Jumamosi, 25 Januari 2014

NIFANYE NINI KABLA YA KUJIENDELEZA KIELIMU?

Japo tunafahamu kwamba elimu ndiyo ufunguo wa maisha lakini swala la kujielimisha sio swala la kukurupuka kama ilivyo kwa wengi na matokeo yake huambulia majuto baada ya kupata mrejesho wasio utarajia.Mtu anaweza kujiendeleza kielimu kwa lengo la kupata cheti ,kuiga, kuvutiwa na ajira njenje,kutaka kuwa msomi,ndugu zake wote wamesoma ,wazazi wameamua,bwana au mke kashauri nk.Hizi zote sio sababu sahii za kujiendeleza kielimu na inatokana na kutofahamu nini cha kufanya kabla ya kujiendeleza kielimu.

Kupitia mada hii fupi utaweza kuondoka na kitu muhimu kabisa kitakacho kusaidia katika maamuzi yako ya kujiendeleza

(1).LENGO LA KUJIENDELEZA KIELIMU
Kabla ya kujua nini cha kufanya kitu muhimu unachotakiwa kufanya ni kutambua lengo la kujielimisha .

 A.kupunguza ujinga
Nimetumia neno kupunguza ujinga kimakusudi hata kama nitatofautiana na watu wengi. Hapa ninamaana  kuwa ujinga hautaisha kwa  mwanadamu  hata kama atapewa  miaka elfu ya kuishi duniani, bado atahitaji kujifunza.kwasababu ujinga maana yake ni hali ya kutojielewa au kutojitambua au kupungukiwa na ujuzi flani ambao hata kwa miaka mingapi huwezi kujua kilakitu.




 Kwa maana hiyo ni lazima kujielimisha kwanza ili kupunguza ujinga wa kutojitambua.

kupitia kujielimisha ndoyo unaweza kutambua thamani yako ,mapungufu yako ,mazingira yako,kipaji chako,na mengineyo japo kwa uchache.

B.kuimarisha kipaji na ndoto.
Kila mtu anakipaji na ana ndoto bila kujali ameelimika au hajaelimika .Elimu ndiyo inayoweza kuimarisha hizi ndoto na vipaji, kwasababu kipaji bila elimu hakitafanyakazi  na ndoto bila elimu itapoteza mwelekeo.pia naomba utambue kuwa kunatofauti kubwa sana kati ya kipaji na ndoto ambapo inanibidi nifafanue kidogo ili kipengele hiki cha kuimalisha kipaji na ndoto kieleweke sawsawa.




(i).kipaji        
Ni ule uwezo wa asili tunaozaliwa nao wa kufanya jambo flani kipekee kabisa bila kufanana na mtu na huwa hakibadiliki kutokana na mazingira au wakati.


Kipaji kinaweza kutambulika ,kuendelezwa au kuimarishwa kupitia elimu.nimewahi kufanya utafiti kwa kuwahoji wanafunzi wengi wa sekondari waniambie wanakipaji gani,wote waliishia kuniambia wanakipaji cha fashon show,kudansi,kuimba,kucheza mpira na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Nilichogundua ni kwamba wamekosa elimu ya kujitambua na kutoelimishwa kuwa hata hesabu,biology,chemistry,geograph,lugha,computer, uandishi navyo ni vipaji kama vingine,kwasababu walioandika tunayojifunza na yanayokuja ni matokeo ya vipaji vilivyotangulia.Sio lengo langu kufundisha kuhusu vipaji ila inahusiana na mada yetu.


(ii).ndoto au maono
Hii ni shauku, hamu  kiu au muono wa mbele  wa kupata au kuifikia hali flani ambayo huwa inabadilika badilika kutokana na mazingira.KWA KIFUPI INAITWA PICHA YA AKILINI.


Wakati flani mtu huwa na ndoto kutokana na mazingira aliyonayo.  Wakati mwingine wote tunaweza kuwa na ndoto ya aina moja mfano kuongoza  NGO ,SHULE ,SOCIAL NETWORK,AU KUWA NA NYUMBA NZURI GARI ZURI au pengine KUWA MTU FULANI nk.tofauti na kipaji kila kimoja kitajitokeza kwa namna ya upekee sana.


Vile vile ndoto huweza kubadilika kwa kuathiliwa na  mazingira,elimu,kipato,makundi nk.leo mtu anaweza kutamani kuwa daktari kwasababu hana elimu na hajui udaktari ni nini  unapatikanaje na kwa sifa zipi.


Vivyohivyo mtu anaweza kuwa na ndoto ya kuwa rubani ,kuwa mchezaji maarufu,muimbaji maarufu nk.mtu huyu baadaye akielimika anaweza kubadilisha ndoto yake na kwenda mbali zaidi au kufahamu hatua za kuchukua kuifikia.

 (2). MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YA KUJIELIMISHA

 A.Tambua kipaji chako kwanza  na sio ndoto




Nimeshaeleza kwa kirefu kuhusu ndoto na kipaji hivyo unapaswa kutambua kipaji chako.Makosa makubwa tunayoyafanya ni kukimbilia kutambua ndoto kabla ya kipaji.

Utatambuaje kipaji chako?

Ni rahisi sana .piga picha maisha yako yaliyopita na kuona mambo machache katika haya

(i)  Ni jambo gani kati ya mambo yote kwako ulikuwa unalimdu kirahisi kuliko yote

(ii) Jambo ambalo wazazi waalimu na watu au marafiki zako wanakubali kwamba unaliweza sana

(iii) Jambo ambalo ukishindanishwa na watu wengine wewe unakuwa wa kwanza au nafasi za juu


(iv)  Jambo ambalo wazo au idea yake inakuja bila kutumia nguvu wala mafunzo mengi


(v)   Jambo ambalo hata ukijitahidi kulikwepa na kufanya mengine bado unalifanya vizuri   kuliko hilo jipya unalolifanya.


(vii) Jambo unalolifanya kwa usahihi mkubwa bila kutumia jitihada nyingi kama wengine


(vii) Jambo ambalo akili na mwili wako vinakubaliana nalo kirahisi kulifanya hata kama wengine wanaliogopa.

Nafikiri maelezo hayo hayahitaji elimu ya kifilosofia au saikologia kuyaelewa,unaweza ukaanzia hapo katika kuchagua ujielimishe katika lipi na si kuingia kila jambo na baadaye kujuta Ukipoteza wakati.Jiulize kuwa kama Christiano Lonaldo angefuata upatikanaji wa ajira na kuamua kosomea ualimu leo angekuwaje?.


B.     Tambua kuwa wewe ndiye mwenye jukumu la kwanza katka kujielimisha
Kumbuka ,mwalimu ,mlezi  au chuo vinachukua nafasi ya pili katika kukuendeleza kielimu.Ikitokea chuo au shule  imesitisha masomo au kufungwa  au mwalimu kutokuwepo  au mzazi kutokuwepo au kufariki au kwa namna yeyote ile mtu anayeshughulika na kusaidia upatikanaji wa elimu yako kutokuwepo, jukumu litabaki kwako kwa asilimia mia.


Ili kipaji chako kiweze kuchanua ni lazima upate elimu inayohusiana na unachotaka kukitumikia ,kwasababu hiyo utakuwa na jukumu la kuhakikisha unajielimisha kwa namna yoyote ili kupunguza ujinga hasa kwa kile unachotaka kukitumikia.


Zipo njia nyingi sana za kujielimisha binafsi  hii ni pamoja na vitabu,semina,majarida ,magazeti,mitandao,tafiti nk.


C. Tambua Bidii ni kusoma na sio mahudhurio
utakuwa ni upotezaji wa muda kama hutajua jukumu lako la msingi katika kujiendeleza ukazingatia mahudhurio na si masomo .Unachotakiwa kufahamu kuwa tuhudhurie darasa au tusihudhurie kujielimisha ni lazima.kwa hiyo kujielimisha ndiyo liwe jukumu lako la msingi.





D. Uchaguzi wa shule au chuo ni muhimu
Unachopaswa kuzingatia katika uchaguzi wa shule au chuo ni ,uwezo wako wa kukabiliana na gharama,mazingira( hapa ni pamoja na teknologia inayotumiwa na shule au chuo, jiografia,umbali,hali ya kimjini au akijijini,nk.)  unapaswa kufahamu hayo yote ili yasije kukupotezea muda wa kujifunza mazingira kwa wakati huohuo ukijifunza ulichokiendea.kitu kingine cha muhimu ni kuangalia uhalali wa chuo au shule pamoja na uwezo wa kukupatia elimu unayoitaka.


E.     Tambua vikwazo vya upatikanaji wa elimu yako
(i) kwa mfanyakazi. Ratiba yako kama itakuwa endelevu, kama sivyo weka mkakati ikiwezekana  badilisha kazi


(ii) kijana wa nyumbani. Jiulize kama una mtu wa kugharamia masomo yako. kama utasoma nyumbani notes utapata wapi?, practicals  utaziendesha vipi?.


(iii) masomo online. Unavifaa vya kutosha kupokelea masomo mtandaoni?,unauelewa wowote kuhusu mtandao?.Umechukua tahadhari yoyote kuhusu uharamia wa mtandao?


(iv) masomo ni mbali.Jiulize kama utamudu usafiri pamoja na gharama za maisha?,kama la,basi bora usome karibu

(iv) UMRI.Tambua umri wako kama unaweza kukuathili katika masomo yako.Tambua pia taratibu za shule na chuo kama zinaweza kukuathili kutokana na umri wako.


Hakikisha umetambua vikwazo vyote na kuvitafutia ufumbuzi mapema.


F. Tambua fursa za kipaji chako




Ni muhimu kabla ya kuamua kujielimisha tambua kwanza fulsa za kipaji chako.kama unafikiri wewe ni-


(i)  Mzuri kwenye hesabu.Unaweza kufanya kazi gani? labda baadaye kuwa space man (astronaut)->” hawa ni wataalamu wanaofanya majaribio ya kisayansi angani”,mwanamahesabu,engineer  wa -> sayansi ,majengo,ndege,meli,mashine, nk.


(ii)  Mzuri kwenye jiografia.Unaweza kuwa mtafiti wa wanyama pori,au wa anga au wa hali ya hewa,madini,viumbe bahari, nk


(iii)   Mzuri kwenye kilimo.Unaweza kuwa mtafiti wa kilimo,afisa kilimo,mkulima,mtaalamu wa mifugo,mfugaji wa kisasa wa samaki nk.

(iv)  Mzuri wa sanaa .Unaweza kuwa mtaalamu wa lugha ukitumika kutengeneza programu mbalimbali za computer zinazohusiana na lugha kama speech synthesis,mashine translation,speech recognition,kutengeneza kamusi,kufundisha lugha,kuimba ,kucheza ,kutengeneza filamu ,mwanafalsafa,mwanasaikologia ,mwandishi wa vitabu nk.

(v) Mzuri wa biashara.Unaweza kuwa mfanya biashara au kufanya kazi katika mabenki,makampuni ya kibiashara,kazi za kiuhasibu nk.

(vii)Mzuri kwenye sayansi. Unaweza kuwa daktari,Muuguzi,mfanyakazi wa maabara,mkemia,nk

Hii ni mifano tu ya fulsa unazoweza kuzitazama ambapo wewe utatazama katika kipaji chako kabla ya kuamua kijiendeleza kielimu.

G.     Anza masomo kabla ya kuandikishwa shule
Kosa kubwa ambalo watu wengi hufanya katika kujielimisha ni kuendelea kusubiri na kusubiri mpaka aingie darasani ndipo aanze masomo.

*Jukumu la kusoma ni la kwako  hivyo kama unania ya dhati ya kujiendeleza basi anza sasa kusoma .wakati mwingine unaweza usinielewe, ninaposema anza sasa kusoma nina maana kile unachoweza kukisoma sasa anza kulisoma.


*Mfano kama wewe unataka kujiendeleza na masomo ya secondary na unafahamu kuwa lugha itakusumbua basi anza kujifundisha lugha kwa kujua misamiati ya maneno usiyoyafahamu.kama hilo haliwezekani basi anza kusoma Kiswahili kwa kutumia kitabu utakachokinunua kwenye maduka maalumu ya vitabu vya kiada.

*unataka kusoma kozi flani katika chuo, anza kuchukua elimu ya ujumla kutoka kwenye notes za waliotangulia kusoma kozi unayokusudia kuisoma na kama unaweza kupata kozi nzima, soma yote .Usifikiri kuhusu kujiandikisha shule kwanza, kitu cha muhimu kwako kwanza ni elimu.

 Hii inamaana gani?,
Kuelimika ndiko kunakotoa  mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo  na sio vyeti. Sikatazi kutafuta cheti, bali elimika kwanza.watu wengi  hawajajikita kwenye dhana ya kuelimika ili walete mabadiliko na badala yake husubiri  vyuoni kwa muda mrefu  ili wapate vyeti na kuja kujifunza upya kitu kilekile walichokisoma.


Wakati mwingine hujifunza kupitia hata kwa watu wasiopitia darasani.Ikatae hali hii itakayo punguza kasi ya kukitumikia kipaji chako na kuchelewesha ndoto zako.


Nakushukuru kwa muda wako ulio utoa kupitia mada hii fupi inayohusu nifanye nini kabla ya kuamua kujiendeleza kielimu?   Naamini umenufaika na mengi karibu kwa mada nyingine.

Maoni 1 :