Ijumaa, 31 Januari 2014

MBINU NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI

Ndani ya chumba cha mtihani kuna changamoto nyingi sana tofautitofauti ambazo bila kuzifahamu unaweza kujikuta ukipoteza mtihani wako na kuambulia ziro usiyoitarajia.kwa kufuata maelekezo haya ya mbinu ndani ya chumba cha mtihani utaweza kutoka na matokeo unayoyatarajia.
Zingatia kuwa mara tu uingiapo ndani ya chumba cha mtihani kabla hujauona huo mtihani,kuna matatizo kadhaa ambayo imekuwa kama ni desturi kukutokea.
                (1)    Hofu
Huyu ndiye muuaji mwenyewe anayeweza kukumaliza na kukufanya utoke katika chumba cha mtihani ukiwa hujielewi nini umefanya. Hapa imenichukua muda kufanya utafiti na kutazama wataalamu wa maswala ya hofu wanasemaje, maana hata mimi nimejaribu kufanya kila liwezekanalo kutokuogopa mtihani lakini nikiingia tu, kwenye chumba cha mtihani mambo yako palepale sijui kwako mwenzangu.Ila leo umepata suluhisho la tatizo hili la awali ambalo ndo muuaji na.1 wa jitihada zetu za kielimu.

(A)   UCHAMBUZI WA SHWALA LA HOFU
      (i)                 Hofu ni nini?
      (ii)               Sababu za hofu
      (iii)             Matokeo yanayoletwa na hofu
      (iv)              Jinsi hofu inavyoweza kukumaliza ndani ya chumba cha mtihan
      
       (i)           Hofu ni nini?
         Kwa mujibu wa utafiti wa sayansi ya tiba ya mfumo taarifa wa mwili (link.neurobiology of fear) uliofanyika mpaka sasa naweza kusema,
Ni kitendo cha kuogopa  kinachotokea katika fikra za binadamu au mnyama ambacho hupelekea kujenga hali ya kujihami dhidi ya hatari inayotaka kujitokeza.Hii inaukweli mkubwa sana kwasababu hakuna mahala ambapo pana hatari na mtu asipate hofu.
       Bila shaka ndiyo maana unaweza kuipata hata unapotaka kufanya maamuzi yatakayoamua hatima ya maisha yako ya mbele kama kuugua magonjwa yasiyo na dawa au kufanya mtihani.
                    (ii)  sababu za hofu
Hofu inaweza kusababishwa na mambo mengi sana ili mradi jambo lenyewe liashirie hatima ya hatari .Unaweza kupatwa na hofu kwasababu ya kufanya mtihani ambao utakaoamua hatima ya kisomo chako ikiwa ni uendelee au ubaki,kushiriki mchezo hatari,kupiga penati itakayoamua ushindi wa timu,kupokea taarifa za majibu ya vipimo vya ugonjwa usio na dawa,kugundulika kwa kosa la kijinai ulilofanya ,taarifa za ugonjwa au kifo  kwa mtu unayempenda au kumtegemea nk.

Tambua kuwa kwa binadamu au mnyama hofu ndiyo kinga ya kwanza katika kujihakikishia usalama.unaposhtushwa au kuona hatari. Kinachofanyika ni kwamba hofu hiyo itatumika kama kichocheo cha kushtua vipeleka taarifa  (fear triggers) katika ubongo wako ambapo itaamuliwa bila wewe kupanga (automatically) kwamba mapigo ya moyo yaongezeke,pumzi kupanda na misuli kukaa katika hali ya utayari kwa lolote litakalotokea.
             Hii humuwezesha aliyetishiwa au kushtushwa kuikimbia, kuiruka au kujilinda na hatari inayokuja,hapa ndipo unapoweza kuona faida ya mhemko (emotion) huu wa  hofu .

Kwa wengine ambao hawako sawasawa  huenda mbali zaidi, badala ya kupata faida hizo wao ndo kwanza hupoteza kilakitu na kujikuta wakidhoofika na kuishiwa nguvu.Sipendi nikuache na maswali hii hutokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa kuratibu matokeo yatokanayo na hofu (reguratory system mulfunctions). 
                       (iii)             Matokeo yaletwayo na hofu
Kunamatokeo mengi yanayoletwa na hofu ambayo si rahisi kutaja yote ila nitachukua yale yanayojitokeza zaidi katika chumba cha mtihani

                  (1)    Homa ya mtihani
                  (2)    Kuchanganyikiwa kwa muda  ( temporal mental confusion)

                     (1)homa ya mtihani
Homa husababishwa na mambo mengi unaweza kutazama linki hii kwa undani zaidi lakini homa ya mtihani ni Ile hali inayompata mtu baada ya kupata mshituko wa hofu anapoingia ndani ya chumba cha mtihani.Ni hali ya kujisikia ubaridi na kutetemeka na wakati mwingine kushindwa hata kutulia ndani ya chumba cha mtihani isitoshe hata kushindwa kuandika kabisa au kutoandika vizuri.

Kwa tafiti za kitaalamu inasemekana husababiswa na mabadiliko makubwa na ya haraka katika mwili kuanzia pale uliposhituka ambapo baada ya mchakato flani katika ubongo taarifa hufika katika( linkadrenal grands) nayo huzalisha(linkcortisol) homoni zitakazo kwenda katika damu na pelekea kuamshwa kwa nguvu mpya ya mapigo ya moyo na moyo kuchukua damu nyingi zaidi,kupumua huongezeka kwa mapafu kuhitaji oxgen nyingi na kuisafirisha haraka katika damu,na ongezeko hilo la oxgen huwezesha nguvu au (glucose) kuzalishwa kwa wingi zaidi na kwa haraka.Hali hiyo pia husababisha mwili kupokea nguvu haraka japo kwa wengine inaweza kuwa kinyume chake kama nilivyokwisha eleza awali.
.
Kwasababu hizo inaaminika kuwa katika kipindi hiki cha mwanzo tunaweza kuhisi joto na pengine kutoka jasho na baada ya kipindi kifupi mwili huanza kutafuta kurejea katika kipimo cha jotoridi lake la kawaida na hivyo katika kipindi flani tunaweza kuanza kuhisi baridi na kutetemeka.Hata hivyo hii ni hali ya mpito tu.

     (2)kuchanganjikiwa kwa muda  (link temporal mental confusion )

Hii ni hali inayomkuta mtu kwa upande wa kifikra na kumfanya kushindwa kuchukua maamuzi sahii au kuchukua maamuzi yasiyo sahii juu ya jambo alilolimudu alipokuwa yuko sawa.Tunapomzungumzia kuchanganyikiwa  tunazungumzia swala mtambuka ambalo wataalamu wanaendelea na utafiti ili kuweza kubaini vyanzo vyake na tiba yake.Hofu pia ni kisababishi kikubwa cha kuchanganjikiwa kwa muda na kupoteza kumbukumbu ndani ya chumba cha mtihani.

       (iv) jinsi hofu inavyoweza kukumaliza ndani ya chumba cha mtihani
kama utakuwa huna ufahamu wowote na swala la hofu ndani ya chumba cha mtihani inaweza kukumaliza kirahisi kabisa na kuzifanya jitihada zako zote za kusoma kuwa ni bure.
          Naomba uelewe kuwa hofu ni swala la kimhemko ambalo linatokana na mahusiano mema ya mwili kwa faida ya mwili katika kujilinda na hatari,yaani macho au akili ikigundua hatari taarifa zinasambazwa haraka katika mwili na mwili kuimarishwa haraka kwaajili ya kuchukua hatua stahiki.

      lakini ukumbuke kuwa kuna mambo mengine hata kama yanatia hofu lakini bado yanafaida kwetu, bila kujali hata kama mfumo wa mwili hautambui hilo.Moja ya hayo mambo ambayo pamoja na kushtua lakini yanafaida ni mtihani. Moja ya njia kuu ya kuipunguza hofu kabla ya kuuona mtihani ni kuyatambua mazingira ya ko ya mtihani kwanza kabla ya kuutambua mtihani wenyewe . Na mazingra yenyewe yanayoweza kukuondoa katika mtihani kupitia hofu ni:-

             (a)   kuuogopa mtihani::> wengi huogopa kuwa mtihani utakuwa mgumu na hivyo wataushindwa
.
             (b)  kuogopa kufeli na hivyo kushindwa kuendelea na masomo

Hizo ni sababu kuu mbili zinazoweza kuikaribisha hofu na kukumaliza kabisa ndani ya chumba cha mtihani.
Pamoja na tafiti nyingi ambazo zimeshafanyika lakini mpaka sasa bado hakujapatikana kinga ya hofu  kibailogia, bali zipo njia mbalimbali za kisaikolojia zinazoweza kuondoa hofu lakini si kuizuia maana ni kitendo cha kiautomatiki, yaani kinachotokea bila kupanga .

              (2)  MBINU ZA KUISHINDA HOFU NDANI YA CHUMBA CHA MTIHANI

                   (A)   Tambua kuwa kuogopa ni tabia ya asili ya binadamu hivyo isikuchukulie nafasi kwenye mtihani wako
                   (B)   Kama una hofu ya kushindwa kumbuka kuhusu uwezo wako na namna ulivyokuwa ukifanya vizuri hapo nyuma kabla ya mtihani.Vilevile wanaofeli huwa ni wachache.

                   (C)   Tarajia matokeo sawa na maandalizi yako.Epuka kujenga matarajio makubwa kupita kiasi
Kumbuka kadiri matarajio yanavyokuwa makubwa ndivyo na hofu huongezeka,kwa maana nyingine kubali hata kama utashindwa.Kufanya hivyo hakuta athili chochote katika ufanyaji wa mtihani wako  maana katika chumba cha mtihani hakuna jitihada nyingine zaidi ya kukumbuka ulichosoma na kujibu,hivyo utajibu kutokana na unachokumbuka.

                   (D)   Ondoa fikra potofu kwamba hukuwa unasoma sana kwa hiyo mtihani utakuwa mgumu kwako.Fikra hizo sio sahii kwakuwa mtu hufaulu kutokana na mbinu alizokuwa anatumia kusoma na si kusoma kwa masaa mengi rejea ( link.jinsi ya kusoma kwa kuelewa na kufaulu ).

                    (E)    Tambua kuwa mtihani huo sio wa mwisho hivyo unaweza kuupata mwingine hata kama hutapita awamu hii.
Kutokana na mada yetu kuwa ndefu nimeamua kuikata, awamu inayofuata tutaendelea na mambo ya muhimu ya kuyafanya dhani ya mtihani wenyewe. Nakuomba usikose .
     
 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni