Jumapili, 9 Februari 2014

MBINU NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI PART TWO

Kumbuka kuwa katika awamu iliyopita nilizungumzia zaidi kuhusu hofu , matokeo yake na jinsi ya kupambana nayo ndani ya chumba cha mtihani.Vilevile niligusia kuhusu kuchanganyikiwa lakini sikuzungumzia ni kwa namna gani kuchanganyikiwa kunavyoweza kukuathili ndani ya chumba cha mtihani. Nitagusia kuchanganyikiwa huko kabla ya kuanza kuuchambua mtihani wenyewe.

KUPAMBANA NA KUCHANGANYIKIWA KWA MUDA NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI .


Hii ni hali inayotokana na hofu.Huwatokea walio wengi hasa wanapopatwa na mshtuko wa hofu mara tu wanapoingia ndani ya chumba cha mtihani .Matokeo yake huwa kama ifuatavyo:-


      *Kutojua nini cha kufanya baadaya mtihani kuanza,hii ina jumuisha kupoteza uwezo wa kuelewa hata melekezo madogo tu ya mtihani.


     *Hupelekea kupoteza kumbukumbu kwa kiwango kikubwa na kutoelewa hata swali la kawaida.Hii hujumuisha pamoja na kutokumbuka hata kuandika namba ya mtihani au jina katika karatasi za mtihani.wengine huwapelekea kushindwa hata kuandika majibu katika vyuma vya kuandika majibu.


    *Papara .hii hupelekea wengine kugeuza mambo kuwa kichwa chini miguu juu ,sehemu ya kuandika jina la mtihani akaandika namba ya mtihani na sehemu ya namba kinyume chake.Vivyohivyo hata sehemu ya majibu kutofuata mtiririko sahii na matokeo yake majibu kuandikwa mahala ambapo si pake,jibu na.2 kuandikwa sehemu ya jibu na. 3 nk

.
    *Kutumia muda mrefu kuelewa swali na hivyo kupoteza muda hata kwenye swali rahisi au kutomaliza kujibu maswali swala ambalo limekuwa likiwakwamisha wengi katika mtihani.

SULUHISHO


Kabla ya kuanza mtihani pata dakika za kuzoea mazingira kwa kujiweka huru kwa kujinyoosha ,kutazama wenzako unaofanya nao mtihani ikiwezekana mpe ishara mwenzako kwamba hauko sawa chochote atakachojibu kitakusaidia. Endapo atakuonyesha ishara ya kwamba usihofu itakupa moyo endapo atakuonyesha ishara ya kifo bado itakuimarisha kwasababu hutakubali kufa kitoto.

      Hali hiyo hutokana na hofu na hofu yenyewe ni kwasababu hujui katika mtihani umeulizwa nini.Ukisha pata mtihani wako utaupitia haraka kama nilivyokwisha eleza hapo chini. ukimaliza utakuwa umejua ukweli wa yale yaliyokuwa yakikutishia na hapo hofu kwa sehemu kubwa itakuwa imeondoka.
      Usianze kufanya mtihani mpaka utakapoona uko sawasawa kwa kuwa hali hii kama utafanikiwa kuupitia mtihani wote huwa haidumu .Na kwa kufuata hatua nilizozifafanua hapo chini hutakuwa na hofu tena na hivyo kuwa mbali na kuchanganyikiwa huku kwa muda.
      Kumbuka kuwa lengo la kukupa mikakati hii sio kukufanya ubaki na mbinu za kujibu mtihani tuu la hasha ,bali ni katika kukusaidia uweze kujibu sawasawa na ulivyoelewa bila kuingiliwa na vitu vitakavyo zuia kuonyesha uwezo wako na kukunyima fursa iliyoko mbele yako.

SIFA ZA MTIHANI NA MBINU ZA KUUKABILI.


Naomba nikugawie siri kidogo, mtihani wowote huwa na sifa zifuatazo :-

1.Maelekezo ya mtihani
2.Maswali ya ufahamu (Yakiufahamu)
3.Maswali ya saikolojia( Yakisaikolojia)
4. Maswali ya kumbukumbu (Yakikumbukumbu)

MAELEKEZO YA MTIHANI


Hapa panajumuisha maelekezo yaliyoandikwa katika utangulizi wa mtihani kama nitakavyofafanua hapo mbele


MASWALI YA UFAHAMU.


haya ni maswali yanayompa mtahiniwa uhuru wa kujieleza kwa kutumia ufahamu wake.hapa mtahiniwa atapewa miongozo kadhaa ya kuelezea mada Fulani kwa kutumia maneno yake na kwa jinsi anavyoweza.Na mara nyingi hapa ndo huwa na marks nyingi.Sehemu hii mara nyingi huanza.Itumie vizuri sehemu hii


MASWALI YA KISAIKOLOJIA


Haya ndiyo maswali yanayoweza kupima uwezo wako wa kisikolojia namna gani unauwezo wa kutofautisha jambo moja na jingine au kutofautisha mambo yanayoonekana kufanana sana.

       wakati mwingine huambatana na mitego midogo itakayopima msimamo wako katika jambo ulilolielewa sawasawa.
Hapa unaweza kupewa vitu vilivyofafanuliwa na kuambiwa uvipange katika makundi,au uvioanishe kwa kutumia alama flani au kupewa maswali rahisi yenye majibu yanayoshabihiana sana .au kupewa majibu yanayoshabihiana na kuambiwa uchague moja.Weka utulivu katika sehemu hii na kufanya unachoamini kuwa ni sawa.Sehemu hii mara nyingi huja baada ya maswali ya ufahamu.

MASWALI YA KUMBUKUMBU


Haya ni maswali ambayo yanapima uwezo wako wa kukumbuka na huwa hayafanani kwa vyovyote na aina ya maswali yaliyo tangulia.Kwa wastani hii ndiyo sehemu iliyo ngumu kwa watu karibu wote isipokuwa kwa wale wanaofahamika kama watu wenye kipaji cha kumbukumbu .

        Maswali ya namna hii mara chache sana huwa yanatoa mwongozo wa jibu, zaidi zaidi huwa yanataka jibu la moja kwa moja na si jibu la maelezo yanayotokana na ufahamu wako.Sehemu hii mara nyingi huwa mwisho.

MBINU ZA KUUKABILI MTIHANI


Mbinu za kuuukabili mtihani ni rahisi sana hasa unapofika hatua hii.Na inakuwa rahisi zaidi endapo utakuwa umekwisha maliza hatua ya kwanza ya kuishinda hofu.

         Kutokana na umuhimu wa mada yenyewe nitaomba hapa twende hatua kwa hatua.

1.soma kwa umakini maelekezo ya mtihani

Itakusaidia kujua sura ya mtihani na kuanza kuuzoea kwa kujua unavipengele vingapi,na meelekezo mengine muhimu ya nini cha kujibu na nini si cha kujibu.
     Epuka kuanza kufanya mtihani bila kusoma maelekezo na epuka kutegemea maelekezo ya msimsmizi wa mtihani.kumbuka kuwa msimamizi anaweza kughafilika kutokana na ujuzi mdogo alionao katika maswala ya kufafanua mambo, au kutojali kwasababu hatowajibika kwa lolote endapo utafanya makosa yeyote yatakayokinzana na maelekezo ya mtihani.
      Kwa kuwa mtihani unakuhusu wewe na msahihishaji anategemea sana jinsi ulivyoyatumia maelekezo katika kujibu mtihani ili atoe marks, hivyo hatojali maana nyingine yeyote kinyume na maelekezo katika usahihishaji wa mtihani wako.Kwasababu hiyo usikubali kupoteza marks kwasababu ya kutofuata maelekezo.
     Fuata maelekezo yote hata kama ni kuandika jina na namba yako ya mtihani katika kila ukurasa kwasababu huwezi jua kama kurasa yako moja itajumuishwa na ya mtu mwingine wakati wa shughuli za usahihisha.

*CHUNGUZA MTIHANI

Utambue kuwa mtihani sio taarifa ya habari kusema lazima uanzie mwanzo hata kama utaratibu huo hauna maslahi kwako.
Hapa unachofanya ni kutulia na bila papara unaupitia mtihani wote kwa haraka kwa lengo la kuuchunguza mtihani .katika kuuchunguza mtihani utakua ukiangalia vitu vitatu

1.maswali ambayo unauwezo wa kuyajibu haraka bila kutumia muda, yaani unayafahamu na majibu yake haya hitaji muda mwingi kuyajibu.

Mara nyingi kwa sababu za usalama wa mitihani hasa ya kitaifa huwa inazuiliwa kuandika chochote katika karatasi ya maswali .
       utakachokuwa unakifanya kwa kutumia nyuma ya karatasi yako ya majibu utakuwa ukinoti maswali ya namna hii yaani yale mepesi sana kwa kuandika namba yake.Kitu utakachokuwa unakifanya hapa utakuwa katika kila namba ya haya mswali utakayokuwa umenoti utakuwa ukiandika neno (one) andika neno hilo mbele ya hizo namba za maswali yako yote uliyoyachagua kuonyesha kuwa ndo utakayoanza kuyajibu.

2 maswali mepesi ila yanahitaji muda kuyajibu hii ni pamoja na maswali yanayohitaji maelezo marefu.

Haya katika mtiririko wako utakuwa ukiyawekea alama ya (two) mbele ya kila swali utakalolichagua kama ulivyofanya katika maswali ya kundi la kwanza.Kufanya hivyo kutakusaidia kuyatambua kwa haraka wakati wa kuyajibu.

3.maswali ambayo huwezi kujibu kabisa

Haya utayawekea alama ya (three) mbele ya kila namba utakayoiandika au unaweza usiyawekee alama yoyote kama utakuwa na uhakila kuwa umejumuisha maswali yote muhimu katika aina ya (one) na(two) .
     usijali kuwa labda kufanya hivyo ni kujivunya moyo la hasha ,kwani hii itakusaidia kuyapata kwanza yale yote utakayoweza kuyajibu kwa uhakika ukianzia na yale yanayohitaji muda mchache na baadaye yenye kuhitaji muda na mwisho utakuja kuyaangalia haya usiyoyaelewa.

*kwa kutumia mwongozo uliouandaa wewe mwenywe anza kujibu maswali ukianzia na kundi la (one) hadi (three).kwa kufanya hivyo kutakupa kujiamini zaidi na kuutawala mtihani, maana utakuwa tayari unamtaji mkononi wa maswali ambayo utakuwa na hakika ya kuyajibu kwa usahihi.


*zingatia muda .katika vitu vinawaangusha watu wengi ni kuhusu muda katika chumba cha mtihani.Ukijua kuwa katika mtihani kunamaswali kadhaa unaweza ukakosa kwa kutokuyajua au kushindwa kuyakumbuka hivyo usiongeze kukosa marks nyingine zitakazo tokana na kutomaliza kazi kwa uzembe wa kutokutunza muda.

     Vitu vya kuepuka ni ,
kufikiri muda mrefu kwenye maswali ya kujieleza,
kurudia rudia kwa swali ambalo hulikumbuki, 
Swali ambalo kanuni yake umeisahau. 

*katika maswali yanayohitaji ufahamu wako wa kujieleza tumia fursa hiyo kwa uhakika kwa sababu hakuna mahala ambapo huwa pana nafasi ya kuchukua marks za bure kama mtu anapoambiwa ajieleze.hakikisha kwamba hufanyi makosa ya kiuandishi au yanayofanan na hayo ili kujihakikishia marks za bure.


*epuka kukata majibu uliyokwisha andika bila kuwa na hakika.Kila jibu utakalokuwa ukiliondoa kwa maana ya kubadilisha hakikisha unauhakika nalo kwa sababu uzoefu umeonyesha kuwa mara nyingi katika yale maswali ya hamsini kwa hamsini yaani nusu unakubali na nusu unakataa, jibu la kwanza huwa ni sahii ila hofu ya kutojiamini hufanya wengi kubadili.

     Hii hujitokeza zaidi katika maswli ya kisaikolojia, kwa sababu mtindo wa maswali hayo ni kukufanya usijiamini katika majibu yako.Mtunga swali hutengeneza swali litakalokuwa na ushawishi mkubwa kukufanya uandike jibu ambalo si la kweli hata kama jibu litakuwa liko wazi.
       Hatua hii ni ya muhimu sana katika mtihani kwasababu huwa na maswali rahisi lakini yanaushawishi mkubwa wa kukufanya uandike jibu ambalo si sahii au uchague jibu la uongo.

*tumia mtihani kupata majibu ya maswali magumu

Baada ya kujirdhisha kuwa umemaliza maswali yote yenye uwezekano wa kujibika anza kuupitia mtihani kwa kupata majibu au mwangaza wa maswali magumu.
        Fananisha swali lako na maswali yaliyopita na ujiridhishe kuwa unachotakiwa kukijibu hakijatajwa kabisa katika mtihani ,ua hakuna maelezo yeyote yanayoweza kutoa mwongozo wa jibu ninalolitaka.

*Usiache swali ambalo halijajibiwa hasa kwa yale maswali ambayo yatakuwa ni magumu kwako mwanzoni.Jibu kila swali hata kama utakuwa huna uhakika kama umejibu sahihi maana kufanya hivyo ni bora kuliko kuacha bila kujibu chochote.


*bakisha muda wa kuupitia mtihani wako kwa majumuisho

Binadamu yeyote anaweza kufanya makosa hata katika mambo ya muhimu kiasi gani, hivyo ni muhimu kupata muda wa kupitia ulichojibu mstari kwa mstari, jibu kwa jibu ili kujihakikishia kuwa hakuna swali lililojibiwa halafu likawa na makosa ya kiuandishi ama vinginevyo.
    Kwa kutumia mwongozo huu ninaimani kuwa sasa utaingia katika chumba cha mtihani ukiwa kifua mbele ukiwa na uhakika wa kufanya vizuri.
Usiache kutembelea blog yako uipendayo kwa mada zenye kuimarisha fikra zako.

Maoni 1 :

  1. Nashkuru kwa maelekezo nitajitatahidi kuyafanyia kazi

    JibuFuta