Jumamosi, 25 Januari 2014

JINSI YA KUUFANYA MWANDIKO WAKO UVUTIE


Kuwa na mwandiko unaovutia ndiyo ndoto ya kila mtu anayeshughulika na uandishi wowote.Hata hivyo siamini kwamba kuna mtu ambaye hajawahi kukutana na swala linalohusu kuandika .Bila kujali kiwango chako cha elimu mada hii fupi inaweza kukuletea mabadiliko makubwa katika uandishi wako.

Mada hii nimeigawanya katika vipengele vinne :-

(i) Chagua mwandiko unaoutaka

(ii) Mbinu za kufanikisha mwandiko unaoutaka
(iii) Umuhimu wa kuwa na mwandiko mmoja
(iv) Ubadilishaji wa mwandiko na madhara yake

(i) CHAGUA MWANDIKO UNAOUTAKA


kabla ya kufikiri kuhusu kuboresha hati ya uandishi wako jambo la muhimu unalotakiwa kufanya ni kuelewa aina ya mwandiko unaoutaka. Kuna mwandiko unaotokana na maumbo tofauti ya herufi kama ifuatavyo:-

Herufi pana,herufi nyembamba au herufi za wastani (ukubwa wa wastani) ambapo ndani yake kuna

(a) Mwandiko wa Herufi ndefu, fupi au za wastani

(b) Mwandiko wa maneno ya kuunganisha ( mcharazo) au herufi za umbali
(c) Mwandiko wa sentensi za kugusa mstari chini au za kuning’inia (maneno yasiyogusa juu wala chini)  kwa wanaotumia kurasa zenye mistari.
kwa kuutazama muundo huo hapo juu unaweza kutengeneza aina tofauti tofauti za mwandiko, nyingi kwa kadiri upendanyo mojawapo ya hizo ni:-

         kundi la kwanza { mwandiko wa herufi ndefu.}


*  Mwandiko wa herufi pana ndefu za kuunganisha (mcharazo mpana) au kutounganisha

*  Mwandiko wa herufi nyembamba ndefu za kuunganisha au kutounganisha (mcharazo mwembamba)
*  Mwandiko wa herufi za ukubwa wastani ndefu za kuunganisha au kutounganisha (mcharazo urefu wastani)
Kundi la pili {mwandiko wa herufi fupi}
*  Mwandiko wa herufi pana fupi za kuunganisha (mcharazo)au kawaida
*   Mwandiko wa herufi nyembamba fupi za kuunganisha (mcharazo) au kutounganisha
*    Mwandiko wa herufi za ukubwa wastani fupi za kuunganisha au kutounganisha

         Kundi la tatu { mwandiko wa herufi za urefu wa wastani} huu unaweza kuwa,


*    Mwandiko wa herufi pana urefu wastani kuunganisha( mcharazo) ama kutounganisha

*     Mwandiko wa herufi nyembamba urefu wa wastani kuunganisha ama kutounganisha
*     Mwandiko wa herufi za ukubwa wastani urefu wastani za kuunganisha ama kutounganisha

Hapa unaweza kupata aina nyingi zaidi ya hizo kulingana na utakavyoamua ila nitoe pendekezo.utafiti wangu umeonyesha kuwa:-


*    Mwandiko mpana unapendeza ukiwa mfupi na usiounganishwa sana maneno yake.

*     Mwandiko mwembamba unapendeza ukiwa mrefu ukiunganishwa maneno yake.
*    Mwandiko wa upana wa wastani unapendeza ukirefushwa na hata bila kurefushwa {kimo}

(ii)            MBINU ZA KUFANIKISHA MWANDIKO UNAOUTAKA


Hapa inabidi turudi nyuma kwenye zama za utoto bila kujali elimu yako wala umri hatua kwa hatua


(a)     USHIKAJI WA KALAMU (ushikaji wa kalamu unaweza kuathili mwandiko wako moja kwa moja bila kujali uzoefu)


* Wanaopendelea mwandiko wa herufi ndefu , wengi wao hushika kalamu juu kidogo kiasi cha sm 1 kutoka chini ya kalamu na zaidi

*    Wanaopendelea mwandiko wa herufi ndefu wastani, wengi wao hushika kalamu kwenye wastani wa sm 1 kutoka chini ya kalamu.
*    Wanaopendelea mwandiko wa herufi fupi hasa pana, wengi wao hushika chini zaidi au sm 1 kutoka chini ya kalamu.
Hapo sio tageti ya somo letu bali naomba uwe makini katika hatua inayofuata.

(b)FANYA ZOEZI LA MAUMBO YA HERUFI


Kumbuka kabla hujaanza zoezi chagua unataka mwandiko wa aina gani,kosa kubwa tunalofanya huwa tunaanza kuandika bila kuwa na uchaguzi wa mwandiko gani tuukao .kwa wale wa Kiswahili na kiingereza ni herufi A to Z. Panga herufi zako kwenye karatasi yenye mistari kama sio daftari.hakikisha unaanza na herufi ya kwanza unaiandika kwa ustadi unaouweza ukiazia mwanzo wa mstari mpaka mwisho ukifuatia na herufi inayofuata kwenye mstari unaofuata kama unavyoona katika mfano huu,


a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a 

b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b 
c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c
d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d

baada ya zoezi hilo utagundua kuna herufi kwako zina ugumu wa kuziunda zifanyie kazi kwa mfano huohuo mpaka zitokee unavyopenda bila kusahau aina ya mwandiko uliochagua na kama mmoja unakuwa mgumu badilisha aina ya mwandiko.Hatua hii ni ya taratibu na usiunganishe herufi zako.

Baada ya kumaliza hatua hii njoo hapa chini,

(b)FANYA ZOEZI LA MAUMBO YA MANENO


Ukianzia na zile herufi zilizokuwa kwako ngumu kwenye hatua ya kwanza, mfano kama kwako k,h,g,z na r ndo zilikua ngumu, unda maneno yanayoyumia herufi hizo na kufanyia mazoezi hata kama hazileti maana .Kumbuka kama kutakuwa na herufi zisizopendeza katika maandishi yako zinaweza kuharibu mwonekano wa mwandiko wako wote na ukaonekana hujui kuandika au una hati chafu.kwa kufuata mfano huu unaweza kuona cha kufanya.


kihagazira kihagazira kihagazira kihagazira kihagazira kihagazira


Fanya zoezi hilo mpaka uone umefaulu zile herufi zote zinazosumbua.


(C)FANYA ZOEZI LA UANDISHI WA SENTENSI


*  Ikiwa sasa umeshafuzu kwa mazoezi yaliyotangulia malizia na uundaji wa sentensi kwa kuamua sasa kufuata mtindo wa kuning’iniza maandishi au kugusisha kwenye mstari kwa chini kama utakavyopenda.

*   hakikisha unafuata taratibu zote za mwanzo kama ulivyoanza katika herufi hadi maneno huku ukigeuza maneno hayo kuwa sentensi.
*  Endesha zoezi taratibu ukipanga unachotaka kitokee na ukidhibiti mwandiko usibadilike yaani herufi moja kwa kurasa nzima .hapa ninamaana herufi hupendeza sana kama itakapoandikwa ikafanana na zilizotangulia.na huo ndo uzuri wa mwandiko wenyewe yaan herufi( A) niliyoiona mwanzo wa ukurasa inafanana na ile iliyopo mwishoni mwa kurasa.
* Kumbuka kama utaamua kugusisha mstari basi ni maandishi yote, na kama yataning’inia basi ni yote tena zingatia nafasi unayoiacha kutoka kwenye mstari mpaka maandishi iwe ni moja ili kuleta mvuto wa maandishi yako.
*  Jambo la mwisho la kuzingatia kumbuka kuacha nafasi inayo fanana kati ya neno na neno maana hapo ndipo panapo leta ustadi wa uandishi wako pole maneno yako yatakapo kuwa yanaonekana yameachana kwa nafasi inayofanana na herufi zake zikifanana.

(d)UANDISHI WA KWENYE KARATASI ISIYO NA MISTARI


Hapa ndipo penye changamoto kwa walio wengi, lakini zoezi ni rahisi sana.

*Chukua karatasi isiyokuwa na maandishi ukiwa na kalamu yako mkononi.

*Laza karatasi yako mezani kisha chukua kalamu yako na uisogeze kwa juu kabisa upande wa kushoto na uilaze huku kile kichwa cha kuandikia kikiwa kinakutazama wewe.


*Isogeze kalamu yako nyuma yaani kama mtu anaeiondoa kwa kuiburuta mpaka kile kichwa cha kalamu tu au pale kalamu inapoanzia kupungua ukubwa au kubonyea ndiyo pabakie ndani ya karatasi.kwamaana nyingine kalamu yako itakuwa ndani ya karatasi yako kwa wastani wa sm1 tu au pungufu.


*palepale ilipo kalamu yako bila kuhamisha isimamishe kisha weka alama ya wino utakayoiona wewe tu, kisha kwa kipimo kilekile au usawa uleule uliopo sogeza kalamu upande wa kulia mpaka usawa wa kati weka alama nyingine, vivyohivyo na upande wa kulia. Hivyo kama utaamua kupiga mstari kutoka alama ya upande wa kushoto kwenda alama ya kulia utapata eneo la juu ya karatasi yako kiasi cha sm1 likiwa limetengwa .sasa usipige huo mstari ila fanya hivi,


*  kwa kufuata alama ulizoziweka ambazo unaziona wewe tu ,zifanye kuwa ndo dira yako ya mstari wako wa kwanza wa uandishi wako,nina maana hiyo ndo itakuwa point yako ya juu ya maandishi yako ya mstari wako wakwanza.kwa maana nyingine kimo cha maandishi yako kitaishia kwenye alama hizo.


*  Nyoosha mstari wako wa maandishi wa kwanza kwa kutumia usaidizi huo wa alama hizo kwa ustadi mkubwa.


*   Mistari inayofuata utahakikisha kile kiasi cha nafasi kati ya maandishi ya juu na chini unachoacha kwenye herufi yako ya kwanza, ndo utakachoacha hata kwenye herufi zako zinazofuata,hivyo itafanya hata mstari unaofuata unyooke.Utaendelea na zoezi hilo mpaka mwisho na utajikuta unanyoosha maandishi hata bila alama yeyote.


(III))UMUHIMU WA KUWA NA MWANDIKO WA AINA MOJA ,(HII ITAKUSAIDIA KATIKA YAFUATAYO)


(a)  itakuwa ndo nembo yako kwa upande wa maandishi

(b)  Itakusaidia kuuboresha mwandiko wako baada ya kuuzoea
(c)  Itakuwa rahisi watu kutambua na kuheshimu kisomo chako kupitia mwandiko wako
(d)  Itakusaidia katika usahihishaji wa mitihani yako kuwa na hati inayosomeka pasi na shaka
(e)  Itakupatia kipaumbele katika uombaji wa kazi kwasababu wengi watahitaji kuona uandishi wako wa mkono(barua nyingi za kazi huandikwa kwa mkono)
(f)  Unachokiandika kinaweza kusomwa na mtu yeyote bila usaidizi wako nk

(iv)  Ubadilishaji wa mwandiko na madhara yake


(a)   Huwezi kuuboresha kwasababu hutouzoea

(b)  kuwatia watu mashaka juu ya kisomo chako
(c)  Faida zote zilizotajwa hapo juu utazikosa
Kazi kwako mwenzangu kuendelea kubaki na hati yako ya mashaka au kutumia mbinu mbadala kama zilivyoelezwa hapo juu kujinasua, nakutakia siku njema na karibu tena.







Maoni 4 :

  1. ahsante saa kionogozi nimejifunza kitu hapaa, Ubarikie sana kwa somo nzuri,..

    JibuFuta
  2. Ahsante kwa kazi nzuri mnayoifanya mbarikiwe sana!

    JibuFuta
  3. Nataka kubali mwandiko katik
    kuchati

    JibuFuta