye mtandao au kutoka kwenye kifaa chochote kilichohifadhi program hii.Unaweza kujipatia program hiyo bure mfano kwenye Link hii.    http://www.adobe.com/products/reader.html

Hatua ya 2

Badili format ya faili zako kuwa katika mfumo wa PDF file ili uweze kuyafungua kwa kutumia program hiyo.Somo hilo sio mahala pake tutalizungumzia kwenye mada yake.

Hatua ya 3

Fungua faili yeyote yenye format ya PDF Kwenye Computer yako.Mfano





Hatua ya 4

Katika menyu bar ya faili lako bofya ( View )





Hatua ya 5

Kwenye Drop down menyu itakayotokea elekeza poiter (kamshale)  yako kwenye Highlight (Read out loud) Itakayofungua drop down menyu ndogo.





Hatua ya 6

Kwenye drop down menyu ndogo bofya (Activate read out loud) Kuwezesha program kuanza kusoma faili lako.




Hatua ya 7

Bofya mara mbili mwisho wa  herufi,neno,sentence,paragrafu,au hata ukurasa na neno hilo au ukurasa huo utazungushiwa kingo kisha moja kwa moja utaanza kusikiliza 
kilichoandikwa.



Mfano mwingine



Hatua ya 8

Kama hutapenda kuendelea na kusikiliza rudi tena kwenye menyu kisha utakapo elekeza pointer (kamshale) yako kwenye Read out loud utaona maelekezo kwenye Drop down menyu ndogo kama ifuatavyo.kisha chagua unachotaka ikiwa ni,

kusitisha Deactivate Read out Loud ,
kusoma ukurasa Read this page only,
kusoma document nzima  Read To End of Document,
Kustop au Kusimama kwa muda, Pause and Stop



Hatua ya 9

Unaweza kutumia kicharazio chako (keyboard) Kwa kufuata maelekezo yaliyo katika picha baada ya Ku activate program.


Nakutakia usomaji mwema.kama unamaoni au swali usisite kuandika katika mwisho wa mada hii karibu.



Alhamisi, 10 Aprili 2014

MBINU ZA KUJITAMBUA

Kwa kifupi naweza kusema kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu wa nini kuhusu wewe.Hali yako,umuhimu wako,malengo yako,hatima yako, changamoto zako, nk, hayo yote yanakuwa wazi kwako kwa kujitambua.
Dhana ya kujitambua kwa zama za sasa imekuwa kama kengele ya kanisa au azana ya msikiti, kwa jinsi ambavyo hutamkwa mara kwa mara.Sasa yatosha kwa jinsi tulivyoisikia,leo nataka tuje na kitu kipya kama kilivyoelezwa katika kichwa cha mada yetu.
Sipendi kukuchukulia muda wako naomba niingie moja kwa moja kwenye mada

1. PIMA UMRI NA KIWANGO CHA FIKRA ZAKO

Sote tunafahamu kuwa hakuna kiwango maalumu cha kufikiri kilichoidhinishwa kimataifa kutoka umri mmoja na mwingine. Bali tunaviwango vya kimataifa vinavyotoa uwiano wa umri wa mtoto na kuandikishwa shule.Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupima kiwango cha fikra zako kwa kulinganisha na umri wako.

Unaweza kupima fikra zako kwa kutazama ubora wa matokeo ya kila unachoamua kutenda pasipo kusaidiwa na mtu mwingine.Pia unaweza kupima fikra zako kwa kuzilinganisha na ubora wa fikra za watu wenye kiwango cha juu cha fikra katika umri wako. Lakini mwisho wa yote viwango bora kabisa vya kifikra vinalenga juu ya usahii wa wakati katika kutekeleza jambo fulani.

 Unaweza kupima jinsi unavyopanga,unavyoamua,unavyotekeleza, na kuendelea au kusitisha maswala fulani fulani katika maisha yako na aina ya matokeo unayoyapata kwa kuzingatia ubora wake.
Kwa kufanya hivyo itakusaidia kuanza kupata picha ya namna gani unajitambua.

2. TAFUTA KUJUA UPEKEE ULIONAO

Hii nayo ni kati ya mbinu bora inayokufanya ujitambue.Watu wengi hupenda kufanana na watu fulani fulani haswa watu ambao wao huwaita role model (mtu wa mfano),Na kusahau kuwa yeye ndiye role model na.1 kwake binafsi.Makosa haya humpelekea mtu huyo kujua zaidi kuhusu huyo role model na.2 na upekee wake kuliko anavyoweza kujifahamu mwenyewe.

Leo imekuwa ni kawaida kumsikia mtu akieleza kwa ufasaa upekee alionao OBAMA na MKEWE lakini ukimuuliza upekee alionao akakujibu kirahisi tuu sijui.Kitu pekee kitakachokuokoa na tatizo hili ni kuamua kufahamu upekee ulionao na si upekee wa mtu mwingine au Role model wako.

Kama wewe ni mwandishi wa vitabu jiulize unatofautiana nini na waandishi wengine,au kama ni mwanafunzi,mwanasayansi,mchezaji,mwanajamii, nk, unatofauti gani na wengine ukiwa na maana uthamani wako uko wapi zaidi.

3. TAFUTA KUJUA CHANGAMOTO ZINAZOKUKABILI

Kama kweli umedhamiria kujitambua unatakiwa kufahamu changamoto au matatizo yanayokukabili.Changamoto hizo zinaweza kuwa ni zile zinazotokana na rika ,mazingira ,kiwango cha elimu yako,Hali uliyonayo (ulemavu, mahitaji maalumu au uathirika wa magonjwa,ndoa,bila ndoasingle nk. ).

Kama ni rika tambua rika lako linakabiliwa na changamoto zipi.Ikiwa ni mazingira tafuta kujua changamoto za kimazingira ulizonazo.Unaishi kijijini ,mjini,shuleni,chuoni,mfanyakazi,kiongozi,mfuasi au vinginevyo ,jiulize katika mazingira hayo unakabiliwa na changamoto gani. Inawezekana wewe ni teenager (13-19 miaka) au kijana au mzee, jiulize kuhusu changamoto zako.Vivyo hivyo kwa kiwango cha elimu pamoja na hali kama ilivyofafanuliwa katika mabano.Orodhesha changamoto zinazokukabili.

Kumbuka hata uonevu wa kibinadamu wa kawaida hutokea zaidi kwa watu wasiozingatia kipengele hiki cha ufahamu wa changamoto. Hakikisha unafahamu wapi utakwama kabla hujafikia na kuanza kuchukua hatua mapema iwezekanavyo.kitendo hicho kitakufanya uwe macho saa zote na kila atakayekuona atakuthamini hivyo kutokuwa na madhara kwako.

4. TAFUTA KUJUA WAJIBU NA MAJUKUMU YA WATU WA RIKA LAKO

Kwa haraka unaweza kufikiri kuwa nataka kufundisha uraia.Utanisamehe kama nitakuwa nimekukumbusha kitu unachoimba au ulichoimba kilasiku shuleni.Lengo langu nataka nikufumbue macho kuhusu wajibu na majukumu kama dhana muhimu katika kujitambua.

Mfano; mama mmoja alikuwa akilia kwa uchungu nje ya nyumba yake huku akijitupatupa chini na kugalagala.Majirani wakaja mbio na kukusanyika kufahamu kilichotokea.Lakini kila walipomuuliza mama alichokua akililia aliwaonyesha kidole katika mlango uliokuwa wazi.

Watu wakakimbilia ndani na kumkuta mtoto wa miaka minne na nusu aliyewekewa kila kikorokoro cha kuchezea lakini hakuna alichokishika wala kukichezea. Walipotoka na kumuuliza mama mbona hatukuona chochote zaidi ya mtoto na vitu,mama akaongeza kilio na kusema “masikini mwanangu asala gani hii! huyu ni mwanangu watatu ,wenzake waliotangulia walikufa kwa moto shambani kwasababu hawakuweza kusogea hata hatua moja moto ulipotokea nilipokuwa kisimani kuteka maji.kinachoniumiza zaidi ni kuona hata huyu naye hagusi chochote nilichomwekea nahisi naye atakufa kifo kama cha wenzake”.

Kwa mfano huo tunapata picha ya mtu asiyetambua wajibu wake anavyoweza kuleta hasara kubwa kwake yeye mwenyewe ,kwa familia yake na kwa taifa lake.Mama aligundua kuwa mtoto wake hajitambui kwa kutonyanyua chochote.majukumu ya msingi ya mtoto wa umri ule ni kucheza.Kutokucheza ilikuwa ni ishara tosha ya kutokujitambua.
Jiulize kama wewe ni mmoja wa wale wasiowajibika?.

Piga picha na kuyatazama majukumu yako kama mtoto,kijana,au mzee.
Jiulize kuwa wewe ni Yule mtoto mwenye kila kilicho mbele yake lakini hakuna anachogusa?.
Jiulize kuwa umekuwa mtu wa kunyooshea vidole majukumu au umekuwa mstari wa mbele kutumikia?.
Umewahi kushiriki kutatua kero yeyote nyumbani kwako ,mtaani kwako au maeneo yaliyokuzunguka?
Jiulize unafanya nini katika kujiandaa kutumia fursa zinazojitokeza duniani?
Nafasi uliyonayo unaitumia kufanya wengine kuinuka au unawadidimiza?
Jiulize kama wewe ukikosekana duniani, dunia itakuwa imepata hasara yeyote?

Wakati unajiuliza maswali hayo ni wazi kuwa utaanza kupata picha ya jinsi ulivyo kwa kupima uwajibikaji wako.Kitendo kicho kitakufanya uongeze uelewa wako juu yako binafsi na kwasababu hiyo utaingia kwenye kundi la watu wanaojitambua.

5. PIMA KUJIAMINI KWAKO
Ili kujitambua inakupasa kuchukua jukumu hili msingi la kupima kujiamini kwako.Hebu jichukue katika fikra zako na kujiweka mbele ya umati mkubwa wa watu wenye uelewa wa kutosha.Jaribu kuwaelezea au kuonyesha kitu ambacho unakifahamu kwa usahihi kabisa hapa duniani.Unahisi unaweza kukifanya kikamilifu bila hofu wala kubabaika.

Unaweza kujikumbusha mambo ambayo yalikuwa yanakufanya ushindwe kujiamini kama bado yapo au la.
Pima ubora wa unachofanya kama una nafasi yeyote katika viwango vya kidunia?.
Kama wewe unajihusisha na sanaa je sanaa yako inaweza kumvutia mtu yeyote duniani?.
kama ni huduma je! huduma yako inaweza kumfaa mtu yeyote duniani?
Kama ni mwanafunzi je wewe unaweza kuwa mwanafunzi bora popote duniani au ni hapo kijijini kwako tu?.
Unaweza kushindanishwa na mtu yeyote duniani kwa hilo ambalo wewe ni bora sana hapo kwenu au ubora huo ni wa hapo kwenu tu?.

Kwa vipimo hivyo vitakufanya uzidi kujitambua na kuchukua hatua ya kuondosha mapungufu uliyonayo na kukufanya uzidi kujiamini.

6. WEKA VIPINDI MAALUMU VYA KUJITATHIMINI
Kitendo cha kujitathimini kitakufanya kujichunguza na kujiweka karibu na wewe binafsi.Tatizo kubwa tulilonalo leo duniani ni kwamba tunawatu wengi ambao wako karibu sana na watu wengine lakini hawako karibu na wao wenyewe. Kifupi ni kwamba wanajua sana kinachoendelea kwa watu wengine kuliko kinachoendelea kwao binafsi.
Wanalaumu watu hawana elimu wakati wenyewe hawana,
Wanatetea unyanyasaji wa kijinsia wakati wao wenyewe wananyanyaswa,
Wanalaumu watu wanaovunja ndoa wakati wao wenyewe wana nyumba ndogo,
Wanalaumu kuhusu wizi wa viongozi wa umma wakati Wao mwenyewe wanaiba kwenye kampuni zao.

Sasa,kitu ambacho kinaweza kusaidia katika kujitambua ni kufanya tathmini binafsi juu ya mwenendo wako.Kabla hatujaanza kukosoa uzembe wa watu wengine tenga vipindi maalumu ikiwa ni kila baada ya wiki,mwezi au mwaka kutathimini ni uzembe wa namna gani umefanya na matokeo yake.Hata hivyo unaweza kufanya tathimini za kila siku ili kutokuwa na mlundikoano wa tafakuri za muda mrefu kuhusu namna ulivyoishi.

Unaweza kutathimini kiwango cha mafanikio kwa kulinganisha na matarajio,kiwango cha mapungufu kwa kwa kulinganisha na namna ulivyoshindwa.Kama mafanikio hayakufikia malengo basi ni wazi kuwa bidii na mbinu bora zaidi zinahitajika na kama matokeo ni kushindwa basi ni wazi kuwa mfumo mzima wa maisha inabidi ubadilike na mbinu mpya zinatakiwa.

Kiwango cha kujitambua kinaendana na tathimini binafsi. Ni kiwango cha hali ya juu cha kutojitambua kuendelea na kazi ileile au mbinu ileile inayokufanya kilasiku ushindwe kutimiza malengo yako.Kila baada ya tathimini lazima uje na mapendekezo mapya yenye mbinu mpya ,mikakati mipya na matarajio mapya.Kwa kufanya hivyo ni dhahili kuwa kiwango chako cha kujitambua kitakua na kuongeza mabadiliko ya kila siku katika maisha yako.

7. KUBALI KUANZA UPYA

Bila kujali wasifu ulionao unaweza kuonyesha kiwango cha kujitambua kwako kwa kuanza upya mara tu unapobaini kuwa kunamakosa makubwa katika mwenendo wa maisha yako.mtu mwenye kiwango cha chini kabisa cha kujitambua hawezi kuanza upya .kwasababu ya kutojitambua kwake haoni shida kwa lolote limpatalo na kuhisi kuwa amestahili.

Mtu asiyejitambua haoni umuhimu wa kubadilisha mtindo wa maisha kwasababu hufikiri kuwa kufanya hivyo ni sawa na kupoteza wakati.Inashangaza sana kumwona mtu anatumia staili ya aina moja katika kupambana na changamoto ambazo kila siku zinabadilika.

Jenga tabia ya kukubali kuanza upya kila unapoona kuwa hatua ya kiwango cha makosa ulichofikia hakiwezi kurekebishika.mfano ,kama pengine fani unayoitumikia haiendani kabisa na kipaji ulichonacho kubali kuanza kujifunza fani nyingine.Na endapo marafiki ulionao wanakusababisha kushindwa kutimiza majukumu yako, kubali kuanza kutafuta marafiki wapya.

Kitendo cha kukubali kuanza upya kitakufanya kujitambua. Utakapoanza awamu ya pili itakusaidia kubaini makosa uliyoyafanya mwanzo na kwasababu hiyo kuwa mwalimu wa wengine.

Kupitia mada hii bila shaka utakuwa umepata uelewa mkubwa sana kuhusu mbinu ya kujitambua na sasa unaweza kuwa na mchango mkubwa kwako na kwa jamii yako.

Jumanne, 8 Aprili 2014

MAMBO MATATU YA KUEPUKA


Najua wewe ni rafiki yangu,kaka yangu ,ndugu yangu,nk.Kutokana na hilo sina budi kukushirikisha katika mambo ambayo kidogo nimeyaona kuwa yanahitaji taadhari ya hali ya juu kidogo.

1. EPUKA FASHON MPYA IJULIKANAYO KAMA ADULT BABY (INFANTILISM)
Japo ukiwauliza wanasaikologia kuhusu Infantilism watakupa majibu tofauti sana na hiki ninachokwenda kukizungumza.Lakini cha ajabu sana tatizo hili limegeuzwa fashion.

Fashion hii ya mtindo wa maisha imeanza kupata umaarufu katika miaka ya hivi karibuni.kama tafsiri ya neno hilo la kiingereza lilivyo infantilism linalotokana na neno INFANT lenye maana ya mtoto aliye katika umri mdogo kati ya miaka 5-7, Ni kwamba mtu huyo anajizoeza kuishi kwa kutumia tabia za watoto wa umri huo.Kitendo cha kuishi kwa kutumia tabia za watoto wa umri huu mdogo ndicho kinachoitwa INFANTILISM.

Katika maisha haya mtu hutumia staili zote za maisha za mtoto mdogo. wengine wamekwenda mbali zaidi hata kuvaa pampers za watoto kama unavyoweza kuona katika picha hizo hapo chini.



Kama unataka kuona picha zaidi unaweza kutembelea link hii http://www.oddee.com/item_98448.aspx&sa=U&ei=tvBQUYCgFqTA0gH9poGwCg&ved=0CC0QFjAF&usg=AFQjCNFmXyNGg5MHWQggOc9PipmuEtVDxA.Hata hivyo baadhi ya mitandao imehamasisha maisha hayo kwa kutoa hata mbinu kama ilivyo katika mtandao wa KNOW HOW ( http://www.wikihow.com/Act-Like-a-Baby-Again)

Sababu za kufanya hivyo ni nyingi kutegemea mtu na mtu.Lakini wengi wao wamekuwa wakidai kuwa kufanya hivyo imewapunguzia bugdha za kimaisha kwa kuwa maisha yamekuwa Very complicated (yanasumbua) vitu vinapanda bei ,tecknologia inaongezeka,uzazi unasumbua,nk ambapo binadamu anahitaji kufanya kila linalowezekana ili kwenda sawa na dunia.

Wengine wamedai kuwa wanaofanya hivyo ni kutokana na namna walivyo,yaani ni watu ambao wana hurka ya kupendelea zaidi maisha ya kitoto na hufurahia zaidi kuishi maisha hayo kuliko maisha ya kiutu uzima .

FAIDA. Kuenjoi maisha bila msongo wa mawazo hasa kwa zama hizi za maisha ni pesa.

HASARA.
A. KUENDELEA KURUDI NYUMA KIFIKRA.
Najua miongoni mwetu wapo wanaopenda kuiga mambo bila kutafakari kwa kina.Binadamu lazima awajibike kujibu maswali yote magumu asipofanya hivyo hakuna mtu mwingine wa kufanya hivyo.

Tusikubali kukaa na wanyonyaji hawa katika dunia hii.Hawataki kufikiri,hawataki kushiriki kujibu maswali magumu,Hawataki kuzaa,Hawataki kushirikiana na watu waliopevuka na Hawana mchango mkubwa kiuzalishaji.

Kama kila mtu akitaka kuwa Adult baby nani ataendeleza dunia wakati wote tutakuwa tumeshikilia chupa za kunyonyea maziwa mdomoni na kuchezea midoli. Napendekeza watu hawa tuwaambukize fikra zilizopevuka wawe na mchango duniani.

B. UCHUMI WA DUNIA KUANGUKA
Tukumbuke kuwa dunia inamzigo mkubwa sana wa kubeba, kama tusipokuwa makini utatuangukia na kutudidimiza milele kwa kuwa hakuna kiumbe kingine chenye uwezo zaidi ya binadamu isipokuwa Mungu.Na Mungu kwasababu hakututuma kufanya ujinga huu hatowajibika kwa lolote.

Mzigo ninaouzungumzia hapa ni wa wagonjwa,walemavu wa aina zote madawa ya kulevya,akili,viungo,nk.Mzigo mwingine ni watoto,wazee,watu wasio na elimu,masikini nk.

Katika mtandao unaofahamika kama WORD DISABLED (http://www.disabled-world.com/disability/statistics/) umewahi kutoa tasmini ya walemavu kufikia kiasi cha milioni 650 katika nchi zinazoendelea duniani.Hiyo ni sawa na asilimia 10 ya watu wote duniani ambayo ni bilioni 7.

Kwa mujibu wa mtandao huohuo katika kila watu 5, 1 ni mlemavu kwa marekani peke yake. Na kwa mujibu wa social security administration ya inchini humo kuwa 33% ya wamarekani watakuwa na ulemavu wanapofikisha umri wa miaka ishirini kazini (http://www.disabled-world.com/)

MZIGO MWINGINE NI WAZEE .Huu ni mzigo wa kudumu ambao kwa mujibu wa taarifa za tar 8/april 2014 za mtandao wa 

http://www.telegraph.co.uk/earth/greenpolitics/population/5872109/Worlds-elderly-to-overtake-number-of-infants.html 

wazee wa umri wa miaka isiyopungua 65 wanakadiriwa kufikia Bilioni 1.3 miaka arobaini ijayo.Na wazee wa umri wa miaka zaidi ya 85 idadi yao ndiyo inayoongezeka haraka kuliko idadi ya watu wengine wowote.

Ukumbuke kuwa hawa wazee huhitaji Pension,matibabu na huduma nyinginezo.

WATOTO
Hawa nao ni mzigo kwa mujibu wa takwimu za benk ya dunia mwaka 2012 watoto chini ya umri wa miaka 15 ni asilimia 26 ya watu wote duniani sawa na bilioni 1 .82 ya watu wote .

Na kwa taarifa tu ni kwamba uzazi unaongezeka kwa kasi sana hasa kwa nchi za afrika ;inakadiriwa ifikapo mwaka 2050 idadi ya waafrika itakuwa mara mbili ya ilivyo hivi sasa ambapo inakadiriwa kufikia bilioni 2.4 . 

Tazama WORLD DATA SHEET  http://www.prb.org/Publications/Datasheets/2013/2013-world-population-data-sheet/data-sheet.aspx

Watu wenye umri wa kufanya kazi kati ya vijana na wazee duniani kwa mujibu wa WORLD BANK ni 52% sawa na watu billion 3.64 ambao katika nchi kama United Arab Emiretes yenye watu zaidi ya milioni 92 wanao fanya kazi ni 17% sawa na milioni 15.64.

Jiulize swali bado tunahitaji kuongeza mizigo mingine ya kujitakia? HATUHITAJI WATU WANAOITWA ADULT BABIES.

2. EPUKA KITU KINACHOITWA SECOND LIFE
Hii ni dizaini mpya ya maisha inayopata umaarufu sana duniani .Na imetumika kama sehemu ya kufanyia RECREATION (MAPUMZIKO YA AKILI) .Maisha haya ni ya kielektronik yanayoendeshwa kwa kutumia program za kompyuta.

Program hizi huwekwa kwenye internet ili mtu aweze kuzitumia atakavyo.Mtu anaweza kuanzisha familia yake mpya itakayokuwa na maisha ayatakayo ikiwa ni ya kijijini au mjini ,vilevile anaweza kuifanya ikawa ni familia nusu mnyama na nusu binadamu.

Katika maisha haya unaweza kuchagua kuwa singo au mtu uliye na mpenzi au mke.Pia zimeanzishwa programu za wanafunzi ambazo si maarufu sana.

Katika program hizo unaweza kubuni makazi na kila kitu unachokitaka kwaajili ya maisha yako au pengine na familiya yako .Kwa kutumia internet unaweza kuishi humo na kufanya kilakitu ambacho ungefanya katika maisha yako halisi kwa kutumia picha za kiwango cha hali ya juu na sauti zilizomo katika program hizo .

MADHARA.
A. Programu hizi zimekaa kimapenzi zaidi hivyo zitakufanya kufikiria ngono kila wakati.
B. Zinaweza kuvunja ndoa yako kwa kuhamisha fikra zako kwenda second life.
C. Zitakuchukulia muda wako wa maendeleo
D. Zitakuondolea uwajibikaji kwa kupenda kuishi maisha ya pichapicha tu.

3. EPUKA KUBEBA MIDOLI (TOYS )
Huu ndiyo mtindo wa zamani zaidi wa kimaisha kuliko hii mingine.Wapo watu wanaodai kuwa huu ni utamaduni wa magharibi.Lakini baadhi ya wanaobeba midoli hii hasa ile ya watoto bandia wanapohojiwa hutoa sababu zifuatazo.

A. Huwasaidi kuwafariji wanapopoteza watoto wao wanaowapenda
B. Huwafariji hasa wanapokuwa hawakufanikiwa kupata watoto
C. Huwasaidia kupunguza hamu ya kuwa na mtoto

Naamini kila utakayemuuliza atakupa sababu yake na baadaye utagundua kuwa hakuna cha umagharibi wala cha umashariki ni swala la kujiendekeza na ubinafsi tu ndiyo unaotawala.

Midoli hii kwa wengine hasa wale wazoefu inawagharimu fedha nyingi kwa kuibadilisha badilisha ili kukata kiu yao. Mfano hii ni midoli inayouzwa kiasi ya pound 200.



Wengi wao hulazimika kununua toy carriers ambazo huuzwa kwenye supamarket mbalimbali dunia nzima.Hulazimika kuingia gharama yeyote ili mradi tu kiu yao ya kulea au kutunza mtoto huyo au mdoli huyo iishe.

Ninachotaka kusema ni kuwa, kwanza shwala hili linatokana na ubinafsi na kutojua thamani tuliyonayo binadamu.Na kama ni utamaduni wa kimagharibi basi unatokana na mazoea mabaya ambayo kizazi hadi kizazi kimerithishwa ambapo nalazimika kusema ni moja ya MILA POTOFU.

Binadamu anamajukumu makubwa sana na thamani yake ni kubwa sana wala hafanani kabisa na kubeba mdoli yaani toys.Mwenyezi mungu ameweka uwezo mkubwa sana ndani yetu na ametupa majukumu makubwa sana.Majukumu hayo ni pamoja na kuzaa,na kuhudumia viumbe hai vyote vilivyopo duniani.

Acha kutoa muda wako kuhudumia midoli na vitu visivyo na faida tuwaachie watoto ambao hawana majukumu yeyote wafanye kazi hiyo. Ebu ona huyu

http://www.mirror.co.uk/news/real-life-stories/the-fake-babies-craze-meet-the-women-786454

Kama unashida ya mtoto wako wengi ambao hawana mama na wanaweza kukuchangamsha wakiwa na full sensitivity.

Jumamosi, 5 Aprili 2014

VYUO MUHIMU VYA SERIKALI

                        KUTEMBELEA BOFYA TAASISI HUSIKA



Dar es Salaam Institute of Technology   Chuo cha teknologia

Uongozi Institute                                    Chuo cha uongozi

Institute of Adult Education-IAE            Taasisi ya elimu ya watu wazima

Institute Of Finance Management            Chuo cha usimamizi wa fedha

Ardhi Institute Morogoro - ARIMO       Chuo cha ardhi  Morogoro

Mineral Resource Institute - MRI          Chuo cha madini Dodoma  

Ardhi Institute Tabora - ARITA            Chuo cha Ardhi tabora

National Institute for Productivity           Chuo cha Taifa cha Uzalishaji

Water Development Management Institute - WDMI      Chuo cha Maendeleo na Usimamizi wa maji

Dar es Salaam Maritime Institute - DMI        Chuo cha ubaharia Dar es Salaam

National Institute of Transport - NIT           Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji

Tanzania Institute of Education - TIE           Taasisi ya  Elimu Tanzania

National College of Tourism - NCT             Chuo cha Utalii Cha Taifa

Bagamoyo Institute of Arts and Culture        Taasisi ya  Sanaa na Utamaduni Bagamoyo

Eastern Africa Statistical Training Centre - EASTC   Kituo cha mafunzo na Takwimu Afrika Mashariki

Tanzania Institute of Accountacy - TIA                     Chuo cha Uhasibu Tanzania

Tanzania Forest Research Institute - TAFORI           Chuo cha Utafiti misitu Tanzania

Tanzania Wildlife Research Institute - TAWIRI          Chuo cha Utafiti Wanyamapori Tanzania

Forest Training Institute - FTI                                   Chuo cha Mafunzo ya misitu 

Forest Industries Training Institute - FITI                  Chuo cha mafunzo ya uzalishaji wa bidhaa misitu    

Pasiansi Wildlife Training Institute - PWMTI             Chuo cha mafunzo ya wanyamapori

Beekeeping Training Institute - Tabora (BTI)             Chuo cha mafunzo ya utunzaji kumbukumbu

Community Based Conservation Training Center - CBCTC     Kituo cha mafunzo ya hifadhi za jamii  

National Instute for Medical Research - NIMR        Chuo cha Taifa cha Utafiti wa Tiba