Jumamosi, 8 Machi 2014

JE MWANAFUNZI AWEJE ?

Kama wewe ni mwanafunzi wa aina yeyote ile iwe chuo , sec ,au ,msingi hii ni mada muhimu sana kwako. Kama utafanikiwa kuisoma yote na kuifanyia kazi basi utakuwa umepata siri itakayo kufanya uone maajabu katika maisha yako. Itamfanya kila mtu astaajabu pale atakapolinganisha elimu yako na uwezo wa fikra zako kwasababu hautafanana na kiwango unachotazamiwa.

Kuna mambo machache yamesahaulika sana ambayo ndiyo msingi wa maisha tangu shuleni nayo ndiyo yatakayoleta matarajio yako yote kiganjani mwako, bila kujali vikwazo unavyokutana navyo.nami naanza kwa kusema :-

1. JIULIZE UNAFIKIRI NINI?

Tumezoea kuambiwa fikiri kabla ya kutenda bila kuambiwa tufikiri nini.Unafikiri nini ni swali linaloweza kukuchanganya kidogo na kukufanya usielewe nina maana gani.Hapa naomba nitoe ufafanuzi kidogo.

Binadamu anafikiri zaidi kuliko anachotenda ,inamaana tunafikiri vitu vingi mno kuliko vitu tunavyovitenda.Kwasababu hiyo muda mwingi katika siku tunautumia katika kufikiri,hata katika wakati tusioupangilia kufikiri bado tumejikuta tukiutumia kufikiri.Tumefikiri tukiwa darasani ,tumefikiri tukiwa kitandani ,tumefikiri tukiwa tunatembea ,tumefikiri hata tunapokuwa tuko bize kiasi gani .Lakini swali letu linarudi palepale UNAFIKIRI NINI?

Unachofikiri ndicho unachotenda na unachotenda ndicho unachovuna.Mtu aliyekasirika katika fikra zake tunamtambua katika matokeo yake na hata akituonyesha furaha kwa nje bado athari za anachofikiri zitajitokeza na hivyo tutagundua tatizo lake.Hapa ndipo tunapopata picha ya matunda ya kufikiri vibaya kwamba huwezi kutumia muda wako wote kufikiri mpira halafu usizungumze mpira na ukafikiri starehe na usionekane zinakopatikana.
Ikiwa kufikiri ni lazima na kufikiri huambatana na matunda, basi tunapaswa kuwa makini muda wote kujua tunachofikiri .Kufanya hivyo kutanyima fursa ya kufikiri yale yasiyokuwa na tija na kutoa fursa kwa yale yenye mchango kwetu .Mwanafunzi anapaswa kutumia muda wake wote kufikiri kuhusu namna atakavyotumia ujuzi wake katika kufanikisha malengo yake na kuepuka kuutoa muda wake katika kufikiri mambo ambayo yataathiri malengo yake.

2. EPUKA KUFIKRI KIAJALI (accidental thinking)

Mwanafunzi aliyepevuka huwa anapanga cha kufikiri na sio kuruhusu kila kitu kuchukua nafasi katika fikra zake.Jijengee tabia ya kijiuliza unafikiri nini unapoona chochote mbele ya uso wako kiwe kizuri au kibaya. Katika kila unachofikiri unapaswa kukihakiki kuwa kitakuwa na tija katika mustakabali wa elimu au hicho unachokifanya kwa sababu usipofanya hivyo utajikuta kila siku unatoka na matokeo usiyoyatarajia. Wengi wamejikuta wakitumia nguvu nyigi kukaa shuleni au vyuoni lakini wamepata matokeo kidogo mno tofauti na nguvu waliyoitumia kutokana na kupoteza muda mwingi kufiri mambo yasiyokuwa chaguo lao la kwanza.Kwasababu hiyo unapaswa kufikiri kwa USAHIHI.

3. TAMBUA MAISHA HAYAMJUI MWANAFUNZI

Mwanafunzi ni kama mtu mwingine yeyote linapokuja swala la usalama ,jinahi ,chakula,mavazi ,malazi nk.Kwa kutokufahamu hilo wengi wanabaki na mshangao pale maisha yanapokuwa hayatoi ushirikiano kwa binadamu anayeitwa mwanafuni.Wengi wameamua kuacha masomo kwa kufikiri kuwa kikwazo ni ule uwanafunzi wao lakini wanapoacha au kukata tama wanajikuta mambo ndiyo yanakuwa magumu zaidi na baadaye hujutia kwa kupoteza fursa hii adimu.

Katika hili naomba nikupe uelewa Fulani ambao sisi katika enzi zetu hakuna mtu aliyewahi kutupa.kuna mambo kadhaa ya kufahamu yanayokwenda sambamba na mwanafunzi yanayoweza kujibu maswali mengi ya changamoto wanazozipitia.mambo haya ni pamoja na

                                  (a) TAMBUA KILA MTU NI MWANAFUNZI

Mwanafunzi sio wewe tu bali ni kila mtu unayemuona mbele yako.Binadamu wote kila siku tunajifunza na laiti kama tungekuwa tunatakiwa tukae darasani mpaka tujue kilakitu ndiyo tuanze maisha basi hakuna hata mtu mmoja ambaye angekuwa ameanza maisha mpaka sasa, kutokana na utitiri wa mambo ya kujifunza.Kufuatia hilo tunajifunza lakini bado tungali tunaishi.Ondoa fikra kwamba utapata upendeleo wa pekee kwa kuwa wewe ni mwanafunzi hivyo ukabweteka na kusubiri watu wakuamulie kilakitu; wakati mwingine hawataamua kwa usahii.
                                   (b) TUMIA KILA FURSA NJEMA

Unapokuwa mwanafunzi huwa swala la kuchangamkia fursa mbalimbali linakuwa nadra kwa kukosa ufahamu wa kutosha kwa kufikiri kuwa kila kitu kitakuwa sawa utakapomaliza shule/chuo.Fikra hizi ni za uwongo kwa kuwa fursa nyingi hutokea mara moja na hazijirudii.Jiulize kuwa hakuna waimbaji wanafunzi? hakuna wanafunzi wafanya biashara? ,hakuna wanafunzi wakulima? Hakuna wanafunzi wafanyakazi? Vipi kuhusu wewe, unatumiaje fursa zinazojitokeza mbele yako, na kama hazijaja je! ulizifuata kule ziliko?
                                   (c) KAA KWENYE NAFASI

Mwanafunzi mwerevu hujitahidi kukaa kwenye nafasi .Hapa nina maana kuwa uwe makini kudumu katika malengo yako na kujiepusha na makundi au shughuli zozote zitakazofanya kazi ya kukutoa katika malengo yako.Epuka ugomwi ambao mwisho wake ni kifungo,fujo za maandamano mwisho wake kufukuzwa au kifungo ,starehe ,ngono mwisho wake kushindwa darasani na magonjwa .Epuka makundi ambayo hayazungumzii wala kufikiri kuhusu elimu kwasababu watakuambuliza wanachofikiri.Hata kama matokeo hayatakuwa ya moja kwa moja basi yatakuwa sio ya moja kwa moja na yatasababisha upungufu wa matokeo unayoyataraji.

Lengo la kukaa kwenye nafasi ni kuboresha uelewa na ufaulu utakaorahisisha kuendelea mbele na masomo yako kwa wepesi zaidi.Na kadiri unavyoendelea mbele ndivyo unavyozidi kufungua fursa nyingi zaidi.

                                      (d) TAFUTA KUWA MBELE

Mbele ndiko kwenye kilakitu,unapokuwa umewatangulia wezako mbele unapogeuka nyuma wale wote wanaokufuata wanageuka kuwa mtaji na kukurahisishia kazi ya kufanikisha mambo yako.Mfano mtu anayetaka kuwa Rais mara nyingi hujitahidi kuanzisha chama au kutafuta wafuasi kwa njia anazozijua yeye na akishawapata huwashawishi wampigie kura na hatimae kufanikisha malengo yake.

Unaweza ukajiuliza utakaa mbele kivipi? Swali rahisi sana .

Shuleni au chuoni ni uwanja wa wazi kuonyesha kirahisi chochote unachotaka kijulikane.Pima uwezo wako na tafuta udhaifu wa wenzako, wapi unaweza ukafanya zaidi ya wezako na kuwashangaza na kilamtu akakukubali.labda ni katika somo Fulani darasani,kama la! Je? ni katika michezo ,Nidhamu?,utulivu?,uwazi?,usafi? nk.Kufanya hivyo kutawavuta wenzako kwako na kukupa nafasi ya kwanza katika jambo hilo kitu ambacho kitakusaidiwa kukufanya usikilizwe,uheshimiwe,ukubalike na hiyo itakuwa mtaji kwako katika siku za baadaye.

                                       (e) JIFUNZE KUHUSU STADI ZA MAISHA

Mwanafunzi hasa wanafunzi wadogo wamenyanyaswa ,wamesumbuliwa,au kukandamizwa kwasababu ya kutozingatia stadi za maisha.Stadi za maisha ndiyo elimu yote inayohusu maisha na changamoto zake kwa ujumla.Dunia ni kama bahari ambamo samaki mkubwa humla mdogo .Mwanafunzi asiyejifunza stadi za maisha anafananishwa na samaki mdogo ambaye anaweza kuliwa na samaki mkubwa wakati wowote.Inashangaza kuona mtu aliyekuwa anaongoza darasani anakuwa mlevi au anapewa mimba na kukimbiwa.Inawezekanaje mtu mwenye elimu ya chuo anawekwa kinyumba na mama mtu mzima maarufu sugar mamii .Wengi wanatumia udogo wa uelewa wako kujinufaisha bila kujali utaathilika kwa kiasi gani.Hakuna mtu anayeweza kukulinda kuliko unavyoweza kujilinda mwenyewe.

Kupitia stadi za maisha utafahamu kuhusu kinachoendelea duniani mfano;-

* Kupitia kusikiliza taarifa za habari utafahamu hali ya usalama ya nchi na nchi nyinginezo,hali ya njaa au baa lolote na ukubwa wake ,kuingia kwa ugonjwa mpya, nk.Weka katika ratiba yako kusikiliza taarifa na si mziki tu kwasababu kutosikiliza mziki hakuna madhara bali kutosikiliza taarifa kunamadhara.

*Kupitia makongamano ya kijinsia na mengineyo utajifunza kuhusu umuhimu wa kujitambua,faida za kujitambua,haki za msingi za kundi lako,wajibu wako, nk.Tafuta makongamano na semina na mikutano ya hadhara ujielimishe.

*Kupitia majarida , vipeperushi,na magazeti na mtandao utapata habari kwa kina tena kwa muda muafaka tofauti na redio au tv ambapo unaweza kupokea habari wakati usiokuwa tayari na usijue ilianzia wapi. Weka muda maalumu kutafuta habari katika mtandao na si kuchati peke yake.Tazama vipindi vinavyokujenga katika tv na si burudani tu.Tafuta maarifa kwenye gazeti na si habari za michezo tuu na usidharau kipeperushi maana kinakuhusu wewe.

*Kupitia watu waliomaliza elimu ya ujuzi au darasa unalosoma utafahamu faida na changamoto za ujuzi unaouchukua au elimu unayosoma hivyo kukufanya uongeze bidii au ubadilishe uelekeo.Usitumie muda wote kukaa na watu wa kiwango kimoja tu cha elimu maana unahitaji kufahamu kinachoendelea baada ya hapo, kitu kitakachofanya uwe na uelewa mpana zaidi kuliko kiwango ulichokifikia.

*Tafuta kujua watu wa eneo lako wanaishi kwa mtindo upi wa maisha na shughuli gani za kiuchumi ndizo zinazochukua nafasi kubwa.Itakusaidia kujipanga katika kutoa mchango wako na kuboresha endapo kama zana na dhana wanazotumia si sahihi au ni duni.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni