Alhamisi, 24 Aprili 2014

TUACHE UNAFIKI TWENDE SERIKALI MOOOJA.



WEWE Zanzibar unalalamika kuwa mambo ya muungano yanazidi kuongezeka hivyo kuondoa utambulisho (identity) wako .

Swali linakuja kuongeza mambo ya muungano na kupunguza kupi ni kuimarisha muungano?

 katika muungano kupoteza ni lazima ndugu yangu. Hata TANGANYIKA amepoteza vingi  mpaka akafa ndiyo maana unamuona huyo mjomba wenu TANZANIA anamsimamia mambo yake.

kama kila mtu akitaka kung’ang’ania chake ndugu yangu hakuna muungano.Naomba ujitafakari usije kuwa umeanza safari, lakini safari yenyewe ikawa ni kurudi nyuma.Leo ZANZIBAR ukiogopa kumezwa na TANGANYIKA ambaye ni mzimu tuu, ukitoka nje  hautamezwa? ni dhihili kuwa utamezwa na dunia.

Kwa hiyo kitu unachotakiwa kutafakari  ni kwamba, ama uendelee kuutukuza UZANZIBARI na kumfufua binamu yakoTANGANYIKA. Akishafufuka mjadiliane pamoja na Mjomba wenu TANZANIA kupunguza mambo ya muungano  ili asikumeze. Lakini wakati huohuo jiandae kumezwa na dunia.

Najua utasema siwezi kumezwa kwasababu una ndoto.Kama unandoto za kula vizuri na kunenepa kuwa kama  HONG KONG miaka ijayo  ili kuwini uchumi wa dunia.Na kama hiyo ndiyo sababu inayokufanya udai serikali kamili!!.

Basi huyo TANGANYIKA unayemfufua, yeye unayemwogopa akali yu kaburini miaka hamsini huku wewe ukijipasua kwa mizinga 21,bendera,wimbo,nk.Sasa mwenzako atakula sahani moja na wewe,na baada ya miaka hiyo unayohesabu wewe kuwa na tumbo kama HONG KONG, yeye atakuwa na tumbo kama AMERIKA.

Kivyovyote vile safari hii TANGANYIKA hatakua na mchezo,  atakumeza na hatokupa nafasi tena kama ilivyokuwa mwanzo alipokuwa akikumeza kimaluweluwe usishangae, yaani kimzimu mzimu.

Hizi ni salamu zangu za miaka hamsini ya muungano, tutafakari  TANZANIA yetu. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA MUUNGANO WETU.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni