Ijumaa, 28 Machi 2014

JINSI TUNAVYOWEZA KUTUMIA MITAALA TZ KUKUZA VIPAJI NA.2

Baada ya kutazama katika hatua ya kwanza ya mada yetu ya jinsi ya kukuza vipaji kupitia mitaala yetu sasa twende hatua ya pili katika mtaala wa elimu ya sekondari.

MAENEO AMBAYO NI UFUNGUO WA KUJIFUNZA (KEY LEARNING AREAS)

Mtaala hapa umefafanua maeneo ambayo mwanafunzi ataelimishwa ili aweze kupanua uelewa wake na hivyo kumfanya kuwa na uwezo wa kuamua kuchagua kuendelea na elimu ya juu na fani atakayo.Na ili kuyafanikisha hayo mtaala umetaja maeneo matano ambayo ndiyo kama ufunguo katika kujifunza nayo ni ;-

A.Lugha (languages)
B. Sayansi asilia (Natural science)
C. Teknologia (Technology )
D. Sayansi ya jamii (social science)
E. Biashara na sanaa za ubunifu (business and aesthetics)

Hapa sasa ndipo panapokwenda kujibu maswali mengi yaliyotapakaa katika jamii.Mtaala umefafanua vizuri sana kwa kuainisha kila somo litakalofundishwa shuleni na eneo linalohusika.
Tuanze na ;-

A.LUGHA;

hapa mwanafunzi atafundishwa lugha ya Kiswahili,Kiingereza,kifaransa,na kiarabu.Kupitia lugha mwanafunzi atajenga uwezo na kuimarisha mbinu za mawasiliano na kumfanya kujiamini na kukidhi mahitaji ya nchi na dunia.

B. SAYANSI ASILIA NA TEKNOLOGIA;( NATURAL SCIENCE)
Hapa mwanafunzi atasoma masomo yafuatayo

1.baiologia (Biology)
2. chemia (Chemistry)
3. Fizikia (Physics)
4. Hisabati ( Mathematics)
5 Mawasiliano na masomo ya kompyuta ( Information and Computer Studies)
6. Elimu ya ufundi ( Technical Education)
7. Kilimo (Agriculture)
8. Uchumi wa nyumbani ( Home Economics)

Kupitia masomo haya mwanafunza atapata msingi bora wa kuanza kushirikiana na mazingira yake kwa kutumia miongozo ya kisayasi na kiteknologia.Mwanafunzi ataanza kuunda bidhaa za kitecnologia kupitia mtaala huu wa elimu ya sekondari.Haya yameainishwa katika sehemu ya mtaala huo.

C. SAYANSI YA JAMII (SOCIAL SCIENCE)

Masomo yafuatayo yanahusika hapa-

1.History
2. Geography
3 Civics

Kupitia masomo haya mwanafunzi atapata nafasi ya kujifunza elimu ya uraia,yaani haki na wajibu wake,ataweza kujitambua na kuendana na jamii,uchumi, siasa, utamaduni na mabadiliko ya kiteknologia yanayochukua nafasi ndani ya jamii na nje ya jamii husika.

D. MASOMO YA BIASHARA (BUSINESS STUDIES)

Hapa mwanafunzi atapata fursa ya kujifunza masomo yafuatayo-

1.Commerce
2.Book-keeping

Katika masomo haya mwanafunzi atapatiwa msingi katika maswala ya usimamizi wa maswala ya fedha (financial Management), kupangilia (planning), masoko ( marketing), Manunuzi (purchasing), mahusiano ya jamii ( public relations) na Ujasiriamali (entrepreneurship).

E. SANAA (AESTHETICS)

Mwanafunzi atasoma masomo yafuatayo-

1. Sanaa za uchoraji,uchongaji na ufinyanzi ( Fine Arts)
2. Sanaa za maonyesho (Theatre Arts)
3. Elimu ya viungo na michezo (Physical Education)
4. Muziki ( Music)

Kupitia masomo haya mwanafunzi ataweza kujifunza mambo ya msingi ya kimaisha ikiwa ni pamoja na ya ujumla na yale ya ujuzi wa kipekee ambayo ni ya muhimu sana katika namna mbalimbali za kimaisha.Hii itawatia moyo wanafunzi kuonyesha vipaji vyao na thamani  yake na kuitambua sanaa pamoja na utayari katika maisha yao.maelezo haya yametoka katika sehemu ya maelezo ya mtaala huo ulio katika lugha ya kiingereza.

Pia kuna masomo ya ziada ambayo mwanafunzi anaweza kuyasoma kufuatana na mzingira fulani kwa kadiri atakavyohitaji.Mfano wale wa shule za sekondari za ufundi wanaweza kusoma somo la ENGINEERING SCIENCE wakati masomo ya EDITIONAL MATHEMATIC, BIBLE KNOWLEDGE na ISLAMIC STUDIES, yanaweza kusomwa na mwanafunzi yeyote kutoka katika shule yeyote ya sekondari.

Kwa ufupi ukiutazama mtaala huo japo una mambo mengi ambayo sijapata nafasi ya kuyasemea lakini kwa sehemu hii tu inaonyesha kujibu maswali mengi yaliyokuwa yakiulizwa na wengi.

Wengi wamekuwa wakisahau kuwa elimu ya msingi na sekondari ni elimu ya awali inayomuandaa mwanafunzi ama kuendelea na elimu ya juu au kujitegemea.Vilevile elimu hii lazima iwe na upana katika mfumo unaokidhi mahitaji ya nchi katika kujitegemea na pia kukidhi mahitaji ya dunia.Mwanafunzi awe na uelewa wa mambo yanavyokwenda na mabadiliko yanayotokea duniani kote sio nchini kwake tu.

CHANGAMOTO ZA MITAALA NA UTATUZI WAKE

Pamoja na kwamba hatujapata nafasi ya kuuchambua mtaala wote lakini kwa ujumla kama utapata nafasi ya kuupitia wote uko vizuri.Kinachojitokeza ni changamoto tu za utekelezaji wa mtaala wenyewe.

Maeneo machache yenye changamoto za utekelezaji wa mtaala kwa sasa viko nje ya shule husika watekelezaji wa mtaala na wakati mwingine hata serikali.

Mfano mtaala unapotaja baadhi ya rasilimari wezeshi zitakazotumika katika kutekeleza mtaala utagundua vingi havitekelezeki kwa sasa mfano;-

TEACHING LOAD AND TEACHER STUDENT RATIO (MZIGO WA KUFUNDISHA NA UWIANO WA MWALIMU NA MWANAFUNZI)

Mtaala umefafanua kuwa mwalimu kwa wastani wa juu kabisa atakuwa na vipindi visivyozidi 30 kwa wiki,vipindi visivyopungua sita (6) kwa siku sawa na masaa manne (4) ya kufundisha.Mtaala unatakiwa ufafanue wazi nini cha kufanya endapo kutatokea upungufu na kufanya malengo ya mwalimu kutotimia.

Mtaala umeeleza kuwa mwalimu anatakiwa afundishe idadi ya wanafunzi 40 katika darasa moja jambo ambalo mpaka sasa halijafanikiwa.Kutokana na upungufu mkubwa wa walimu na majengo. mtaala ulitakiwa kutoa mapendekezo juu ya hatua zinazotekelezeka endapo kutatokea upungufu wa walimu.Kufanya hivyo kutasaidia kupunguza tatizo lolote linalosabishwa na upungufu wa walimu,kuliko kusubiri tathmini za mwisho zitakazoamua nini cha kufanya tukiwa tumeshapoteza sehemu kubwa ya wahitimu.

SCHOOL FACILITIES (VIWEZESHI VYA SHULE)

Mtaala umejieleza kuwa rasilimari wezeshi za shule zita toka moja kwa moja selikarini,selikari za miji,na wamiliki wa shule binafsi.Rasirimali wezeshi hizo ni pamoja na;-
PHYISICAL RESOURCES (rasilimali zinazoonekana)

Pametajwa ujenzi wa madarasa,maabara,maktaba,chumba cha mawasiliano (kitakachokuwa na computer,photocopy mashine,fax,internet connection,printing mashine,scanning mashine)mabweni ,jiko na chumba cha matibabu au dispensery kwa shule za bweni.

A . MADARASA

Mtaala umetoa ufafanuzi kuwa chumba cha darasa kinatakiwa kiwe na ubao wa kuandikia , vifaa vya kukalia na kuandikia vilivyotimia.Hili bado ni changamoto na mtaala ungepaswa kutamka wazi kuwa endapo vifaa hivi havitapatikana ni njia gani mbadala inaweza kutumika, kunusuru matokeo yeyote yanayosababishwa na watoto kutokuwa na vifaa vya kukalia na kuandikia.Ninapendekeza kuwa kuanzishwe kodi maalumu kwa watu wote wanaosomesha watoto wao kwenye shule za gharama na nje ya nchi.kodi hii itumike kufidia upungufu utakaojitokeza katika viwezeshi hivyo.Pia wazazi wenye kipato cha kati walazimike kupeleka vifaa hivyo ili vilivyopo vitumike kwa wasiojiweza.Na ukizingatia zoezi hili sio la kila siku basi baada ya muda mfupi tutakuwa tumemaliza tatizo.

B.MAABARA

Maabara imeelezwa kuwa iwe imekamilika ikiwa na vifaa vyote muhimu kwa majaribio ya kisayansi.Maabara hizi hazipatikani kwenye shule nyingi na badala yake napendekeza kuwa maabara za shule jirani zitumike kusaidia wanafunzi wa shule zisizokuwa na maabara.Kuhusu gharama za usafiri kama ni mbali wazazi watachangia kama wanavyochangia kwanye mavazi nk.Hata hivyo shule zinaweza kuwa na miradi ya kujitegemea itakayochangia gharama za usafiri.

C.MAKTABA

Zimetajwa kuwepo kila shule zikiwa na vitabu vyote vya kiada na ziada.mpaka sasa shule nyingi hazina maktaba.Wananchi wahamasishwe kuzijenga kama walivyojenga shule na watu binafsi wapewe fursa ya kuwekeza kama miradi ya kimaendeleo.wanaweza kuwekeza kwa mtindo wa hisa kama mradi wa kijiji au kikundi cha uwekezaji.Watawekeza vitabu kwa kuwalipisha wanafunzi wa shule zinazowazunguka kiasi kidogo cha fedha ikiwa kwa mwaka au hata kwa siku na fedha hiyo itawawezesha kujikwamua kiuchumi.

D. MABWENI NA NYUMBA ZA KULALA WALIMU.

Hayo yametajwa na mitaala kuwa ni muhimu katika shule za bweni.changamoto iliyopo shule hizi ni chache na zilizopo haziko kwenye viwango .Ninapendekeza kuwa wanafunzi wachaguliwe kulingana na mahala wanakotoka.Na utaratibu wa kupata huduma nyingine ambazo hazipo utumike utaratibu ambao nimependekeza awali.

E.KUMBI

Imependekezwa kuwa kuwepo na kumbi zitakazokuwa zikitumika kwa shughuli mchanganyiko .Kwa shule ambazo hazina kumbi napendekeza kuwa zitumie madarasa kwa dharula.


Pia imeelezwa kuwa kumbi hizo zitatumika katika baadhi ya michezo ya ndani.Napendeleza kuwa kuwepo na darasa moja maalumu liyakalokuwa likitumika katika shughuli za michezo ya namna hii ili kukidhi hitaji la wahusika kabla ya kuwa na ukumbi rasmi.

F.VIFAA VYA MAWASILIANO (ICT FACILITIES)

Vifaa kama computer , mashine za fotokopi,scanner,internet,nk navyo vimezingatiwa katika mtaala.Ninachopendekeza vifaa hivi view ni lazima kwa kila shule kutokana na umuhimu wake. Kwa mujibu wa unyeti wa shwala husika ninapendekeza kuwepo na wazabuni watakaokuwa na mkataba na wizara ya elimu kwaajili ya kutoa huduma hii endapo shule itakuwa haina vifaa hivi.

Kitendo cha kuendelea kusubiri pasi na kuchukua hatua ya kupeleka vifaa hivi mashuleni tutaendelea kubaki nyuma kimaendeleo kwa kuwa majirani zetu watatumia mwanya wa ujinga na ushamba wetu kujinufaisha.

Kutumia vifaa hivi vya kisasa kujifunzia na kufundishia ndiyo njia rahisi zaidi ya kijipatia elimu na kuongeza uelewa.Kwa wale wenye uwezo mtaala ueleze wazi kuwa wataruhusiwa kutumia vifaa hivi sawa na kama ambavyo wazazi walivyoruhusiwa kuwanunulia vitabu watoto wao.kufanya hivyo kutajenga mazoea ya matumizi ya vifaa hivi kwa watoto na kuwafanya waongeze uwezo wao wa kuelewa.

Mtaala pia umetaja maswala kadhaa ambayo yanatekelezeka kama maeneo ya kupumzikia,michezo,vyoo kwa wenye mahitaji maalumu, vifaa maalumu kwaajili watoto wenye mahitaji maalumu nk.Kifupi ni kwamba hayo yote yanatekelezeka.mfano;-

A. Maeneo ya mapumziko na michezo

Kwa maeneo ya kupumzikia napendekeza sio lazima yawe majengo bali inaweza kupandwa miti maalumu yenye kivuli cha kutosha na kutumika kwa mapumziko.Katika michezo ninaimani kuwa shule nyingi zinamaeneo ya wazi ambayo yanaweza kutumika kwaajili ya michezo kwa utaratibu maalumu utakaopangwa na shule.

B. Vifaa maalumu kwa wenye mahitaji maalumu .

kwanza watu wenye mahitaji maalumu huwa ni wachache.Hivyo mitaala ieleze wazi kuwa kama serikari haitawapa vifaa maalumu vitatoka wapi kutokana na ulazima wake.

C. Vyoo kwa wenye mahitaji maalumu.

Napendekeza tubadilishe miundombinu ya baadhi ya vile vilivyopo kutatua tatizo la uhitaji wa watu wenye mahitaji maalumu.

Ninaimani kunamambo mengi katika mtaala wa elimu ya sekondari ambayo ni changamoto. lakini tukitumia nia ya dhati ya kuendeleza vipaji vya watoto wetu, tunaweza kutumia changamoto hizo kama daraja na kutafuta mbinu mbadala katika kutekeleza mtaala wetu.
Mfano katika changamoto ya muda wa kujifunza mtaala umeeleza kuwa mwanafunzi atajifunza kwa siku 194 kwa mwaka.kutakuwa na vipindi 40 kwa wiki sawa na vipindi 8 kwa siku.Masaa matano (5) ya kujifunza kilasiku.

 Kwa hesabu za haraka muda huu ni mchache sana kujifunza .Vivyohivyo bado kunasiku dharula zinazofanya wanafunzi wasitumie muda wao vizuri kujifunza.Dharura hizo ni pamoja na upungufu wa walimu,sikukuu za kitaifa,Maradhi kwa walimu na majanga.Ninapendekeza siku ya jumamosi itambuliwe na mitaala na kuongeza siku za kujifunza walau kufikia siku 236.

Sio rahisi kutaja changamoto zote ila tuzitambue kwa faida ya kuboresha mtaala wetu.Ninaimani kuwa tukitumia mtaala kwa kuzingatia rasirimali tulizonazo tunaweza kuendeleza vipaji vya watoto wetu na kuwafanya wawe na mchango katika jamii yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni