Ijumaa, 31 Januari 2014

MBINU NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI

Ndani ya chumba cha mtihani kuna changamoto nyingi sana tofautitofauti ambazo bila kuzifahamu unaweza kujikuta ukipoteza mtihani wako na kuambulia ziro usiyoitarajia.kwa kufuata maelekezo haya ya mbinu ndani ya chumba cha mtihani utaweza kutoka na matokeo unayoyatarajia.
Zingatia kuwa mara tu uingiapo ndani ya chumba cha mtihani kabla hujauona huo mtihani,kuna matatizo kadhaa ambayo imekuwa kama ni desturi kukutokea.
                (1)    Hofu
Huyu ndiye muuaji mwenyewe anayeweza kukumaliza na kukufanya utoke katika chumba cha mtihani ukiwa hujielewi nini umefanya. Hapa imenichukua muda kufanya utafiti na kutazama wataalamu wa maswala ya hofu wanasemaje, maana hata mimi nimejaribu kufanya kila liwezekanalo kutokuogopa mtihani lakini nikiingia tu, kwenye chumba cha mtihani mambo yako palepale sijui kwako mwenzangu.Ila leo umepata suluhisho la tatizo hili la awali ambalo ndo muuaji na.1 wa jitihada zetu za kielimu.

(A)   UCHAMBUZI WA SHWALA LA HOFU
      (i)                 Hofu ni nini?
      (ii)               Sababu za hofu
      (iii)             Matokeo yanayoletwa na hofu
      (iv)              Jinsi hofu inavyoweza kukumaliza ndani ya chumba cha mtihan
      
       (i)           Hofu ni nini?
         Kwa mujibu wa utafiti wa sayansi ya tiba ya mfumo taarifa wa mwili (link.neurobiology of fear) uliofanyika mpaka sasa naweza kusema,
Ni kitendo cha kuogopa  kinachotokea katika fikra za binadamu au mnyama ambacho hupelekea kujenga hali ya kujihami dhidi ya hatari inayotaka kujitokeza.Hii inaukweli mkubwa sana kwasababu hakuna mahala ambapo pana hatari na mtu asipate hofu.
       Bila shaka ndiyo maana unaweza kuipata hata unapotaka kufanya maamuzi yatakayoamua hatima ya maisha yako ya mbele kama kuugua magonjwa yasiyo na dawa au kufanya mtihani.
                    (ii)  sababu za hofu
Hofu inaweza kusababishwa na mambo mengi sana ili mradi jambo lenyewe liashirie hatima ya hatari .Unaweza kupatwa na hofu kwasababu ya kufanya mtihani ambao utakaoamua hatima ya kisomo chako ikiwa ni uendelee au ubaki,kushiriki mchezo hatari,kupiga penati itakayoamua ushindi wa timu,kupokea taarifa za majibu ya vipimo vya ugonjwa usio na dawa,kugundulika kwa kosa la kijinai ulilofanya ,taarifa za ugonjwa au kifo  kwa mtu unayempenda au kumtegemea nk.

Tambua kuwa kwa binadamu au mnyama hofu ndiyo kinga ya kwanza katika kujihakikishia usalama.unaposhtushwa au kuona hatari. Kinachofanyika ni kwamba hofu hiyo itatumika kama kichocheo cha kushtua vipeleka taarifa  (fear triggers) katika ubongo wako ambapo itaamuliwa bila wewe kupanga (automatically) kwamba mapigo ya moyo yaongezeke,pumzi kupanda na misuli kukaa katika hali ya utayari kwa lolote litakalotokea.
             Hii humuwezesha aliyetishiwa au kushtushwa kuikimbia, kuiruka au kujilinda na hatari inayokuja,hapa ndipo unapoweza kuona faida ya mhemko (emotion) huu wa  hofu .

Kwa wengine ambao hawako sawasawa  huenda mbali zaidi, badala ya kupata faida hizo wao ndo kwanza hupoteza kilakitu na kujikuta wakidhoofika na kuishiwa nguvu.Sipendi nikuache na maswali hii hutokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa kuratibu matokeo yatokanayo na hofu (reguratory system mulfunctions). 
                       (iii)             Matokeo yaletwayo na hofu
Kunamatokeo mengi yanayoletwa na hofu ambayo si rahisi kutaja yote ila nitachukua yale yanayojitokeza zaidi katika chumba cha mtihani

                  (1)    Homa ya mtihani
                  (2)    Kuchanganyikiwa kwa muda  ( temporal mental confusion)

                     (1)homa ya mtihani
Homa husababishwa na mambo mengi unaweza kutazama linki hii kwa undani zaidi lakini homa ya mtihani ni Ile hali inayompata mtu baada ya kupata mshituko wa hofu anapoingia ndani ya chumba cha mtihani.Ni hali ya kujisikia ubaridi na kutetemeka na wakati mwingine kushindwa hata kutulia ndani ya chumba cha mtihani isitoshe hata kushindwa kuandika kabisa au kutoandika vizuri.

Kwa tafiti za kitaalamu inasemekana husababiswa na mabadiliko makubwa na ya haraka katika mwili kuanzia pale uliposhituka ambapo baada ya mchakato flani katika ubongo taarifa hufika katika( linkadrenal grands) nayo huzalisha(linkcortisol) homoni zitakazo kwenda katika damu na pelekea kuamshwa kwa nguvu mpya ya mapigo ya moyo na moyo kuchukua damu nyingi zaidi,kupumua huongezeka kwa mapafu kuhitaji oxgen nyingi na kuisafirisha haraka katika damu,na ongezeko hilo la oxgen huwezesha nguvu au (glucose) kuzalishwa kwa wingi zaidi na kwa haraka.Hali hiyo pia husababisha mwili kupokea nguvu haraka japo kwa wengine inaweza kuwa kinyume chake kama nilivyokwisha eleza awali.
.
Kwasababu hizo inaaminika kuwa katika kipindi hiki cha mwanzo tunaweza kuhisi joto na pengine kutoka jasho na baada ya kipindi kifupi mwili huanza kutafuta kurejea katika kipimo cha jotoridi lake la kawaida na hivyo katika kipindi flani tunaweza kuanza kuhisi baridi na kutetemeka.Hata hivyo hii ni hali ya mpito tu.

     (2)kuchanganjikiwa kwa muda  (link temporal mental confusion )

Hii ni hali inayomkuta mtu kwa upande wa kifikra na kumfanya kushindwa kuchukua maamuzi sahii au kuchukua maamuzi yasiyo sahii juu ya jambo alilolimudu alipokuwa yuko sawa.Tunapomzungumzia kuchanganyikiwa  tunazungumzia swala mtambuka ambalo wataalamu wanaendelea na utafiti ili kuweza kubaini vyanzo vyake na tiba yake.Hofu pia ni kisababishi kikubwa cha kuchanganjikiwa kwa muda na kupoteza kumbukumbu ndani ya chumba cha mtihani.

       (iv) jinsi hofu inavyoweza kukumaliza ndani ya chumba cha mtihani
kama utakuwa huna ufahamu wowote na swala la hofu ndani ya chumba cha mtihani inaweza kukumaliza kirahisi kabisa na kuzifanya jitihada zako zote za kusoma kuwa ni bure.
          Naomba uelewe kuwa hofu ni swala la kimhemko ambalo linatokana na mahusiano mema ya mwili kwa faida ya mwili katika kujilinda na hatari,yaani macho au akili ikigundua hatari taarifa zinasambazwa haraka katika mwili na mwili kuimarishwa haraka kwaajili ya kuchukua hatua stahiki.

      lakini ukumbuke kuwa kuna mambo mengine hata kama yanatia hofu lakini bado yanafaida kwetu, bila kujali hata kama mfumo wa mwili hautambui hilo.Moja ya hayo mambo ambayo pamoja na kushtua lakini yanafaida ni mtihani. Moja ya njia kuu ya kuipunguza hofu kabla ya kuuona mtihani ni kuyatambua mazingira ya ko ya mtihani kwanza kabla ya kuutambua mtihani wenyewe . Na mazingra yenyewe yanayoweza kukuondoa katika mtihani kupitia hofu ni:-

             (a)   kuuogopa mtihani::> wengi huogopa kuwa mtihani utakuwa mgumu na hivyo wataushindwa
.
             (b)  kuogopa kufeli na hivyo kushindwa kuendelea na masomo

Hizo ni sababu kuu mbili zinazoweza kuikaribisha hofu na kukumaliza kabisa ndani ya chumba cha mtihani.
Pamoja na tafiti nyingi ambazo zimeshafanyika lakini mpaka sasa bado hakujapatikana kinga ya hofu  kibailogia, bali zipo njia mbalimbali za kisaikolojia zinazoweza kuondoa hofu lakini si kuizuia maana ni kitendo cha kiautomatiki, yaani kinachotokea bila kupanga .

              (2)  MBINU ZA KUISHINDA HOFU NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI

                   (A)   Tambua kuwa kuogopa ni tabia ya asili ya binadamu hivyo isikuchukulie nafasi kwenye mtihani wako
                   (B)   Kama una hofu ya kushindwa kumbuka kuhusu uwezo wako na namna ulivyokuwa ukifanya vizuri hapo nyuma kabla ya mtihani.Vilevile wanaofeli huwa ni wachache.

                   (C)   Tarajia matokeo sawa na maandalizi yako.Epuka kujenga matarajio makubwa kupita kiasi
Kumbuka kadiri matarajio yanavyokuwa makubwa ndivyo na hofu huongezeka,kwa maana nyingine kubali hata kama utashindwa.Kufanya hivyo hakuta athili chochote katika ufanyaji wa mtihani wako  maana katika chumba cha mtihani hakuna jitihada nyingine zaidi ya kukumbuka ulichosoma na kujibu,hivyo utajibu kutokana na unachokumbuka.

                   (D)   Ondoa fikra potofu kwamba hukuwa unasoma sana kwa hiyo mtihani utakuwa mgumu kwako.Fikra hizo sio sahii kwakuwa mtu hufaulu kutokana na mbinu alizokuwa anatumia kusoma na si kusoma kwa masaa mengi rejea ( link.jinsi ya kusoma kwa kuelewa na kufaulu ).

                    (E)    Tambua kuwa mtihani huo sio wa mwisho hivyo unaweza kuupata mwingine hata kama hutapita awamu hii.
Kutokana na mada yetu kuwa ndefu nimeamua kuikata, awamu inayofuata tutaendelea na mambo ya muhimu ya kuyafanya dhani ya mtihani wenyewe. Nakuomba usikose .
     
 



Alhamisi, 30 Januari 2014

MARA NGAPI RASIMU YA KATIBA YA TANZANIA IMETAJA ELIMU ?

Hapa utazifahamu ibara zote zinazohusiana na elimu. ziko 32 na zimetajwa katika maeneo 25 ya katiba ya jamuhuri ya muungano.

KIFUPI ZIMETAJWA KATIKA MAENEO YAFUATAYO

1.       HAKI ZA BINADAMU,WAJIBU WA RAIA NA MAMLAKA ZA NCHI
2.       HAKI YA ELIMU NA KUJIFUNZA
3.       HAKI YA MTOTO
4.       HAKI YA WALEMAVU
5.       UCHAGUZI WA RAIS
6.       UTEUZI WA WAZIRI AU NAIBU WAZIRI
7.       UTEUZI WA MWANASHERIA MKUU
8.        KATIBU NA NAIBU KATIBU WA SECRETARIETI YA TUME YA UHUSIANO NA            URATIBU WA SERIKALI
9.       UCHAGUZI WA WABUNGE
10.         UCHAGUZI WA SPIKA WA BUNGE
11.       UTEUZI WA JAJI MKUU
12.       UTEUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA
13.     UTEUZI WA MSAJILI MKUU WA WA MAHAKAMA
14.     UTEUZI WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
15      MWENYEKITI NA MJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA
16.     UTEUZI WA WAJUMBE WA TUME HURU YA UCHAGUZI
17.     ELIMU YA MPIGA KURA
18.     UTEUZI WA MKURUGENZI WA  UCHAGUZI
19.     UTEUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
20.     UTEUZI  MWENYEKITI WA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI
21.     UTEUZI WA WAJUMBE WA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI.
22.     MAJUKUMU YA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI
23.     UTEUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI TUME YA HAKI ZA BINADAMU
24      KAZI ZA TUME YA HAKI ZA BINADAMU
25.     UTEUZI WA MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKAR

 NA HIZI NDIZO IBARA NA MAELEZO YAKE
        
       HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RIA NA MAMLAKA ZA NCHI

       Hii ni ibara ya nyongeza maana haijataja elimu mojakwa moja japo inahusiana moja kwa moja na elimu. Vinamba vidogo havihusiki katika namba za ibara bali ni katika kuhifadhi kumbukumbu ya mara ambazo katiba imetaja elimu.

Ibara 30.
Ibara ndogo (1).
kifungu ( A).
kifungu kidogo( iii).

kila mtu ana haki na uhuru  kufanya ugunduzi,ubunifu na utafiti wa sanaa,sayansi na  mapokeo ya asili

Ibara ya 41.
Ibara ndogo (2)

1.Kila mtu anayeishi katika jamuhuri ya muungano ana haki ya kuishi katika mazingira safi,salama na ya kiafya,inahusisha haki kwa kila mtu kutumia maeneo ya umma au sehemu mbalimbali za mazingira yaliyotengwa kwa madhumuni ya burudani,
elimu,afya,ibada,utamaduni na shughuli za kiuchumi.

     2. HAKI YA KUJIFUNZA

Ibara ya 42.
Ibara ndogo (1)
kila mtu ana haki ya

    2  (a)    Kupata Fulsa ya kupata elimu bora bila ya vikwazo

    3  (b)   Kupata elimu bora ya msingi bila malipo na inyomtayarisha kikamilifu mwanafunzi ama kuendelea na elimu ya ngazi inayofuata au kuweka msingi wa kuanza kujitegemea;

    4 (c)    Kupata elimu bora inyotolewa nje ya utaratibu wa umma kwa gharama nafuu; na

    5 (d)   Kupata fursa sawa ya kupata elimu ya juu ili mradi anasifa stahiki kupata elimu hiyo,bila ubaguzi wa aina yoyote.

6  Ibara ndogo ya  (2) kwa madhumuni ya ibara ndogo (1),

kila mtu anahaki ya kuchagua taaluma na ajira anayoitaka kwa mujibu wa elimu yake na ujuzi alionao.

      HAKI YA MTOTO

Ibara ya 43.- 
Ibara ndogo ya (1) 
kila mototo ana haki ya –

7   (c) kucheza na kupata na kupata elimu bora

HAKI ZA WALEMAVU

8  Ibara ya 45.-
Ibara ndogo(1)
kifungu (b)
mtu mwenye ulemavu anastahiki kupata elimu kwa kutumia vifaa maalumu na kushiriki katika shughuli za kijamii.

9  Ibara ya 45.
Ibara ndogo1 
kifungu cha(d)
Kutumia lugha za alama maandishi na nucta nundu,maandishi yaliyokuzwa au njia nyingine zinazofaa.

10  Ibara ya 45.-
Ibara ndogo (1)
kifungu cha (e)
mtu mwenye ulemavu anahaki ya kusoma, kujifunza na kuchanganyika na watu wengine
                    
                    
11  Ibara ya 46.-
Ibara ndogo ya (1).
kifungu cha (b) 
mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha makundi madogo katika jamii: kupewa fursa maalumu za elimu na fursa za kujiendeleza kiuchumi na fursa za ajira.

12  Ibara ya  46. 
Ibara ndogo (2)
 serikari na mamlaka za nchi zitachukua  hatua za makusudi za kukuza na kuendeleza shughuli za kiuchumi na kuweka miundo mbinu ya makazi ,elimu na afya kwaajili ya kizazi cha sasa na vijavyo vya jamii ya watu walio katika makundi madogo.

UCHAGUZI WA RAIS

13  Ibara ya 79-
Ibara ndogo ya (1)
kifungu cha (e)
mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa na kushika madaraka ya urais wa jamhuri ya muungano ikiwa anayo shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

UTEUZI WA WAZIRI AU NAIBU WAZIRI

14  Ibara ya 101
Ibara ndogo ya (1)
 kifungu cha(B)
mtu atateuliwa kuwa waziri au naibu waziri wa serikari ya jamhuri ya muungano ikiwa awe na shahada ya  chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.

MWANASHERIA MKUU

15  Ibara ya 104.
Ibara ndogo (2)
Mtu anayestahili kuwa mwanasheria mkuu atakuwa na sifa zifuatazo,
Kifungu cha (b)

awe Na shahada ya sheria ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.

KATIBU NA NAIBU KATIBU WA SECRETARIETI WA TUME YA UHUSIANO NA URATIBU WA SERIKALI.

16  Ibara ya 112-
Ibara ndogo (2)
kifungu(b)
 mtu atateuliwa kuwa katibu au naibu katibu ikiwa ana shahada kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria.(secretarieti ya tume ya uhusiano na uaratibu wa serikali.)

UCHAGUZI WA WABUNGE.

16  Ibara ya 125.
Ibara ndogo (1)
kifungu (b)

Mtu yeyote atakuwa na sifa za kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge endapo anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili au kiingereza na elimu isiyopungua kidato cha nne.

UCHAGUZI WA SPIKA WA BUNGE.

17 Ibara ya 135.
Ibara ndogo 1
kifungu  (a) 
angalau awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria.
Uteuzi wa jaji mkuu

JAJI MKUU

18  Ibara ya 158.
Ibara ndogo (3)
Kifungu cha (b) 
Mtu ataweza kuteuliwa kuwa jaji mkuu endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka arobaini na tano na mwenye sifa  ya uadilifu ,tabia njema na uaminifu na awe na awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika na mamlaka inayoshughulikia elimu ya juu katika jamhuri ya muungano. Inajirudia kwa naibu jaji mkuu(159)2

UTEUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA.

19  Ibara ya 169.
Ibara ndogo  (3)
Kifungu(b)

 mtu ataweza kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa mahakama ya rufani endapo atakuwa na sifa zifuatazo. Awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambulika na mamlaka inayo shughulikia elimu ya juu katika jamhuri ya muungano,na
Vivyo hivyo kwa makamu mwenyekiti wa mahakama ya rufaa.

Sifa hiyo inatumika hata kwa majaji  wa mahakama ya rufaa kama ilivyoainishwa kwenye ibara 169.3

MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA.

20  Ibara ya 176.
Ibara ndogo (2) 
Kifungu (b) 

Mtu ataweza kuteuliwa kuwa msajili wa mahakama endapo atakuwa na sifa zifuatazo:-

Awe na shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa  na mamlaka  inayoshughulikia elimu ya juu katika jamhuri ya muungano.

TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA.

21  Ibara ya 180
Ibara ndogo (1)
Kifungu (g) 
 kutakuwa na tume ya utumishi wa mahakama ambayo itakuwa na wajumbe nane watakaoteuliwa na rais kama ifuatavyo;

 wawakilishi wawili wa vitivyo vya sheria kutoka vyuo vikuu,mmoja kutoka Tanganyika na mmoja kutoka Zanzibar watakaopendekezwa na vyuo vya elimu ya juu husika.

MWENYEKITI NA MJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA.
22  Ibaraya186.
Ibara ndogo (3)
kifungu cha(b)

Sifa za mwenyekiti na mjumbe wa tume ya utumishi wa umma zitakuwa kama ifutavyo,

Awe na shahada ya chuo cha  elimu kinachotambulika  kwa mujibu wa sheria za nchi.

MJUMBE WA TUME HURU YA UCHAGUZI.

Mjumbe wa tume huru ya uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo:
23  Ibara ya 190
Ibara ndogo (6)
kifungu(d).
Awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu 
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

ELIMU YA MPIGA KURA.

24  Ibara ya 193.
Ibara ndogo (2) 
 tume huru ya uchaguzi itakuwa  pia na wajibu wakutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi au kura ya maoni na kuratibu utoaji wa elimu ya uraia kuhusu uchaguzi na kusimamia asasi za kiraia,taasisi au makundi ya watu watakaotoa elimu hiyo.

MKURUGENZI WA  UCHAGUZI.

25  Ibara ya 195
Ibara ndogo (2)
mkurugenzi wa uchaguzi atakuwa na sifa zifuatazo,

Awe na shahada ya chuo cha elimu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.

26  Ibara ya198.
Ibara ndogo (2).
Kifungu (d)
msajili wa vyama vya siasa atakuwa na sifa zifuatazo,

Awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

MWENYEKITI WA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI

27  Ibaara ya 200.
Ibara ndogo (5)
Kifungu cha (b) 
sifa za mwenyekiti zitakuwa kama ifuatavyo:

Mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika  kwa mujibu wa sheria za nchi.hii ni hata kwa makamu mwenyekiti wa tume.

WAJUMBE WA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI.

28  Ibara ya 201
Ibara ndogo (2)
Kifungu cha (b)
sifa za wajumbe wa tume ya maadili ya uongozi na uwajibikaji zitakuwa kama ifuatavyo,

Mtu mwenye shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi:

MAJUKUMU MAHUSUSI YA TUME YA MAADILI YA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI.

29  Ibara ya 203.
Ibara ndogo (2)
Kifungu cha (g) 

bila kuathili masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1)majukumu mahususi ya tume yatakuwa ni: kutoa elimu kwa umma kuhusu maadili na miiko ya viongozi wa umma.

TUME YA HAKI ZA BINADAMU.
Sifa za mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa tume zitakuwa kama zifuatazo:

30  Ibara ya 208 .
Ibara ndogo ya (5)
Kifungu cha (b)
Mtu mwenye shahada ya sheria kutoka chuo cha elimu ya juu kinanchotambulika kwa mujibu wa sheriaza nchi.

KAZI ZA TUME YA HAKI ZA BINADAMU.

Kazi na majukumu ya tume ya haki za binadamu yatakuwa kama ifuatavyo:


31  Ibara ya  210.
Ibara ndogo (1)
Kifungu cha (d)
kufanya utafiti na kutoa elimu kwa uma kuhusu haki za binadamu na utwala bora .

MDHIBITI NA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKARI

32  Ibara ya 216
Ibara ndogo (2)
Kifungu cha (b)
mtu ataweza kuteuliwa kuwa mdhibiti  na mkaguzi wa hesabu za serikari ikiwa ansifa zifuatazo:
Amefuzu mafunzo  ya juu ya uhasibu na kusajiliwa na mamlaka husika

hiyo ni sehemu tu ya katiba iliyotaja elimu kusoma Rasimu nzima 

Jumamosi, 25 Januari 2014

JINSI YA KUUFANYA MWANDIKO WAKO UVUTIE


Kuwa na mwandiko unaovutia ndiyo ndoto ya kila mtu anayeshughulika na uandishi wowote.Hata hivyo siamini kwamba kuna mtu ambaye hajawahi kukutana na swala linalohusu kuandika .Bila kujali kiwango chako cha elimu mada hii fupi inaweza kukuletea mabadiliko makubwa katika uandishi wako.

Mada hii nimeigawanya katika vipengele vinne :-

(i) Chagua mwandiko unaoutaka

(ii) Mbinu za kufanikisha mwandiko unaoutaka
(iii) Umuhimu wa kuwa na mwandiko mmoja
(iv) Ubadilishaji wa mwandiko na madhara yake

(i) CHAGUA MWANDIKO UNAOUTAKA


kabla ya kufikiri kuhusu kuboresha hati ya uandishi wako jambo la muhimu unalotakiwa kufanya ni kuelewa aina ya mwandiko unaoutaka. Kuna mwandiko unaotokana na maumbo tofauti ya herufi kama ifuatavyo:-

Herufi pana,herufi nyembamba au herufi za wastani (ukubwa wa wastani) ambapo ndani yake kuna

(a) Mwandiko wa Herufi ndefu, fupi au za wastani

(b) Mwandiko wa maneno ya kuunganisha ( mcharazo) au herufi za umbali
(c) Mwandiko wa sentensi za kugusa mstari chini au za kuning’inia (maneno yasiyogusa juu wala chini)  kwa wanaotumia kurasa zenye mistari.
kwa kuutazama muundo huo hapo juu unaweza kutengeneza aina tofauti tofauti za mwandiko, nyingi kwa kadiri upendanyo mojawapo ya hizo ni:-

         kundi la kwanza { mwandiko wa herufi ndefu.}


*  Mwandiko wa herufi pana ndefu za kuunganisha (mcharazo mpana) au kutounganisha

*  Mwandiko wa herufi nyembamba ndefu za kuunganisha au kutounganisha (mcharazo mwembamba)
*  Mwandiko wa herufi za ukubwa wastani ndefu za kuunganisha au kutounganisha (mcharazo urefu wastani)
Kundi la pili {mwandiko wa herufi fupi}
*  Mwandiko wa herufi pana fupi za kuunganisha (mcharazo)au kawaida
*   Mwandiko wa herufi nyembamba fupi za kuunganisha (mcharazo) au kutounganisha
*    Mwandiko wa herufi za ukubwa wastani fupi za kuunganisha au kutounganisha

         Kundi la tatu { mwandiko wa herufi za urefu wa wastani} huu unaweza kuwa,


*    Mwandiko wa herufi pana urefu wastani kuunganisha( mcharazo) ama kutounganisha

*     Mwandiko wa herufi nyembamba urefu wa wastani kuunganisha ama kutounganisha
*     Mwandiko wa herufi za ukubwa wastani urefu wastani za kuunganisha ama kutounganisha

Hapa unaweza kupata aina nyingi zaidi ya hizo kulingana na utakavyoamua ila nitoe pendekezo.utafiti wangu umeonyesha kuwa:-


*    Mwandiko mpana unapendeza ukiwa mfupi na usiounganishwa sana maneno yake.

*     Mwandiko mwembamba unapendeza ukiwa mrefu ukiunganishwa maneno yake.
*    Mwandiko wa upana wa wastani unapendeza ukirefushwa na hata bila kurefushwa {kimo}

(ii)            MBINU ZA KUFANIKISHA MWANDIKO UNAOUTAKA


Hapa inabidi turudi nyuma kwenye zama za utoto bila kujali elimu yako wala umri hatua kwa hatua


(a)     USHIKAJI WA KALAMU (ushikaji wa kalamu unaweza kuathili mwandiko wako moja kwa moja bila kujali uzoefu)


* Wanaopendelea mwandiko wa herufi ndefu , wengi wao hushika kalamu juu kidogo kiasi cha sm 1 kutoka chini ya kalamu na zaidi

*    Wanaopendelea mwandiko wa herufi ndefu wastani, wengi wao hushika kalamu kwenye wastani wa sm 1 kutoka chini ya kalamu.
*    Wanaopendelea mwandiko wa herufi fupi hasa pana, wengi wao hushika chini zaidi au sm 1 kutoka chini ya kalamu.
Hapo sio tageti ya somo letu bali naomba uwe makini katika hatua inayofuata.

(b)FANYA ZOEZI LA MAUMBO YA HERUFI


Kumbuka kabla hujaanza zoezi chagua unataka mwandiko wa aina gani,kosa kubwa tunalofanya huwa tunaanza kuandika bila kuwa na uchaguzi wa mwandiko gani tuukao .kwa wale wa Kiswahili na kiingereza ni herufi A to Z. Panga herufi zako kwenye karatasi yenye mistari kama sio daftari.hakikisha unaanza na herufi ya kwanza unaiandika kwa ustadi unaouweza ukiazia mwanzo wa mstari mpaka mwisho ukifuatia na herufi inayofuata kwenye mstari unaofuata kama unavyoona katika mfano huu,


a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a a 

b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b b 
c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c c
d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d d

baada ya zoezi hilo utagundua kuna herufi kwako zina ugumu wa kuziunda zifanyie kazi kwa mfano huohuo mpaka zitokee unavyopenda bila kusahau aina ya mwandiko uliochagua na kama mmoja unakuwa mgumu badilisha aina ya mwandiko.Hatua hii ni ya taratibu na usiunganishe herufi zako.

Baada ya kumaliza hatua hii njoo hapa chini,

(b)FANYA ZOEZI LA MAUMBO YA MANENO


Ukianzia na zile herufi zilizokuwa kwako ngumu kwenye hatua ya kwanza, mfano kama kwako k,h,g,z na r ndo zilikua ngumu, unda maneno yanayoyumia herufi hizo na kufanyia mazoezi hata kama hazileti maana .Kumbuka kama kutakuwa na herufi zisizopendeza katika maandishi yako zinaweza kuharibu mwonekano wa mwandiko wako wote na ukaonekana hujui kuandika au una hati chafu.kwa kufuata mfano huu unaweza kuona cha kufanya.


kihagazira kihagazira kihagazira kihagazira kihagazira kihagazira


Fanya zoezi hilo mpaka uone umefaulu zile herufi zote zinazosumbua.


(C)FANYA ZOEZI LA UANDISHI WA SENTENSI


*  Ikiwa sasa umeshafuzu kwa mazoezi yaliyotangulia malizia na uundaji wa sentensi kwa kuamua sasa kufuata mtindo wa kuning’iniza maandishi au kugusisha kwenye mstari kwa chini kama utakavyopenda.

*   hakikisha unafuata taratibu zote za mwanzo kama ulivyoanza katika herufi hadi maneno huku ukigeuza maneno hayo kuwa sentensi.
*  Endesha zoezi taratibu ukipanga unachotaka kitokee na ukidhibiti mwandiko usibadilike yaani herufi moja kwa kurasa nzima .hapa ninamaana herufi hupendeza sana kama itakapoandikwa ikafanana na zilizotangulia.na huo ndo uzuri wa mwandiko wenyewe yaan herufi( A) niliyoiona mwanzo wa ukurasa inafanana na ile iliyopo mwishoni mwa kurasa.
* Kumbuka kama utaamua kugusisha mstari basi ni maandishi yote, na kama yataning’inia basi ni yote tena zingatia nafasi unayoiacha kutoka kwenye mstari mpaka maandishi iwe ni moja ili kuleta mvuto wa maandishi yako.
*  Jambo la mwisho la kuzingatia kumbuka kuacha nafasi inayo fanana kati ya neno na neno maana hapo ndipo panapo leta ustadi wa uandishi wako pole maneno yako yatakapo kuwa yanaonekana yameachana kwa nafasi inayofanana na herufi zake zikifanana.

(d)UANDISHI WA KWENYE KARATASI ISIYO NA MISTARI


Hapa ndipo penye changamoto kwa walio wengi, lakini zoezi ni rahisi sana.

*Chukua karatasi isiyokuwa na maandishi ukiwa na kalamu yako mkononi.

*Laza karatasi yako mezani kisha chukua kalamu yako na uisogeze kwa juu kabisa upande wa kushoto na uilaze huku kile kichwa cha kuandikia kikiwa kinakutazama wewe.


*Isogeze kalamu yako nyuma yaani kama mtu anaeiondoa kwa kuiburuta mpaka kile kichwa cha kalamu tu au pale kalamu inapoanzia kupungua ukubwa au kubonyea ndiyo pabakie ndani ya karatasi.kwamaana nyingine kalamu yako itakuwa ndani ya karatasi yako kwa wastani wa sm1 tu au pungufu.


*palepale ilipo kalamu yako bila kuhamisha isimamishe kisha weka alama ya wino utakayoiona wewe tu, kisha kwa kipimo kilekile au usawa uleule uliopo sogeza kalamu upande wa kulia mpaka usawa wa kati weka alama nyingine, vivyohivyo na upande wa kulia. Hivyo kama utaamua kupiga mstari kutoka alama ya upande wa kushoto kwenda alama ya kulia utapata eneo la juu ya karatasi yako kiasi cha sm1 likiwa limetengwa .sasa usipige huo mstari ila fanya hivi,


*  kwa kufuata alama ulizoziweka ambazo unaziona wewe tu ,zifanye kuwa ndo dira yako ya mstari wako wa kwanza wa uandishi wako,nina maana hiyo ndo itakuwa point yako ya juu ya maandishi yako ya mstari wako wakwanza.kwa maana nyingine kimo cha maandishi yako kitaishia kwenye alama hizo.


*  Nyoosha mstari wako wa maandishi wa kwanza kwa kutumia usaidizi huo wa alama hizo kwa ustadi mkubwa.


*   Mistari inayofuata utahakikisha kile kiasi cha nafasi kati ya maandishi ya juu na chini unachoacha kwenye herufi yako ya kwanza, ndo utakachoacha hata kwenye herufi zako zinazofuata,hivyo itafanya hata mstari unaofuata unyooke.Utaendelea na zoezi hilo mpaka mwisho na utajikuta unanyoosha maandishi hata bila alama yeyote.


(III))UMUHIMU WA KUWA NA MWANDIKO WA AINA MOJA ,(HII ITAKUSAIDIA KATIKA YAFUATAYO)


(a)  itakuwa ndo nembo yako kwa upande wa maandishi

(b)  Itakusaidia kuuboresha mwandiko wako baada ya kuuzoea
(c)  Itakuwa rahisi watu kutambua na kuheshimu kisomo chako kupitia mwandiko wako
(d)  Itakusaidia katika usahihishaji wa mitihani yako kuwa na hati inayosomeka pasi na shaka
(e)  Itakupatia kipaumbele katika uombaji wa kazi kwasababu wengi watahitaji kuona uandishi wako wa mkono(barua nyingi za kazi huandikwa kwa mkono)
(f)  Unachokiandika kinaweza kusomwa na mtu yeyote bila usaidizi wako nk

(iv)  Ubadilishaji wa mwandiko na madhara yake


(a)   Huwezi kuuboresha kwasababu hutouzoea

(b)  kuwatia watu mashaka juu ya kisomo chako
(c)  Faida zote zilizotajwa hapo juu utazikosa
Kazi kwako mwenzangu kuendelea kubaki na hati yako ya mashaka au kutumia mbinu mbadala kama zilivyoelezwa hapo juu kujinasua, nakutakia siku njema na karibu tena.







NIFANYE NINI KABLA YA KUJIENDELEZA KIELIMU?

Japo tunafahamu kwamba elimu ndiyo ufunguo wa maisha lakini swala la kujielimisha sio swala la kukurupuka kama ilivyo kwa wengi na matokeo yake huambulia majuto baada ya kupata mrejesho wasio utarajia.Mtu anaweza kujiendeleza kielimu kwa lengo la kupata cheti ,kuiga, kuvutiwa na ajira njenje,kutaka kuwa msomi,ndugu zake wote wamesoma ,wazazi wameamua,bwana au mke kashauri nk.Hizi zote sio sababu sahii za kujiendeleza kielimu na inatokana na kutofahamu nini cha kufanya kabla ya kujiendeleza kielimu.

Kupitia mada hii fupi utaweza kuondoka na kitu muhimu kabisa kitakacho kusaidia katika maamuzi yako ya kujiendeleza

(1).LENGO LA KUJIENDELEZA KIELIMU
Kabla ya kujua nini cha kufanya kitu muhimu unachotakiwa kufanya ni kutambua lengo la kujielimisha .

 A.kupunguza ujinga
Nimetumia neno kupunguza ujinga kimakusudi hata kama nitatofautiana na watu wengi. Hapa ninamaana  kuwa ujinga hautaisha kwa  mwanadamu  hata kama atapewa  miaka elfu ya kuishi duniani, bado atahitaji kujifunza.kwasababu ujinga maana yake ni hali ya kutojielewa au kutojitambua au kupungukiwa na ujuzi flani ambao hata kwa miaka mingapi huwezi kujua kilakitu.




 Kwa maana hiyo ni lazima kujielimisha kwanza ili kupunguza ujinga wa kutojitambua.

kupitia kujielimisha ndoyo unaweza kutambua thamani yako ,mapungufu yako ,mazingira yako,kipaji chako,na mengineyo japo kwa uchache.

B.kuimarisha kipaji na ndoto.
Kila mtu anakipaji na ana ndoto bila kujali ameelimika au hajaelimika .Elimu ndiyo inayoweza kuimarisha hizi ndoto na vipaji, kwasababu kipaji bila elimu hakitafanyakazi  na ndoto bila elimu itapoteza mwelekeo.pia naomba utambue kuwa kunatofauti kubwa sana kati ya kipaji na ndoto ambapo inanibidi nifafanue kidogo ili kipengele hiki cha kuimalisha kipaji na ndoto kieleweke sawsawa.




(i).kipaji        
Ni ule uwezo wa asili tunaozaliwa nao wa kufanya jambo flani kipekee kabisa bila kufanana na mtu na huwa hakibadiliki kutokana na mazingira au wakati.


Kipaji kinaweza kutambulika ,kuendelezwa au kuimarishwa kupitia elimu.nimewahi kufanya utafiti kwa kuwahoji wanafunzi wengi wa sekondari waniambie wanakipaji gani,wote waliishia kuniambia wanakipaji cha fashon show,kudansi,kuimba,kucheza mpira na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Nilichogundua ni kwamba wamekosa elimu ya kujitambua na kutoelimishwa kuwa hata hesabu,biology,chemistry,geograph,lugha,computer, uandishi navyo ni vipaji kama vingine,kwasababu walioandika tunayojifunza na yanayokuja ni matokeo ya vipaji vilivyotangulia.Sio lengo langu kufundisha kuhusu vipaji ila inahusiana na mada yetu.


(ii).ndoto au maono
Hii ni shauku, hamu  kiu au muono wa mbele  wa kupata au kuifikia hali flani ambayo huwa inabadilika badilika kutokana na mazingira.KWA KIFUPI INAITWA PICHA YA AKILINI.


Wakati flani mtu huwa na ndoto kutokana na mazingira aliyonayo.  Wakati mwingine wote tunaweza kuwa na ndoto ya aina moja mfano kuongoza  NGO ,SHULE ,SOCIAL NETWORK,AU KUWA NA NYUMBA NZURI GARI ZURI au pengine KUWA MTU FULANI nk.tofauti na kipaji kila kimoja kitajitokeza kwa namna ya upekee sana.


Vile vile ndoto huweza kubadilika kwa kuathiliwa na  mazingira,elimu,kipato,makundi nk.leo mtu anaweza kutamani kuwa daktari kwasababu hana elimu na hajui udaktari ni nini  unapatikanaje na kwa sifa zipi.


Vivyohivyo mtu anaweza kuwa na ndoto ya kuwa rubani ,kuwa mchezaji maarufu,muimbaji maarufu nk.mtu huyu baadaye akielimika anaweza kubadilisha ndoto yake na kwenda mbali zaidi au kufahamu hatua za kuchukua kuifikia.

 (2). MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUCHUKUA HATUA YA KUJIELIMISHA

 A.Tambua kipaji chako kwanza  na sio ndoto




Nimeshaeleza kwa kirefu kuhusu ndoto na kipaji hivyo unapaswa kutambua kipaji chako.Makosa makubwa tunayoyafanya ni kukimbilia kutambua ndoto kabla ya kipaji.

Utatambuaje kipaji chako?

Ni rahisi sana .piga picha maisha yako yaliyopita na kuona mambo machache katika haya

(i)  Ni jambo gani kati ya mambo yote kwako ulikuwa unalimdu kirahisi kuliko yote

(ii) Jambo ambalo wazazi waalimu na watu au marafiki zako wanakubali kwamba unaliweza sana

(iii) Jambo ambalo ukishindanishwa na watu wengine wewe unakuwa wa kwanza au nafasi za juu


(iv)  Jambo ambalo wazo au idea yake inakuja bila kutumia nguvu wala mafunzo mengi


(v)   Jambo ambalo hata ukijitahidi kulikwepa na kufanya mengine bado unalifanya vizuri   kuliko hilo jipya unalolifanya.


(vii) Jambo unalolifanya kwa usahihi mkubwa bila kutumia jitihada nyingi kama wengine


(vii) Jambo ambalo akili na mwili wako vinakubaliana nalo kirahisi kulifanya hata kama wengine wanaliogopa.

Nafikiri maelezo hayo hayahitaji elimu ya kifilosofia au saikologia kuyaelewa,unaweza ukaanzia hapo katika kuchagua ujielimishe katika lipi na si kuingia kila jambo na baadaye kujuta Ukipoteza wakati.Jiulize kuwa kama Christiano Lonaldo angefuata upatikanaji wa ajira na kuamua kosomea ualimu leo angekuwaje?.


B.     Tambua kuwa wewe ndiye mwenye jukumu la kwanza katka kujielimisha
Kumbuka ,mwalimu ,mlezi  au chuo vinachukua nafasi ya pili katika kukuendeleza kielimu.Ikitokea chuo au shule  imesitisha masomo au kufungwa  au mwalimu kutokuwepo  au mzazi kutokuwepo au kufariki au kwa namna yeyote ile mtu anayeshughulika na kusaidia upatikanaji wa elimu yako kutokuwepo, jukumu litabaki kwako kwa asilimia mia.


Ili kipaji chako kiweze kuchanua ni lazima upate elimu inayohusiana na unachotaka kukitumikia ,kwasababu hiyo utakuwa na jukumu la kuhakikisha unajielimisha kwa namna yoyote ili kupunguza ujinga hasa kwa kile unachotaka kukitumikia.


Zipo njia nyingi sana za kujielimisha binafsi  hii ni pamoja na vitabu,semina,majarida ,magazeti,mitandao,tafiti nk.


C. Tambua Bidii ni kusoma na sio mahudhurio
utakuwa ni upotezaji wa muda kama hutajua jukumu lako la msingi katika kujiendeleza ukazingatia mahudhurio na si masomo .Unachotakiwa kufahamu kuwa tuhudhurie darasa au tusihudhurie kujielimisha ni lazima.kwa hiyo kujielimisha ndiyo liwe jukumu lako la msingi.





D. Uchaguzi wa shule au chuo ni muhimu
Unachopaswa kuzingatia katika uchaguzi wa shule au chuo ni ,uwezo wako wa kukabiliana na gharama,mazingira( hapa ni pamoja na teknologia inayotumiwa na shule au chuo, jiografia,umbali,hali ya kimjini au akijijini,nk.)  unapaswa kufahamu hayo yote ili yasije kukupotezea muda wa kujifunza mazingira kwa wakati huohuo ukijifunza ulichokiendea.kitu kingine cha muhimu ni kuangalia uhalali wa chuo au shule pamoja na uwezo wa kukupatia elimu unayoitaka.


E.     Tambua vikwazo vya upatikanaji wa elimu yako
(i) kwa mfanyakazi. Ratiba yako kama itakuwa endelevu, kama sivyo weka mkakati ikiwezekana  badilisha kazi


(ii) kijana wa nyumbani. Jiulize kama una mtu wa kugharamia masomo yako. kama utasoma nyumbani notes utapata wapi?, practicals  utaziendesha vipi?.


(iii) masomo online. Unavifaa vya kutosha kupokelea masomo mtandaoni?,unauelewa wowote kuhusu mtandao?.Umechukua tahadhari yoyote kuhusu uharamia wa mtandao?


(iv) masomo ni mbali.Jiulize kama utamudu usafiri pamoja na gharama za maisha?,kama la,basi bora usome karibu

(iv) UMRI.Tambua umri wako kama unaweza kukuathili katika masomo yako.Tambua pia taratibu za shule na chuo kama zinaweza kukuathili kutokana na umri wako.


Hakikisha umetambua vikwazo vyote na kuvitafutia ufumbuzi mapema.


F. Tambua fursa za kipaji chako




Ni muhimu kabla ya kuamua kujielimisha tambua kwanza fulsa za kipaji chako.kama unafikiri wewe ni-


(i)  Mzuri kwenye hesabu.Unaweza kufanya kazi gani? labda baadaye kuwa space man (astronaut)->” hawa ni wataalamu wanaofanya majaribio ya kisayansi angani”,mwanamahesabu,engineer  wa -> sayansi ,majengo,ndege,meli,mashine, nk.


(ii)  Mzuri kwenye jiografia.Unaweza kuwa mtafiti wa wanyama pori,au wa anga au wa hali ya hewa,madini,viumbe bahari, nk


(iii)   Mzuri kwenye kilimo.Unaweza kuwa mtafiti wa kilimo,afisa kilimo,mkulima,mtaalamu wa mifugo,mfugaji wa kisasa wa samaki nk.

(iv)  Mzuri wa sanaa .Unaweza kuwa mtaalamu wa lugha ukitumika kutengeneza programu mbalimbali za computer zinazohusiana na lugha kama speech synthesis,mashine translation,speech recognition,kutengeneza kamusi,kufundisha lugha,kuimba ,kucheza ,kutengeneza filamu ,mwanafalsafa,mwanasaikologia ,mwandishi wa vitabu nk.

(v) Mzuri wa biashara.Unaweza kuwa mfanya biashara au kufanya kazi katika mabenki,makampuni ya kibiashara,kazi za kiuhasibu nk.

(vii)Mzuri kwenye sayansi. Unaweza kuwa daktari,Muuguzi,mfanyakazi wa maabara,mkemia,nk

Hii ni mifano tu ya fulsa unazoweza kuzitazama ambapo wewe utatazama katika kipaji chako kabla ya kuamua kijiendeleza kielimu.

G.     Anza masomo kabla ya kuandikishwa shule
Kosa kubwa ambalo watu wengi hufanya katika kujielimisha ni kuendelea kusubiri na kusubiri mpaka aingie darasani ndipo aanze masomo.

*Jukumu la kusoma ni la kwako  hivyo kama unania ya dhati ya kujiendeleza basi anza sasa kusoma .wakati mwingine unaweza usinielewe, ninaposema anza sasa kusoma nina maana kile unachoweza kukisoma sasa anza kulisoma.


*Mfano kama wewe unataka kujiendeleza na masomo ya secondary na unafahamu kuwa lugha itakusumbua basi anza kujifundisha lugha kwa kujua misamiati ya maneno usiyoyafahamu.kama hilo haliwezekani basi anza kusoma Kiswahili kwa kutumia kitabu utakachokinunua kwenye maduka maalumu ya vitabu vya kiada.

*unataka kusoma kozi flani katika chuo, anza kuchukua elimu ya ujumla kutoka kwenye notes za waliotangulia kusoma kozi unayokusudia kuisoma na kama unaweza kupata kozi nzima, soma yote .Usifikiri kuhusu kujiandikisha shule kwanza, kitu cha muhimu kwako kwanza ni elimu.

 Hii inamaana gani?,
Kuelimika ndiko kunakotoa  mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo  na sio vyeti. Sikatazi kutafuta cheti, bali elimika kwanza.watu wengi  hawajajikita kwenye dhana ya kuelimika ili walete mabadiliko na badala yake husubiri  vyuoni kwa muda mrefu  ili wapate vyeti na kuja kujifunza upya kitu kilekile walichokisoma.


Wakati mwingine hujifunza kupitia hata kwa watu wasiopitia darasani.Ikatae hali hii itakayo punguza kasi ya kukitumikia kipaji chako na kuchelewesha ndoto zako.


Nakushukuru kwa muda wako ulio utoa kupitia mada hii fupi inayohusu nifanye nini kabla ya kuamua kujiendeleza kielimu?   Naamini umenufaika na mengi karibu kwa mada nyingine.