FREE CLASS

UWIANO WA UJUZI NA UHARIBIFU WA DUNIA

Ujuzi tunaweza kuufafanua kwa namma kuu mbili
(a) Ni maarifa au uwezo wa kufanya jambo fulani anaokuwa nao mtu
(b) Hali ya kutambua kitu fulani au kuwa na ufahamu uliopatikana kwa uzoefu.
Ninaposema uwiano wa ujuzi na  uharibibu ninamaana ya uwezo au uzoefu ulio ndani ya binadamu juu ya kitu fulani ambao wakati mwingine unatumika vibaya na kufanya mambo kuharibika badala ya kuwa bora.Ndugu yangu ujuzi ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu,kwasababu hakuna lolote linaloweza kufanywa bila ujuzi .katika mada hii naomba niongelee jinsi ujuzi unavyoweza kutumika kuleta uharibifu unaoweza kuiangamiza dunia na kuifanya isiwe mahali panapofaa kwa maisha ya binadamu tena.

1. LENGO LA KUTAFUTA UJUZI NA MATAMANIO YA BINADAMU
(A) LENGO LA KUTAFUTA UJUZI
Lengo kuu la kutafuta ujuzi ni kuutumia katika kujiendeleza na kuiendeleza dunia na sio kuibadilisha kwa maana ya kuifanyia mabadiliko kutoka hali yake ya asili.
*Ujuzi unatakiwa utumike kurahisisha maisha na kumfanya mwanadamu kuishi raha mstarehe
*Ujuzi unatakiwa kwaajili ya kuunda zana za kurahisisha kazi na kuzikarabati.
*Ujuzi unatakiwa kurejesha au kukarabati kila uharibifu unaotokea katika mwili wa binadamu.
*Ujuzi unatakiwa kutumika kuboresha na kukarabati kila uharibifu unaotokea katika dunia.
kilakitu kinachoharibika huwa kinahitaji ukarabati au kurejeshwa katika hali yake ya mwanzo kabla ya uhalibifu. Tutambue kuwa dunia imefanywa kuwa hai kutoka na utimamu wa vijenzi vyake na inahitaji ukarabati kila inapopatwa na uharibifu ,naam ukarabati wa kila uharibifu na si uharibifu flani flani tu kama ambavyo tumekuwa tukifanya; mfano kupanda miti kwa lengo la kupunguza hewa ya okaa huku tukisahau kuwa kuna gesi nyingine tulizozalisha kutokana na kemikali zilizosambaa hewani kimakosa au kwa makusudi.Gesi hizo ni pamoja na zile zinazotokana na uteketezaji wa kemikali hatari na madawa yaliyokwisha muda wake.

Wakati mwingine hatujali hata mashimo tunayoyaacha mara baada ya kumaliza kuchimba madini. Isitoshe hatujui hata tutafanya nini na pengo kubwa litakalobaki ardhini baada ya kuyamaliza maji yote tunayochimba kwa shughuli zetu za kila siku hasa za viwanda kutokana na kutokuwa na mkakati wowote na wenye uwiano wa kurejesha maji tunayoyatoa.

Nashindwa hata kufikiri ni namna gani tunaweza kuiokoa mito yetu inayopokea maji yanayotoka katika mashamba yetu yaliyojaa kemikali na sumu za kila aina zinazotumiwa kila kukicha kwaajili ya kupata mazao bora ukizingatia kuwa mashamba huwa juu na mito huwa chini.Pia unaweza ukatafuta jibu wewe mwenyewe kwamba maji yenye kemikali kutoka viwandani huwa yanakwenda wapi? ,bila shaka ni ardhini na je? ni nani ameshawahi kutushirikisha tumsaidie kuzitoa hizo sumu ardhini ili tuchimbe maji ya kunywa na kwaajili ya kutengeneza bidhaa nyingine tunazokunywa.


Kusudi la kuifanyia dunia ukarabati ni kuhakikisha inabaki katika hali yake ileile ya asili . Ujuzi wetu unapaswa kuhusika moja kwa moja katika uendelezaji wa asili ya dunia au kukarabati uhai wa wake na kama ni vinginevyo huwenda dunia isifae tena kwa maisha na kuwa ni mahala pa shughuli nyingine tofauti na maisha ya binadamu .kumbuka uhai wa dunia ndiyo uhai wa kila kiumbe hai ndani yake kama sisi tutakufa dunia itaendelea kuishi na kama dunia ikifa sisi hatuna uwezo wa kuishi.Ni wazi kuwa kutumia ujuzi wetu kunusuru na kuendeleza maisha ya dunia ndiyo kufanya maisha yetu yazidi  kuendelea juu ya uso wa dunia yenyewe.
(B) MATAMANIO YA BINADAMU
Haya ni matarajio makubwa ya binadamu yenye shauku ya kutaka kuwa na maisha bora na rahisi sana katika kila jambo.kwasababu hii binadamu asiye na tafakari anataka kutumia mbinu rahisi zinazopatikana kwa muda mfupi ili awahi kupata mahitaji yake bila kujali athari za matokeo ya hatua aliyochukua.Inafanana kabisa na mfano wa mwenyenyumba aliyeuza nyumba yake na kwenda kulipia hoteli ya kifahari ambayo alionjeshwa utamu wa usingizi wake siku moja kabla.Aliishi kwa muda na baada ya pesa kuisha kila mtu anafahamu kilichofutia.

2. MUUNDO WA DUNIA NA TABIA ZAKE.
Dunia imeundwa kwa vijenzi vingi ikiwamo
(a) Atmosphere (hewa), inajumuisha gesi zote pamoja na unjevunyevu uliopo juu ya uso wa dunia.Hewa kavu ndiyo inayochukua sehemu kubwa ikiwa na wastani wa 78.09%.Gesi zinazojulikana kuchukua nafasi kubwa juu ya uso wa dunia ni nitrogen 78.084%(78) oxgen 20.946%(21),argon 0.9340%(0.9),carbon dioxide 0.035%(0.03) na nyinginezo zinazochukua nafasi ndogo.Kiasi cha unyevunyevu katika hewa kinachukua wastani wa 1%.hili eneo ndilo lenye kazi kubwa ya kuimarisha uhai wa viumbe pamoja na kufyonza na kuchuja mionzi ya jua hivyo kupunguza makali yake katika uso wa dunia.Kwa ujumla eneo hili linachukua umbali wa hadi km 400 kutoka katika uso wa dunia lakini 80% ya eneo hewa iko ndani ya km16 (10ml) kutoka katika uso wa dunia. 
(b) Hydrosphere (maji) inajumuisha bahari,maziwa ,mito,na maji yaliyokusanyika juu ya uso wa dunia.eneo hili ndilo linalochukua sehemu kubwa ya uso wa dunia kwa kiasi cha 70%.Ni eneo muhimu kwa maisha ya binadamu pamoja na viumbe hai wengine waishio katika uso wa dunia.linasaidia kusharabu 90% ya mionzi ya jua inayotua juu ya uso wa dunia .Eneo hili linasifa kubwa ya kuwa katika mwendo kwa muda wote kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo upepo.
(c) Biosphere (viumbe hai) inajumuisha eneo lote la anga na la uso wa dunia linalokaliwa na viumbe hai.Kwa wastani ni eneo lote linaloanzia 10km kutoka hewani hadi chini kabisa ya bahari.Hili nalo ni muhimu kwa maendeleo ya dunia kwa sababu linawezesha viumbe hai kuishi na ambao ni moja ya nguzo muhimu ya ikologia katika uso wa dunia. 
(d) Lithosphere (tabaka la juu la ardhi) inajumuisha tabaka lote gumu la juu la ardhi na miamba na la chini ya bahari.Linakadiriwa kuwa zaidi ya km 100 kwenda chini.eneo hili linaundwa kwa sehemu kubwa kutokana na mchanganyiko wa oksijeni na silikoni (silicate SiO2) na kemikali nyinginezo ni oksijeni ( oxygen) 46.6% (47),silikoni(silicon) 27.7% (28),alumini (aluminum) 8.1% (8),chuma( iron) 5%,kalisi(calcium) 3.6%(4),sodiamu 2.8%(3),potasiamu 2.6%(3) na magnesi(magnesium) 2.1%(2) .Hili ndilo tabaka jembamba,gumu,kavu,lenye nguvu,lililoshikamana sana,la kunyumbuka kuliko matabaka mengine.
(e) Mesosphere (mentle) (tabaka la kati la ardhi) inajumuisha eneo lote la kati ya lithosphere na barysphere .Lina wastani wa km 2900 kwenda chini na jotoridi kwa wastani wa juu kiasi cha 3000 Centigrade. Kwaasili ni eneo linaloundwa kwa miamba dhaifu yenye mkusanyiko wa oksaidi na salfaidi.
(f) Barysphere (tabaka la chini la ardhi) inajumuisha tabaka la chini kabisa la ardhi .tabaka hili limegawanyika katika sehemu kuu mbili ( dense core) tabaka la ndani lililoshikamana sana na (outer core) tabaka la nje tepetevu. Yote mawili yana wastani wa nusu kipenyo kisichopungua km 3000 kuelekea katika kitovu cha katikati ndani ya dunia.Eneo la nje linawastani wa jotoridi la 3900 Centigrade na la ndani lina wastani wa 4800 Centigrade yote yakiundwa zaidi na kemikali za chuma na nikeli huku la ndani likiwa katika hali ya chembechembe angavu na la nje likiwa katika hali ya utepetevu.

*Ieleweke kuwa kwa asili dunia haina tabia ya kuchukuliana na vitu vyenye kuleta uharibifu dhidi ya vijenzi vyake.
* Dunia haina tabia ya kuchukuliana na taka zozote zinazotokana na uzalishaji wa kubuniwa na binadamu.
*haina tabia ya kushirikiana na vitu visivyokuwa vya asili ila vitu visivyo vya asili huitegemea dunia.
Mwenendo wa dunia unategemea uasilia wa muundo wake na tabia zake. kila kinachoonekana duniani katika hali yake ya asili kinahusika moja kwa moja kuendeleza uhai wa dunia.Sina hakika kuwa mpaka sasa tunaishi katika dunia yenye ulemavu mkubwa kiasi gani, unaotokana na uharibifu wa shughuli za binadamu. pia Inawezekana tunaishi katika dunia iliyokwisha kufa siku nyingi.

Mpaka sasa hakuna anayejishughulisha na kurudisha asili ya maisha ya dunia zaidi ya kuona jitihada kubwa za kupambana na tabia za asili za dunia.Kibaya zaidi unavyozidi kupambana na tabia za asili za dunia ndiyo unaifanya kuwa hatari zaidi kwa siku za usoni.

Katika ujuzi wetu tunaoupata inatupasa kutazama kwa makini kama unahusika katika kuendeleza uhai wa dunia na kama sivyo basi tuna pokea ujuzi batili wenye nguvu ya uharibifu na punde utatulea kihama ambacho hata hatukuwahi kukitarajia wala kukisikia masikioni mwetu.

3. KWANINI MWANADAMU NDIYO MWARIBIFU NA.1 WA DUNIA?
Swali hili lina majibu mengi lakini nitajibu kwa uchache kama ifuatavyo:-
(A) Ni rahisi mno kuharibu kitu chochote kuliko kukiunda au kukirejesha katika hali yake ya asili.

(B) Ameambukizwa uharibifu kutoka kwa waliotangulia.
kila kukicha binadamu anaamka na mawazo mapya ya tengeneza milipuko .tukitazama movie tunaona milipuko,tukitazama taarifa za habari tunaona milipuko ,milipuko katika masherehe makubwa ,milipuko migodini,milipuko jeshini nk.bila shaka hata huyu binadamu atakaye amka kesho naye atakuja na mlipuko mwingine mpya bora kuliko huo wa kwanza.

(C) bidhaa zenye uharibifu zinafaida kubwa ,
umeme utokanao na mitambo ya nyuklia ,viwanda ,magari ya mafuta ya petrol ,uchimbaji wa madini,silaha za kivita kama maroket ,mabomu ya nyuklia nk ,madawa ya kuuwa wadudu,mbolea za mashambani ,madawa ya aina mbalimbali,simu za mikononi na vifaa vingine vya kielectronic ambavyo hata vikichakaa haijulikani vitatupwa wapi na hata vikiangamizwa mabaki ya maangamizi yake haijulikani yanakwenda wapi.

mfano mwaka 2007 mwezi May India iliripotiwa kuangamiza (E-West) yaani electronic west(vifaa chakavu vya kielekroniki) tani zipatazo 146,000 wakati taasisi moja huko Marekani ijulikanayo kama (environmental protection agency) wakala wa utunzaji wa mazingira kama sijakosea Kiswahili chake ikiripoti kuangamizwa kwa computer 600 kilasiku katika mji mmoja tu wa California. Ilibainika kuwa wastani wa 70% ya kemikali zisizotakiwa katika ardhi yake zinatokana na bidhaa hizo ikiwamo (Dioxins) ambayo kwa sehemu kubwa huundwa na chlorine itokanayo na( chloranited plastics PVC)mchanganyiko wa chlorine na plastiki .Katika fact sheet iliyotolewa na shirika la afya duniani (WHO) mwezi may 2010 inadaiwa kuwa kwa tafiti zilizofanywa kemikali hizi zipo kila mahali.Ilielezwa kuwa binadamu ana weza kudhurika zaidi kupitia mafuta yaliyo katika nyama, samaki,na vyakula vilivyo na kemikali hizi ambapo madhara yake ni kupata matatizo ya uzazi ,kansa,mfumo wa kinga ya mwili, na kuingilia homonsi. Hiyo ni kwa mujibu wa miaka kadhaa iliyopita kwa hali itakavyokuwa sasa unaweza ukajijibu mwenyewe.

kwa huku kwetu tumeshuhudia uangamizwaji wa bidhaa feki kila kukicha zikiwamo tvs,cds,redios,subwoofers,dvds deck,nk ambavyo vyote vinahatari kwa ardhi ambayo tunaitumia kwa shughuli za kilasiku.

(D) ujinga wa kutojua wajibu wake.
binadamu ndiye kiumbe pekee mwenye wajibu wa kujibu kila kinachotokea katika dunia na kama si hivyo hakuna maana ya kuwepo kwa binadamu katika dunia.Kupitia ujuzi wako unatakiwa kuhakikisha kuwa unawajibika kwa uhai wa dunia na si familia yako tu kwa kufahamu kuwa, hakuna kiumbe kingine kitakacho tetea uhai na kukarabati uharibifu wa wake zaidi ya binadamu.

Katika kila ujuzi tunaochagua kuufanya kuwa maalumu kwa maisha yetu kunauwezekano wa kuisaidia dunia katika kuimarisha uhai wake na si kama tunavyofahamu au kufundishwa.Tumezoea kusikia kuwa kuna bwana mazingira bwana misitu nk. Lakini hawa hawatembei na mazingra haya na kumgawia kila mtu punde panapokucha na kuyarudisha jioni,bali mazingira haya ni mali yetu sisi na ndiyo tunayoyatumia kufanyia shughuli zetu za kila siku.

kila unaposimama iwe baharini, nchi kavu, angani,chini ya ardhi panakuhusu wewe. Binadamu unayemwona mbele yako yeye ni nyongeza tu katika shughuli nzima ya kuiendeleza uhai wa dunia, lakini aliye muhimu kabisa ni wewe.Wewe ni mjuzi katika kutengeneza simu ya mkononi ,umesha piga picha na kuona mwisho wa hiyo simu? Na je umeshapima matokeo baada ya matumizi yake katika uharibifu wa dunia utakaojitokeza?je umechukua hatua gani baada ya kugundua mapungufu ? muundaji wa( magari ,meli ,boti ,treni,ndege,maroketi,setilites pamoja na mtumiaji, vivyohivyo kwa mrutubishaji wa nyuklia , mtengenezaji wa mbolea ,mchimba madini, maji ardhini ,gesi, mafuta,mkulima unayefyeka misitu na kugeuza mashamba,mfanyabiashara wa bidhaa chakavu ,wajenzi wa majengo marefu na mafupi, mwananchi mkata mkaa,na wengineo , unashughulikiaje swala la uhai wa dunia kupitia huo ujuzi wako?.

Naomba nitamke kuwa ukitaka kuokoa maisha yako yaangamize kwa kuokoa dunia na ukitaka kuyaangamiza yaokoe kwa kuangamiza dunia. Jitihada ya kwanza katika ujuzi tulionao binadamu ni kujitambua kisha kuendeleza uhai wa dunia na si kuibadilisa kama tunavyojaribu kufanya, kwa kuwa kufanya hivyo kutaifanya dunia kuwa kitu kingine kabisa na si kwa matumizi ya binadamu wajao.Ila kwa makusudi! binadamu wakati wa kupasiana ujuzi tunaacha kupasiani jukumu hili kubwa la kuimarisha au kuendeleza uhai wa dunia na badala yake mkakati mkubwa tunauweka juu ya kurahisisha mijongeo ,ulinzi,mawasiliano,upatikanaji wa chakula,mavazi,matibabu,makazi,nk.Sasa ni wakati wa kuwajibika kwa uhai wa dunia, isije ikawa ilishatufia bila sisi kujua na kujikuta tukitumia nguvu kubwa kujiendeleza na baada ya muda ikashindwa kuhimili uharibifu na kutuangamiza sote pamoja nayo.

(E) kurahisisha maisha
Binadamu ndiye kiumbe mwenye shughuli nyingi duniani tofauti na viumbe wengine lakini ndiye anayependa rahisi kuliko viumbe vyote .Hutumia kila kiwezekanacho kila ujuzi kurahisisha kila anachofanya katika maisha yake ya kilasiku. Ikumbukwe kuwa hata kama maisha yatarahisishwa vipi kwa kutumia ujuzi wetu ,lakini kama urahisi huo unatokana na kuharibu sehemu flani ya dunia, basi tujue kuwa hatujarahisisha maisha bali tumeongeza ugumu mara dufu kwa sababu uharibifu wa dunia wa namna moja hujibu kinyume chake kwa namna zaidi ya moja.

Kwa mfano teknologia ya matumizi ya mkaa hapo awali ilionekana kama ni mkombozi wa mwanadamu katika kuhifadhi nishati ya joto. Lakini ili uipate ni lazima uharibu misitu na ukiharibu misitu utakuwa umesababisha kukosekana kwa mvua kutokanako na kukosekana kwa unyevunyevu unaohifadhiwa na misitu na vievile utasababisha kuongezeka kwa hewa ya okaa (caborn dioxide) itakayo zorotesha tabia nchi kwa kupandisha joto hivyo kuathili kilimo kwa kukosa mvua,upatikanaji wa maji,kupoteza wanyama kwa kukosa uoto wa asili, na mengineyo.Bila shaka sisi sote ni mashuhuda wa haya na tunaona dunia inavyoweza kujibu zaidi ya mara moja kwa kosa moja tu la matumizi yetu mabaya ya ujuzi tulionao.

Kwa kuto yatambua hayo tutakuwa tukionyesha wazi kuwa hatujajitambua na kwasababu hiyo hatutatofautiana na mababu wa zamani ambao walihamia huku na kule katika kupigania uhai wao pasipo kujua lolote kuhusu uhai wa dunia, na matokeo yake waliambulia kunyang’anyana rasilimali chache zilizowagawa kwa ujinga wa kutotambua wajibu wao mkuu.
4 . USHAHIDI WA UHARIBIFU WA DUNIA
Kuna ushahidi mkubwa sana wa uharibifu wa dunia unaotokana na matumizi ya ujuzi wa hali ya juu,kati na chini alionao binadamu. Ili nisikuchoshe nitataja maeneo machache yaliyoweza kuharibiwa
(a)   UHARIBIFU WA HEWA
Hewa imeharibiwa kwa namna tofautitofauti na kuleta matokeo ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja kulingana na kiwango cha uharibifu kwa uwiano wa  eneo husika.
Kiwango kikubwa cha uharibifu  wa hewa kimesababiswa na ongezeko la kaboni daioksidi (co2) ambayo kwa takwimu za mwaka 2007 imechangiwa kwa 94% kutokana na mafuta asilia ya petrol ,makaa ya mawe na gesi.Chembechembe nyingine huingia moja kwa moja katika hewa kama ilivyo kwa salfa oksaidi (so2), chembechembe nyingine za ardhi (crustal materials) na chembechembe za kikaboni.

Gesi nyingine hujitengeneza zenyewe katika tabaka la ozoni pale zinapochanganyika na oksijeni kwa kuunguzwa na mionzi ya jua.Sio lengo langu kufundisha ECOLOGIA bali ni kukupa walau ushahidi wa kinachotokea kwa ufupi.

Kwa mtindo huu kumekuwa na gesi aina kadhaa ambazo zimeingia katika hewa na kuifanya kuwa si salama tena ,mfano wa gesi hizo ni:-kwa kiingereza..
CARBON MONOXIDE (CO) huchangia kuzalisha  kaboni dioksaidi na tabaka ozone na madhara yake ni kupunguza kiasi cha oksijeni kinachotakiwa katika mwili, ongezeko la joto na wakati mwingine huleta matatizo ya moyo na maumivu ya kifua .

AMMONIA  (NH3) huchangia ongezeko lake kwenye maji ya mito na maziwa na uharibifu wa madini ya naitreti (nitrate) katika maji ya ardhini.Ikiunganika na baadhi ya kemikali huleta matatizo ya kiafya .

VOLETILE ORGANIC COMPAUND (VOC2) huchangia ongezeko la kabon daioksaidi na kuongeza joto ,tabaka ozone ,madhara kwa tabia nchi , mabadiliko ya mazingira,kansa kwa binadamu na matatizo mengine makubwa ya kiafya.

MERCURY  (Hg) madhara yake hayana tofauti na yale yanayotokana na mchanganyiko wake katika maji kama ilivyoelezwa katika matokeo ya uharibifu wa dunia.

OZONE (03) Huathili ukuaji wa mimea  kwa kuzuia mimea kujitengenezea chakula,pia huzuia kwa kiasi Fulani mimea kupokea kaboni daioksaidi na kuifanya kudhoofika.Kwa binadamu hupelekea kupatwa magonjwa ya mapafu,kukohoa na kupumua kwa shida na athma (asthma)

PARTICULATE MATTER (PM) zinaweza kuathili muundo wa chembechembe za ardhi. Chembechembe kadhaa huakisi mionzi lakini nyingine kama kaboni nyeusi husharabu joto na kuongeza joto duniani.

LEAD (Pb) huharibu mimea na wanyama pori, pia hufanya ongezeko katika ardhi na kuchangia uharibifu wa viumbe ya nchi kavu na majini.
Pamoja na hewa nyingine za sumu zenye madhara kwa binadamu ,zote hutokana na mabadiliko makubwa ya matumizi ya ujuzi wa binadamu.
(b) MAJI
maji yameharibiwa kwa shughuli za kiviwanda
kemikali na madini kama arsenic, mercury, chromium, nickel, barium, cadmium, cobalt, selenium , vanadium, mafuta ya petrol ,cyanides,thiocyanides,phenolic,fluorides(,radioactive substances kemikali zenye mionzi hatari) vimetumika kwa wingi viwandani na wakati mwingine kutiririshwa katika mifereji au mito au ardhini na hivyo kuathiri maji ya ardhini na baharini.kwa Tanzania imewahi kutokea huko North Mara mwaka 2010 wakati ambapo mecury ilitiririswa katika mto kutoka mgodi wa uchimbaji dhahabu na kuharibu maji kabisa.

Huko India ukaguzi wa maeneo yenye viwanda (SUVEY OF INDUSTRIALIZED ZONE) ulionyesha kuwa maziwa makubwa ,vyanzo vya mito mikubwa maji yake hayafai kwa kunywa vile vile katika maeneo ya viwanda maji ya ardhini hayafai kwa matumizi ya kunywa binadamu.Fikiri kuhusu mafuta aina zote yanayomwagika ardhini,baharini na kwingineko yanakwenda wapi.


maji yameharibiwa kutoka majumbani
kutokana na unyunyiziaji wa madawa ya kuua wadudu na vimelea,sabuni na kemikali nyingine tunazotumia kuogea na kusafishia vitu vinginevyo,sumu zinazotumika kuua mbu na wadudu wasumbufu zinyunyiziwazo katika mifereji ya maji taka.Sumu zitokanazo na maji ya kuzima moto ambayo yote huishia ardhini na kuharibu maji , sisi sote tumekuwa mashahidi wa hayo.

maji yameharibiwa kutoka mashambani
kwa kilimo cha kutumia kemikali kama zinc, copper, manganese (Mn),
sulphur (S), iron, (B),chumvi chumvi za phosphates, nitrates, urea, potassium, nk zinafaa kwa kiwango flani lakini kiasi kinachoingia katika maji ni maradufu ya mahitaji ya viumbe hai na kugeuka kuwa hatari kwetu.

Maji yameharibiwa kutoka meneo mengine
Kuna compounds cyanides( zinazopatikana katika sumu za kuua wadudu na wanyama aina ya panya) thiocyanides, phenolic compounds, fluorides, radioactive substances kemikali zenye mionzi hatari kama za uraniamu na kadhalika( mfano huko fukushima Japani), ambazo ni hatari kwa maisha ya binadamu na wanyama zimepatikana katika maji.Matumizi ya kemikali za kuuwa wadudu zimetumika kwa wingi mashambani bila kujali kuwa hata maji yanaathilika aidha kwa kutiririkia mtoni na katika maziwa au kuzama katika ardhi na kuathili maji yaliyo ardhini.

maji yameharibiwa kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari
joto linapoongezeka kina cha bahari kinaongezeka na kina cha bahari kinapoongezeka maji huja ardhini na yakisogea ardhini ardhi hufyonza chumvichumvi kali zilizomo ndani yake na hivyo kuathili kilimo,maji kwa matumizi ya binadamu ,wanyama na mitambo.

(b) Uharibifu wa mali na majengo
Kutokana na mafuriko,majanga ya moto ni matukio ya kawaida kabisa katika kipindi cha miaka 40 iliyopita ambapo zaidi ya visa 100,000 vimeripotiwa ikiwa ni zaidi ya hekta milioni kumi.Hali hii inatokana na ukame ambao husababishwa na kutoweka kwa kiasi kikubwa cha unyevunyevu na ukosefu wa mvua juu ya uso wa dunia.

(c) kushuka kwa tabaka la ardhi (Land subsidence)
tukio hili hutokana na kutoa maji ya ardhini pamoja na gesi kwa muda mrefu mfano katika meneo ya kaskazini mwa Itali Revenna ambayo baada ya vita vya pili vya dunia ilikuwa inashuka kwa kiwango cha 110mm kwa mwaka. Mfano mkubwa wa tukio hili ni mji wa Venice ambao umekuwa na hatari nyingi zinazotokana na kushuka kwa ardhi kunakotokana na utoaji wa maji kwa kiasi kikubwa ardhini. Mbaya zaidi ni kwasababu mji huu uko ufukweni mwa bahari nchini Itali .
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                            











  Matukio kama hayo yameripotiwa katika miji ya Bangkok ambayo katika kipindi cha miongo mitatu tangu mwaka 1978 imeripotiwa kushuka kwa 1m katika maeneo kadhaa.Pia mji wa Kolkata na mingineyo .Nishukuru kwa serikali ya Beijing kwa kuanza kuchukua hatua za kusitisha matumizi ya baadhi ya visima vya maji ya ardhini kama ilivyoripotiwa katika mtandao wa http://europe.chinadaily.com.cn/china/2012-02/28/content_14707333.htm . Tathmini iliyofanywa kupitia mamlaka husika mwaka 2009 zimeonyesha kupitia visima vikubwa vya maji ya ardhini 10,000 vimeweza kufanya ongezeko la ushukaji wa ardhi kwa zaidi ya mm 137 kwa mwaka katika maeneo ya mijini na vijijini Beijing.

5. MATOKEO YA UHALIBIFU WA DUNIA
A. KUONGEZEKA KWA KINA CHA BAHARI
kwa mujibu wa (MILLENNIUM ECOSYSTEM ASSESSMENT) wahanga wakubwa ni wale wanaoishi miji iliyo karibu na bahari .Sababu kubwa ya kuongezeka kwa kina cha bahari ni kutanuka kwa bahari kutokana na kuongezeka kwa joto yaani (themal expansion) wanafizikia wanajua hili wanaweza wakafafanua kwa undani lakini kifupi ni kwamba mada inapopata moto hutanuka.hivyo hata kwa maji ya bahari joto linapoongezeka duniani maji ya bahari huanza kupoteza density yake yaani ule mgandamizo wake hupungua na kuanza kujiachia hivyo kuchukua nafasi kubwa zaidi, na kama hali ya joto itabaki ile ile basi na maji yatabaki katika hali hiyo hiyo mpya hayatarudi katika hali yake ya kwanza, kwasababu hiyo tutashuhudia kuongezeka kwa kiwango cha maji.

IPCC (INTERNETIONAL PANEL ON CLIMATE CHANGE) imewahi kutoa tathmini ya ongezeko la jumla la kina cha bahari la 2cm hadi 7cm katika kipindi cha karne iliyopita kupitia kutanuka kwa bahari (THERMAL EXPANSION).
wakati mwingine kina cha bahari huongezeka kutokana na kuyeyuka kwa barafu kutoka katika maeneo mbalimbali ya dunia kutokana na kuongezeka kwa joto.IPCC imewahi kuripoti ongezeko la 2cm hadi 5cm katika kipindi cha karne iliyopita kupitia ongezeko hili.

(i) Njia nyingine inayosababisha kina cha bahari kionekane kinaongezeka ni ( relative sea level rise)
Ni uwiano  wa kimo cha bahari na ardhi ambapo inaweza kutokea kama bahari ikipanda kutokana na kupanda na kushuka kwa ardhi.Katika maeneo fulani fulani kama maeneo ya mwambao wa Norway na sehemu flani ya kati ya Atlantik katika mwambao wa marekani mashariki.maeneo haya yanatabia ya kupanda na kushuka kutokana na joto. Wakati barafu inapopata moto na kupungua uzito ardhi ya chini hupanda na bahari kuonekana imeshuka na barafu inapoongezeka uzito matokeo huwa kinyume chake.

(II) Matokeo ya kuongezeka kwa kina cha bahari
Tathmini iliyofanywa na IPCC (INTERNETIONAL PANEL ON CLIMATE CHANGE) ni kwamba kina cha bahari kitaongezeka kwa wastani wa 20cm na 86cm ifikapo mwaka 2100 na haitaishia hapo bali ongezeko litaendelea kwa kadri siku zitakavyozidi.

ongezeko la futi moja (30cm) la kina cha bahari linaweza kuathili wastani wa 4500cm (150 futi)kwenda ndani ya ardhi.hii inamaana gani ? ni kwamba maji ya bahari yanapopanda kwa wastani wa futi moja basi yatasogea mbele kiasi ya wastani wa futi 150 ili yaweze kukaa katika utulivu wake wa kawaida na .Endapo yataongezeka kwa 90cm tutegemee kusambaa mara tatu zaidi . Kuendelea kwa kitendo hiki kutapoteza majengo mengi,fukwe nyingi,maeneo ya kuzalia viumbe vingi vinavyozaliana katika fukwe hizo.
Kutokana na utamaduni wa binadamu kupambana na tabia za asili za dunia badala ya kuirejesha dunia katika hali yake ya mwanzo, maeneo mengi ya kingo za fukwe yanajengwa vizuizi vya maji kitu kitakacho pelekea kupotea kwa maandhali nzuri ya fukwe kwa kukosa hali yake ya asili punde maji yatakaposogea katika kingo hizo. Maeneo mengi yameshaathirika tayari.Lakini tutambue kuwa kufanya hivyo ni hatari sana kwa siku za usoni pale maji yatakapofanikiwa kubomoa kingo hizo.
Hatari nyingine ni kwamba kina cha bahari kinapoongezeka uwezekano wa mafuriko yatokanayo na gharika huongezeka .ORGANIZATION FOR ECONOMIC CO-OPERATION AND DEVELOPMENT  2007 (OECD) inataja miji 136 yenye bandari ambayo ina wakaazi zaidi ya milioni moja na iko katika hatari ya kupatwa na mafuriko yatokanayo na gharika.Tathmini za mwaka 2005 kwa miji kumi yenye hatari ya mafuriko iliyo na mali zenye uwezekano wa kupotea kwa mafuriko zenye thamani ya dola 3000 bilioni( $3000 bil ) ambayo ni sawa na wastani wa 5% ya pato lote la dunia kwa wakati huo. Miji hii kumi yenye hatari zaidi ni pamoja na Miami,greater New York,New Orleans,Osaka-kobe, Tokyo, Amsterdam, Rotterdam, Nagoya, Tampa-St Petersburg na Virginia Beach. Miji hii ina kiwango cha 60% ya hatari ya miji yote lakini ikitoka katika nchi kubwa tatu tu: USA, Japan na Netherlands.

(B) KUONGEZEKA KWA JOTO DUNIANI
kwa mujibu wa repoti ya IPCC (INTERNATIONAL PANEL ON CLIMATE CHANGE) 2001ni kwamba joto liliongezeka duniani kwa kiasi cha 0.6 0 C (10 fahrenheit)tangu 1861.Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2100 joto litaongezeka kwa kiasi cha juu cha 5.8 0C.

Pamoja na kuongezeka kwa hewa nyingine hewani kama METHANE,na NITROUS OXIDE lakini kwa asilimia kubwa kuongezeka kwa hewa ya okaa CARBON DIOXIDE ndiko kuliko leta mabadiliko makubwa ya hali joto.Hewa hii huzalishwa kwa njia nyingi haswa zinazotokana na shughuli za kilasiku za binadamu.Shughuli zenyewe zinaweza kuwa ni viwanda ambavyo vingi hutumia nishati ambazo zikiungua huzalisha carbon ambayo inapoingia hewani hujiungamanisha na hewa ya oxygen na kugeuka kuwa carbon dioxide.Vyombo vya usafiri vikiwamo magari yanayoongezeka kila kukicha,na vyombo vingine vya majini na angani, hivi vyote vimekuwa vikichangia ongezeko la CARBON. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na binadamu nae anachangia kuongezeka kwa hewa hii ya okaa bila kuwasahau wanyama .

Hewa hii ya carbon dioxide inatabia ya kusharabu nishati ya joto na kuihifadhi kwa muda kabla ya kuiachilia tena duniani au nje ya dunia hivyo kufanya kiasi cha joto kuongezeka kila baada ya muda.

Matokeo ya kuongezeka kwa joto
kuongezeka kwa kwa kina cha bahari kama ilivyoelezwa awali,kutokana na kuyeyuka kwa barafu au kutanuka kwa bahari.
*kupungua kwa uoto wa asili na ukame
baada ya kuongezeka kwa joto mvua za msimu zimepungua na wakati mwingine kukosekan hali iliyosababisha maeneo mengi kugeuka kuwa jangwa ,misitu ya asili kupungua kama si kwisha kabisa.Mazao mengi hayawezi kustahimili ukame hivyo kusababisha ukosefu wa chakula maeneo mengi.
mafuriko katika baadhi ya maeneo kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari na wakati mwingine mvua zisizokuwa na utaratibu.
*kuyeyuka kwa barafu na hivyo kudhoofisha utalii.Milima kama ya atlas na kilimanyaro ni mifano iliyopungua barafu yake kwa kiasi kikubwa.

(c) KUONGEZEKA KWA MAGONJWA
Kutokana na kuongezeka kwa joto vimelea vingi vinavyoishi kwenye joto vimeweza kuzaliana kwa wingi na kusababisha hali mbaya ya kiafya duniani.Mfano mzuri ni ugonjwa wa malaria ambao unatokana na mbu anyeishi zaidi katika maeneo yenye joto.
Njia nyingine ni magonjwa yatokanayo na matumizi ya kemikali hatari na madini mabalimbali yatumiwayo viwandani na mashambani .Madini na kemikali hizi tunapozinywa au kuzila kwenye maji au katika chakula zimekuwa na madhara makubwa kwa uhai wa binadamu mfano wa kemikali au madini yenye madhara ni kama ifuatavyo:-

ZINC-wastani wa kiwango cha juu kabisa ni kwa mama mjamzito ni 25mg kwa siku ,zaidi ya mg 165 husababisha matatizo ya kibofu,kutapika nk.

COOPER-zaidi ya 470mg ni sumu

BARIUM-zaidi ya 100 mg ni hatari kwa afya ya binadamu

IRON zaidi ya mg 10 katika kila kilogram inaweza kuathili mishipa ya damu,matatizo ya kupumua haraka,presha mbaya ya damu,usingizi,vilevile kuongeza uzalianaji wa bacteria na virusi mwilini ambavyo hutegemea zaidi madini haya kwa maisha yao.

MERCURY ni sumu na zaidi ya mg 100 inaweza kusababisha maumivu ya kichwa,maumivu yasiyo ya kawaida,kuhara,kuharibika kwa chembe nyekundu za damu,matatizo ya ubongo na mfumo wa fahamu,kiharusi,kubadili mfumo wa uzazi,kupoteza kumbukumbu nk.

ARSENIC ni sumu kwa samaki na wanyama na binadamu zaidi ya 25mg inaweza kusababisha kuhara,kutapika,kichefuchefu,kuwashwa kwa pua na koo,kututumka kwa ngozi na hata kifo.Inaweza kusababisha kansa ya ngozi,ini na mapafu na matatizo mengineyo.

KEMIKALI ZENYE MIONZI zinaweza kuharibu tishu za seli za mwili,kuharibu mfumo wa uzazi,ikiwa mama atapatwa na mionzi hii mibaya inaweza kuzuia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa ubongo na tishu zinazohusiana na utengenezaji wa mifupa kwa mototo atakezaliwa.kunamadhala mengine mengi yanayotokana na kemikali nyingi tunazozalisha kwasababu mbalimbali ZA kurahisisha maisha yetu.
6. MASWLI NILIYONAYO JUU YA KINACHOENDELEA DUNIANI
(1) vizazi vinavyokuja vitaikuta dunia iliyohai au itakuwa haifai tena kwa matumizi ya binadamu)
(2) kama dunia haitafaa kwa maisha ya binadamu je tutahamia wapi?(3)kweli kitu kinachoitwa( evolution of man ) mageuk o ya binadamu ni mageuko ya mwili tu au pamoja na fikra? kama ni pamoja na fikra mbona uharibifu bado unaendelea? Na kama ni lazima utokee mbona hakuna marejesho ya kinachoharibika? kama yapo mbona dunia haitambui marejesho hayo? Na kama dunia haitambui marejesho mbona binadamu aliyeendelea anachukua hatua zilezile zinazoshindwa? 
(3) Ni kweli haiwezekani kuiendeleza dunia bila kuiaribu kwa upande mwingine.?
(4)Hii milipuko mikubwa kabisa inayobuniwa kila kukicha na wataalamu wa hali ya juu wanaotufundisha sisi tunaokuja nyuma yao itamlipua nani? Je binadamu? Kama ni binadamu ili abakie nani duniani?la kama si binadamu je ? Ni dunia ? kama ni dunia binadamu atakwenda wapi? Kama ni sehemu tu ya dunia je! wale binadamu waliokosa mahala pao hawatakuja kwetu na kuwa mzigo wetu sote?Kama hawatakuja kwetu je?nani atawahudumia kule waliko wakingali hawana dunia iliyo hai?
(5)hapo mwanzo binadamu aliharibu mimea na wanyama wenzake kwa chakula,kisha akaanza kuharibu miamba na kutengeneza zana za mawe,kisha akaongeza na moto kuchoma misitu kutafuta chakula, kutumia moto akachoma chuma kupata zana bora zaidi,akaongeza na madini mengine kupata vito na mapambo,tukaja na sisi tukaongeza na nyuklia ,kuzalisha umeme milipuko,vipuli nk.,kwa mpango huu wa kuharibu ili kupata kitu tumeharibu bahari ,uoto wa asili,anga,tabia nchi nk kwa kunufaika na viwanda ,mafuta,vyombo vya usafiri nk. ?je vitu hivi havitaisha ? kama vikiisha vizazi vijavyo vitapata wapi cha kuharibu kwaajili ya kuendeleza maisha yao?bado ujuzi huu wa kuaribu hiki kutengeneza kile unatija katika dunia yetu ?bado dunia itaendelea na uhai wake?je tumeshawahi kufikiri kuzalisha bila kuharibu sehemu ya dunia? Kama haiwezekani je?ni bora kuendelea kuharibu na kubaki na dunia iliyokufa au tuboreshe fikra zetu kwanza?kama tunaogopa kuangamia kwa kuzidiwa na mahitaji yanayotuzunguka, kwa uharibifu wa kila kukicha tena kwa kutumia ujuzi wa hali ya juu hatutaangamia kutokana na mrejesho wa dunia kwa uharibifu wetu?

                                   (6) Ufumbuzi
ni wakati sasa wa wanadunia kuamua kwa dhati kuchukua hatua za makusudi kwa kuamua kubadilisha fikra ya kuharibu na kuunda kwa kufikiria kuunda bila kuharibu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni